Tunapozungumzia Maneno 'Jamhuri ya Muungano wa Tanzania' Tunamaana Gani Hasa??

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,190
KWA JAMHURI YETU HII YA MUUNGANO WA TANZANIA - HIVI KWELI WANANCHI TU WAKWELI??

Kama mtu anaona ajabu kwa taifa kubwa kama nchi yetu Tanzania ambayo tumeishi kwa zaidi ya miaka 50 BILA YA KATIBA ilioandikwa na wananchi wenyewe basi nikuombe to ukanisaidie jibu la swali langu dogo to hapo chini.

1. Je, katika Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania, ni Zanzibar ndio iko Tanganyika au ni Tanganyika ndio iko Zanzibar???

2. Je, katika kujikumbusha kule sayansi zetu za jikoni pindi tunapopika chai, ukiunganisha glasi mbili za maji na glasi mbili za maziwa na kisha kukolezea majani chai; kile kinachopatkana mwisho wa mapishi hayo ya kimuunganiko itakua ni nini hasa??

a) Ni maziwa yalio na majani chai.
b) Ni maji yalio na majani chai.
c) Ni chai ya maziwa na maji pembeni.
d) Ni chai ya rangi na maziwa pembeni.
e) Ni chai ya rangi (maji pamoja na majani chai basi).
f) Ni chai ya maziwa (maji mchanganyiko na maziwa ikikolezwa majani chai basi).

Je, kwa wale mliowahi kushiriki sayansi ya kupika chai jiko walau hata kwa siku moja tu unafikiri ni jibu gani moja tu ambayo ni sahihi kuliko yote hapo juu??

Sasa, ukiwa umesimama katika vyatu vyake mwenzetu mpika chai hapo juu na tukirudi katika hali ya kawaida unaweza ukaelezea kwamba Jamhuri yetu tuipendayo saaaana ya Muungano wa Tanzania yenyewe itakua inachukua aina gani ya MUUNGANIKO ukipewa

(i) Serikali ya Zanzibar
(ii) Serikali ya Tanganyika na
(iii) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili vile vile ukachanganye madawa???

Kwa jibu lako lolote utakalokua umelipata kutokana na hili zoezi la pili, tukisimama kwenye ukweli unafikiri mambo yamejipandanga vizuri nchini mwetu???

SWALI:

Nawashilisha hoja huku nikiwaulizeni enyi Wana-JF mliosoma sayansi walau hata kwa shule za msingi na kushiriki kupika chai nyumbani wenzetu mnaona nini katika Muungano wetu ambalo watu hua hatudhubutu kuuzungumzia kwa kinywa kipana???
 
This is the hot issue indeed,
...will look forward into it,
 
Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. hivi ndivyo nchi inatakiwa kuitwa.
Lakini ilitakiwa kuitwa Jamhuri ya Tanzania kama Nchi zetu mbili zingejiua na kuwa na nchi moja.
Kwa sasa hatuna jina lililo sawa kwa kuwa kuna nchi moja tu katika muungano. Where is the other?
 
Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. hivi ndivyo nchi inatakiwa kuitwa.
Lakini ilitakiwa kuitwa Jamhuri ya Tanzania kama Nchi zetu mbili zingejiua na kuwa na nchi moja.
Kwa sasa hatuna jina lililo sawa kwa kuwa kuna nchi moja tu katika muungano. Where is the other?

Nashukuru kwamba wachache wenu mliotembelea THREAD hii hapa mtakua mmegundua kwamba hoja iliomo humu ndani NI YA KUFIKIRISHA SANA TENA SANA.

Kutokana na ukweli huu, ni mategemeo yangu ya kwamba Wana-JF watakaodiriki kutembelea hapa na hata kutoa mchango wao kimawazo NI SHARTI TUWATAMBUE KAMA GREAT THINKERS WA KWELI kama ambavyo tunavyojiita humu.

Ukitaka kufaidi katika mjadala wa hoja hii, kwanza usiwe na haraka sana wa kujieleza ovyo ovyo, pili uondoe kabisa chembechembe za KIITIKADI akilini mwako na kuruhusu upande wa KIUCHAMBUZI WA KINA kichwani ifanye kazi bila bugudha. Kama kuna ka-chai jirani rudi mezani and take a cool sip before continuing.

Kwa hoja hii, ni sawa na kusema kwamba tuko katika maabara kutafuta MAJIBU HALISI yaliofichama uvunguni. Hii ni hoja itakayoweza kujadiliwa kwa kipindi kirefu sana.

Ila ukijua ya kwamba wewe ni MVIVU WA KUJIUMIZA KICHWA japo hata kidogo basi bora ukarudi kule kwenye chumba cha tatu kushoto cha JUKWAA LA GOSSIPS.
 
Umewahi kujiuliza ni vipi unaweza kuelezea ujazo wa maji kwenye glasi kama maji hayo yanafikia mstari wa katikati wa glasi? Unaweza kusema glass imejaa nusu au glass imepungua nusu na majibu yote ni sahihi! Tanganyika iko Zanzibar au Zanzibar iko Tanganyika. Jibu lolote ni sahihi kwa sababu hakuna anayejua! Kuhusu Chai katika maziwa na maji...angalau jibu ni Chai ya Maziwa
 
Swala hili sio gumu. Nadhani tukiuelezea mfano wako wa chai kisayansi zaidi yafaa tujikumbushe zile hesabu za seti. Utakumbuka kuna seti yenye memba, seti tupu, ungano na muunganiko. Ngoja, sio lazima ukumbuke kila maana ya kila neno katika hayo. Muhimu unatakiwa ukumbuke kwamba seti mbili zinaweza kuwa na uhusiano (muunganiko) wa aina tatu kutegemea wingi wa memba wanaokuwa katika ungano. Aina ya kwanza ni pale kunapokuwa hakuna mamba katika ungano, yaani kila seti ni seti yenye memba tofauti na seti nyingine. Ungano linakuwa ni seti tupu. Aina ya pili ni muungano wenye memba wachache katika ungano huku kila moja ya seti ikibaki na memba wachache. Aina ya tatu na ya mwisho ya muungano ni pale seti zinapokuwa zimeungana kabisa kiasi memba wote wa kila seti wanakuwa katika ungano. Ukitaka kurahisisha maelezo yangu tumia mchoro wa veni. Kwa maelezo haya nasema muungano wetu uliosukwa sukwa tofauti na misingi hii ya kisayansi ya muunganiko wa vitu hauwezi kudumu milele. Una kasoro ya msingi na ndio maana kero zake sio tu kwamba hazitaisha bali lazima kila siku zitaongezeka. Kila mmoja atakuwa akihisi anaonewa na kupunjwa. Mimi ni kati ya wanaoamini kwamba bila kujali hali ya kisiasa ya Zanziber ilivyokuwa kabla ya muungano (namaanisha mapinduzi na woga wa waliopinduliwa nao kupindua, na hivi kujificha kwenye muungano kwa ajili ya ulinzi) na bila kujali hali tete inayoweza kujitokeza ikiwa Tanganyika itawaachia Pemba na Unguja (mahasimu wa CCM/CUF au waarabu na waafrika au waliopindua na waliopinduliwa au walioelimika na wasioelimika) naona tunahitaji mjadala wa kitaifa kujadili upya muundo wa muungano mmojawapo kati ya aina tatu nilizosema. Hiyo ina maana tuwe na ama serikali mbili - muungano basi, au muungano kwa baadhi ya mambo na kila sehemu moja - bara na zanzibar - wanabakia na serikali, yaani kuwa na serikali tatu au kuunda serikali moja. Kujadili muungano kwa uwazi ndiyo njia pekee itakayouokoa.
 
..tuacheni longolongo.

..Tanganyika na Zanzibar zishirikiane kupitia EAC.

..kuwa na serikali tatu ni kuwabebesha wa-Tanganyika gharama zisizokuwa na ulazima.
 
Your REAL LOVE FOR KNOWLEDGE is recognised at free play on such issues of DIFFICULT BUT POSSIBLE answering the correct way.

Na zaidi nimevutiwa na sehemu za maelezo yako maeneo ambayo yako katika wino mwekundu hapo chini. Kikubwa zaidi, tukumbuke ya kwamba majibu ya swali kwenye hoja hii kamwe haitohesabiwa kukamilika, mbali na kutupeleka kwenye usahihi wa mawazo, hadi pale ambapo jibu kwenye mfano wa mpika chai litakapooanishwa na lile la hali halisi ndani ya nchi yetu.

Nakushukuru mno kwa kuniletea kakipenyo cha mwanga wa mawazo ambayo sikua nayo hapo awali hadi pale niliposoma mchango wako huu hapa jukwaani JF.

Umewahi kujiuliza ni vipi unaweza kuelezea ujazo wa maji kwenye glasi kama maji hayo yanafikia mstari wa katikati wa glasi? Unaweza kusema glass imejaa nusu au glass imepungua nusu na majibu yote ni sahihi! Tanganyika iko Zanzibar au Zanzibar iko Tanganyika. Jibu lolote ni sahihi kwa sababu hakuna anayejua! Kuhusu Chai katika maziwa na maji...angalau jibu ni Chai ya Maziwa
 
jamani, nchi ya tanganyika ndiyo iliyojibadili jina na kujiita JMT na kisha kufanya modifikesheni kidogo juu ya masuala ya pamoja na jirani zao zanzibar yahusuyo fedha, ulinzi, mambo ya nje na mambo ya ndani ili kuimarisha uhuru wa tanganyika na zanzibar amabao ulikuwa unatishiwa na uvamizi wa marekani/uingereza waliotaka kuingilia somalia na baadaye pemba baada ya mapinduzi ya zanzibar lengo likiwa kuanzisaha kambi za kijeshi mashariki mwa afrika (kama ile ya marekani iliyoko saudi arabia kwa ajili ya kudhibiti mambo mashariki ya kati au guantanamo bay iliyoko cuba). inasemekana manuwari za kijeshi za uingereza zilikuwa zimefika mwambao wa mombasa na kama zingeingia pemba/unguja kabla ya muungano, mapinduzi ya zanzibar yangekomeshwa na utawala wa sultani kurejeshwa kwani ndiye aliyekuwa akitambuliwa na UN kama kiongozi halali wa zanzibar.

hivyo muungano ulifanywa haraka kuepusha kurejea usultani visiwani na ndipo mwalimu akaligeuza jina la tanganyika kuwa JMT huku zanziba ikipoteza hadhi ya kuwa nchi kimataifa (sovereignty) na kufutwa uanachama wake katika UN. hatua ya kupotea kwa jina la tanganyika ilichangiwa sana na mwalimu binafsi kulichukia jina la tanganyika na hajaeleza sababu za ulichukia kiasi kile licha ya kuhojiwa mara nyingi. sababu pekee aliyosema ilikuwa eti hata alipowauliza wajerumani jina hili lina maana gani na lilitoka wapi walishindwa kumjibu!

hivyo huu sio muungano wa kawaida kama muungano wa chai katika mfano hapo juu, muungano huu sio wa wazi sana kwa raia wa kawaida, ni siri nzito kwelikweli ambayo ikifunuliwa inaweza kuibua mengi sana. mfano wazanzibari wanaweza kusema karume aliwasaliti na kuliuza taifa lao kwa mwal nyerere
 
Kwa Mtaji huu Waliowahi Kusema Wana-JF hushindia Umbea tu Waombe Radhi

Nilisema tangu mwanzo ya kwamba katika THREAD hii hapa sitegemei sana kama wachangiaji tutakua wengi.

Maana yake ni kwamba hapa ni kuonyesha tu (i) Uwezo wa kufikiri nje ya mipaka ya kiitikadi, Uwezo ya kujenga hoja na kuitetea, (iii) kukosekana kwa nafasi yoyote ya KISHABIKI katika mjadala mzima.

Hakika wale waliowahi kubeza wana-JF kwamba ni watu ambao ni wambea tu wanaoshindia kujadili mambo ya watu, endapo watafanikiwa kufungua mlango huu na kuona kiwango cha utoaji hoja kama Ndugu KAKATI anavyoonekana akishusha mada hapa chini basi kama ni muungwana kiasi chake basi tutakuta ametundika ukutani HOJA YA KUTUOMBA MSAMAHA.

Big up sana KAKATI. Kweli umenikumbusha zile hesabu za BAM kule ma-Form Six miaka hiyooo. Cha kushangaza sana hapa, nilikua nikichukia hisabati lakini uwezo wako wa kuinogesha humu kwa kutumia mifano hai ... mama yangu!!!


Swala hili sio gumu. Nidhani tukiuelezea mfano wako wa chai kisayansi zaidi yafaa tujikumbushe zile hesabu za seti.

Utakumbuka kuna seti yenye memba, seti tupu, ungano na muunganiko. Ngoja, sio lazima ukumbuke kila maana ya kila neno katika hayo. Muhimu unatakiwa ukumbuke kwamba seti mbili zinaweza kuwa na uhusiano (muunganiko) wa aina tatu kutegemea wingi wa memba wanaokuwa katika ungano. Aina ya kwanza ni pale kunapokuwa hakuna mamba katika ungano, yaani kila seti ni seti yenye memba tofauti na seti nyingine. Ungano linakuwa ni seti tupu.

Aina ya pili ni muungano wenye memba wachache katika ungano huku kila moja ya seti ikibaki na memba wachache. Aina ya tatu na ya mwisho ya muungano ni pale seti zinapokuwa zimeungana kabisa kiasi memba wote wa kila seti wanakuwa katika ungano. Ukitaka kurahisisha maelezo yangu tumia mchoro wa veni. Kwa maelezo haya nasema muungano wetu uliosukwa sukwa tofauti na misingi hii ya kisayansi ya muunganiko wa vitu hauwezi kudumu milele.

Una kasoro ya msingi na ndio maana kero zake sio tu kwamba hazitaisha bali lazima kila siku zitaongezeka. Kila mmoja atakuwa akihisi anaonewa na kupunjwa. Mimi ni kati ya wanaoamini kwamba bila kujali hali ya kisiasa ya Zanziber ilivyokuwa kabla ya muungano (namaanisha mapinduzi na woga wa waliopinduliwa nao kupindua, na hivi kujificha kwenye muungano kwa ajili ya ulinzi) na bila kujali hali tete inayoweza kujitokeza ikiwa Tanganyika itawaachia Pemba na Unguja (mahasimu wa CCM/CUF au waarabu na waafrika au waliopindua na waliopinduliwa au walioelimika na wasioelimika) naona tunahitaji mjadala wa kitaifa kujadili upya muundo wa muungano mmojawapo kati ya aina tatu nilizosema.

Hiyo ina maana tuwe na ama serikali mbili - muungano basi, au muungano kwa baadhi ya mambo na kila sehemu moja - bara na zanzibar - wanabakia na serikali, yaani kuwa na serikali tatu au kuunda serikali moja. Kujadili muungano kwa uwazi ndiyo njia pekee itakayouokoa.
 
Mkuu,

Hii habari ya maji, ukichanganya na majani ya chai na maziwa ,mimi naona ni mzunguko. Mimi sayansi ya jiko, ya kupika chai imenipiga chenga. Ninachofahamu mimi ni hivi.

Hapo mwanzo ilikuwapo Tanganyika na Zanzibar
Marais wa nchi hizi,waliamua kuunganisha baadhi ya mambo, mambo yakaitwa mambo ya muungano na pia nchi ikaitwa jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Pia kila nchi ikabaki na mambo yake mengine kivyake vyake.


Rais wa Tanganyika aliona jina hili, Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni refu sana, akatokea muhindi mmoja akamwambia usipate tabu,nitalifupisha, akampatia Tanzania, kwa hiyo, Rais akafurahi akasema sasa Jina lile linalosomeka Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar sasa libadilishwe na liwe Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, pia utaifa uwe Utanzania.

Baadae Tanzania ndio likawa jina lililozoeleka kumaanisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mambo ya muungano yakawa yanaongezeka kila baada ya muda. Lakini hadi leo tunazungumza bado kuna mambo exclusively ya muungano, exclusively ya Tanganyika na Exclusively ya Zanzibar lakini kuna serikali mbili tu, katiba ziko mbili tu, territories ziko mbili tu, Tanzania na Zanzibar. What is wrong in this formula? Did Tanganyika just disappear like that? in the vaccum? You guessed right!

Maeneo ya muungano ni Tanganyika na Zanzibar sio Tanzania bara na Tanzania Visiwani. Ukitaka ku-refer sehemu moja ya Jamhuri wa muungano basi kila sehemu ina jina lake. Moja linajuulikana Zanzibar lakini jengine limesahaulika.

Chukua mfano UK, ina territories zake, England, wales, Scotland, Northern Ireland
Chukua US ina states zake na kila moja ina jina lake.
Chukua Tanzania, Tanzania ni exception, majina ya asili yanapotea, badala yake unapata Tanzania bara na Tanzania visiwani. Do you think I am joking?
Our union is magical. believe me! Tanzania is formed by two parts, one is Tanzania mailand and the other is Tanzania islands. Repeat the lie until it is seen,believed to be true!

Make your own conclusion after some thinking!
 
Nadhani kama ninavyoona unatoa majibu rahisi rahisi kwa kudhani wewe ndiye unaelewa zaidi kuhusu nini ni sahihi mimi najitoa kwenye thread hii na endelea na msimamo wako wa kudhani maji sukari na maziwa vitaleta ukombozi wa kweli nchi hii.
Bila kuuma maneno ni kwamba your wasting our time with useless discussions here.
 
Upo vizuri' naamini katiba mpya itakuwa na jibu sahihi la fumbo hili la woga.
 
Nadhani kama ninavyoona unatoa majibu rahisi rahisi kwa kudhani wewe ndiye unaelewa zaidi kuhusu nini ni sahihi mimi najitoa kwenye thread hii na endelea na msimamo wako wa kudhani maji sukari na maziwa vitaleta ukombozi wa kweli nchi hii.
Bila kuuma maneno ni kwamba your wasting our time with useless discussions here.

Naheshimu sana maoni haya. Ndio maana ya mjadala murua. Wakati mwingine washiriki hugeuka sentimental pia!!
 
Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. hivi ndivyo nchi inatakiwa kuitwa.
Lakini ilitakiwa kuitwa Jamhuri ya Tanzania kama Nchi zetu mbili zingejiua na kuwa na nchi moja.
Kwa sasa hatuna jina lililo sawa kwa kuwa kuna nchi moja tu katika muungano. Where is the other?

Unapenda sana kuchonga!
 
Kwenye katiba mpya, hili litawekwa sawa....Japo swali litaibuka tena, katiba ipi ya bara au ile ya znzb?
Wanzanzibari walishafanyia marekebisho katiba yao, na hivyo katiba ya tanganyika itatakiwa kufatana na ile ya znzbr, la vinginevyo tukaechini kwanza tuone kama huu muungano unatufaa au la, maana wanzeji wakigoma kufanya marekebisho wabara kwenye baadhi ya maeneo watakwama
 
Mzee nimekupata katika hili.

Kwa zaidi, umenitekenya mno kimawazo akilini mwangu kwa hicho kipande cha sentensi kulikokolezwa wino mwekundu hapo.

Nikiendelea kupasoma basi naona kama mapishi yetu ya chai yanatoka kama chai ya rangi na maziwa pembeni hivi na wala bila kuwepo na muunganiko wowote wa pishi zima!!

Na kwa nini iwe hivyo????


Kwenye katiba mpya, hili litawekwa sawa....Japo swali litaibuka tena, katiba ipi ya bara au ile ya znzb?

Wanzanzibari walishafanyia marekebisho katiba yao, na hivyo katiba ya tanganyika itatakiwa kufatana na ile ya znzbr, la vinginevyo tukaechini kwanza tuone kama huu muungano unatufaa au la, maana wanzeji wakigoma kufanya marekebisho wabara kwenye baadhi ya maeneo watakwama
 
The Dreamer, Hakika hii ni falsafa ngumu kweli kweli lakini lina ukweli mkubwa kwetu nchini.


Umewahi kujiuliza ni vipi unaweza kuelezea ujazo wa maji kwenye glasi kama maji hayo yanafikia mstari wa katikati wa glasi? Unaweza kusema glass imejaa nusu au glass imepungua nusu na majibu yote ni sahihi! Tanganyika iko Zanzibar au Zanzibar iko Tanganyika. Jibu lolote ni sahihi kwa sababu hakuna anayejua! Kuhusu Chai katika maziwa na maji...angalau jibu ni Chai ya Maziwa
 
Natamani kupata watu wengi wanajadili suala hili. Hata tukiahirisha vipi tunalo tu!
 
Back
Top Bottom