Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
Ukipata msiba nyumbani kwako siku ya Sikukuu, utaweka Msiba au utafanya sherehe ya sikukuu? Tafakari.
Tunapozungumza maovu ya serikali ya awamu ya tano, kuna watu wanatulazimisha tukae kimya, na wengine wanakuja na visingizio eti, kuna mazuri hatuyaoni.
Wanataka tuongelee Standard Gauge lakini hawataki tuongelee jaribio la kuuawa kwa Tundu Lissu.
Nawauliza; nyumbani kwenu kukitokea msiba siku ya sikukuu, mtaweka msiba au mtapiga muziki na kufurahia sikukuu?
Binafsi mtu anayenilazimisha nizungumze mambo chanya ya serikali hii, wakati kuna mambo mengi yanayotishia ustawi wa Taifa letu, namuona kama jirani anayepiga na kucheza muziki mkubwa nyumbani kwake wakati mimi nina msiba. Ni haki yake kufanya hivyo, lakini kwenye fikra zangu tayari nina jina lake na ninamuweka kwenye kundi analostahili.
Swali! Je! Hayo mazuri ni wajibu au hisani? Reli ya standard Gauge inajengwa kwa mikopo, na hakuna kiongozi atatoa pesa mfukoni mwake. Ni kodi za wananchi na/au misaada ndio vitalipa hiyo mikopo. Vivo hivyo kwa miradi yote inayotumika kujitafutia sifa za uongo na kweli.
Uongozi ni falsafa. Kujenga Taifa sio kujenga 'vitu' bali kujenga watu. Kiongozi atakayestahili sifa ni yule atakayekuja na falsafa ya kuwajenga watanzania ili waweze kujenga nchi yao wenyewe.
Mzalendo yeyote anapaswa kuhoji, kuhoji na kuhoji.
Trilioni 1.5 zipo wapi?
Makinikia yamefikia wapi?
Sukari imeshuka bei?
Wasiojulikana wamejulikana?
Nani amempoteza Ben Saa Nane?
Nani aliagiza kuuawa kwa Tundu Lissu?
Nani aliyemteka Azori Gwanda?
Nani anahusika na mauaji ya Viongozi wa kisiasa?
Nani alimuua Aquilina?
Nani anatamani kuzungumzia ujenzi wa Flyover kabla ya kuzungumzia haya? Nani anataka tucheze muziki wa sikukuu wakati tuna misiba?