Tunapozungumza maovu ya Serikali ya awamu ya tano, kuna watu wanatulazimisha tukae kimya na wengine kuja na visingizio eti kuna mazuri hatuyaoni

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
Ukipata msiba nyumbani kwako siku ya Sikukuu, utaweka Msiba au utafanya sherehe ya sikukuu? Tafakari.

Tunapozungumza maovu ya serikali ya awamu ya tano, kuna watu wanatulazimisha tukae kimya, na wengine wanakuja na visingizio eti, kuna mazuri hatuyaoni.
Wanataka tuongelee Standard Gauge lakini hawataki tuongelee jaribio la kuuawa kwa Tundu Lissu.
Nawauliza; nyumbani kwenu kukitokea msiba siku ya sikukuu, mtaweka msiba au mtapiga muziki na kufurahia sikukuu?

Binafsi mtu anayenilazimisha nizungumze mambo chanya ya serikali hii, wakati kuna mambo mengi yanayotishia ustawi wa Taifa letu, namuona kama jirani anayepiga na kucheza muziki mkubwa nyumbani kwake wakati mimi nina msiba. Ni haki yake kufanya hivyo, lakini kwenye fikra zangu tayari nina jina lake na ninamuweka kwenye kundi analostahili.

Swali! Je! Hayo mazuri ni wajibu au hisani? Reli ya standard Gauge inajengwa kwa mikopo, na hakuna kiongozi atatoa pesa mfukoni mwake. Ni kodi za wananchi na/au misaada ndio vitalipa hiyo mikopo. Vivo hivyo kwa miradi yote inayotumika kujitafutia sifa za uongo na kweli.

Uongozi ni falsafa. Kujenga Taifa sio kujenga 'vitu' bali kujenga watu. Kiongozi atakayestahili sifa ni yule atakayekuja na falsafa ya kuwajenga watanzania ili waweze kujenga nchi yao wenyewe.

Mzalendo yeyote anapaswa kuhoji, kuhoji na kuhoji.

Trilioni 1.5 zipo wapi?
Makinikia yamefikia wapi?
Sukari imeshuka bei?
Wasiojulikana wamejulikana?
Nani amempoteza Ben Saa Nane?
Nani aliagiza kuuawa kwa Tundu Lissu?
Nani aliyemteka Azori Gwanda?
Nani anahusika na mauaji ya Viongozi wa kisiasa?
Nani alimuua Aquilina?

Nani anatamani kuzungumzia ujenzi wa Flyover kabla ya kuzungumzia haya? Nani anataka tucheze muziki wa sikukuu wakati tuna misiba?
 

Bartazar

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
1,031
2,000
Wamelewa madaraka hadi wanafikia kusema chama chao chakavu kinachobebwa kwa mbeleko ya dola kitatawala milele.... Wakati hata dola imara sana ya RUMI ya nyakati hizo haikutawala milele... Kama walivyolewa madaraka akina kaisari Nero
 

Naytsory

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,177
2,000
Haya mambo hayataki ushabiki wa vyama maana ni kwa maslahi ya taifa. Ila wanafiki utawaona wanaanza kubeza. Kisa mtu yupo kwenye green pasture. Lakini kimsingi ni vema Mtanzania kumjali mwenzako na si nafsi yako mwenyewe, maana leo mimi kesho wewe. Kodi tunalipa wote maskini na tajiri, mwenye cheo na asiye na cheo, sasa kwanini tusishirikiane kudhibiti hawa viongozi wetu ambao tuna mamlaka ya kufanya hivyo?
 

magia

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
2,332
2,000
Vijana wa lumumba wale uwezo wao wa kufikiri ni mdogo
Wasameheni bure wako kazini wanakuwa waliopiga propaganda watakula wapi?
Hiyo ndiyo kazi waliyoichagua kama vile mchawi hujali nani anaathirika ilimradi apate riziki yake. Usikute hao wengine wala hawana upendo na CCM lakini kwa vile ni ajira anajitahidi kutoa maneno ya shombo hata ikibidi kufuraia kifo cha mtu.
Maana siku hizi kuna wajamasishaji wa kukodi msibani, wa kukodi wanalia kuliko wafiwa
 

Dudu Baya

Member
Oct 31, 2010
61
125
Mtoa mada kwanini usiombe uraia nchi nyingine yenye kujali zaidi malalamiko yako na kuhamia huko. Tumewachoka kwa kweli Chama cha Demokrasia na Malalamiko.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,556
2,000
Mtoa mada kwanini usiombe uraia nchi nyingine yenye kujali zaidi malalamiko yako na kuhamia huko. Tumewachoka kwa kweli Chama cha Demokrasia na Malalamiko.
Sio mmetuchoka, sema mnajisikia fedheha na mnajione wenye hatia madhambi hayo yakitajwa na ni wazi hata nyinyi vibaraka wa awamu hii hamtaki kusikia hayo matendo yakitamkwa maana sio ya kibinadamu.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,870
2,000
Hoja za wapinzani hazina mguso kwa wananchi wa kawaida
Unazungumzia kupitea kwa Azori Gwanda Rufiji,lakini huzungumzii kuuwawa kinyama watu zaidi ya 200 Rufiji hapo hapo
 

kivyako

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
14,282
2,000
Wanafanya sherehe kwenye msiba, uhai wa mtu wanaufunika kwa miundo mbinu, kila kitu kina mwisho na kuna kujuta baadae, au ndo tuseme tumefunga awamu za serikali??? Thubutu, hata mtu akae miaka 30, kuna serikali ya awamu ya sita itakuja tu! Mamlaka ni vitu vya kupita tena kwa kasi sana
 

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,374
2,000
Maskini.. Makamanda wanatia huruma kiasi hiki ?? Hayo yote mnayosema yameshasikika na kuzoeleka masikioni mwa kila mmoja wetu na hakuna hatua iliyochukuliwa, what is your next move? Inatakiwa kuwe na mkakati mpya wa kuendeleza mapambano vinginevyo upinzani hautakuwa tofauti na mbwa aliyefungwa mnyororo huku akilibwekea linyani linalokula mahindi lakini hawezi kulifukuza wala kuling'ata linyani hilo.
 

Twamo

JF-Expert Member
May 27, 2017
2,361
2,000
Mtoa mada kwanini usiombe uraia nchi nyingine yenye kujali zaidi malalamiko yako na kuhamia huko. Tumewachoka kwa kweli Chama cha Demokrasia na Malalamiko.
Subiri siku moja baba, mama au mtoto wako atekwe au apigwe risasi ndo huo upuuzi na ujinga wako utakutoka! Na nyie ndio wapinga maendeleo ila hamjijui!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom