Tunapouliza Halima Mdee kafanya nini Kawe kwa Miaka yake 10 tujiulize na Sisi kwa 'Kujipendekeza' Kwetu kwa Mamlaka kama 'Wadau' kumetusaidia nini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,545
108,861
Ni 'Akili' ya kawaida tu isiyotaka ujihangaishe sana tu Kujua kuwa Kukaa Kwako Kawe ambako pengine kutokana na 'Unafiki' wako kama 'Mdau' kama hakuna Maendeleo basi haimaanishi kuwa Kawe nzima hakukuwa na Maendeleo. Tena nadhani Mbunge Halima Mdee anastahili Kongole/ Pongezi nyingi tu kwani pamoja na 'Kuandamwa' mara kwa mara na Kesi zisizo na Kichwa, Miguu na Kiuno mara Kusumbuliwa na Spika Ndugai huku akikosa 'Ushirikiano' wa Serikalini lakini bado tu Dada wa Watu ameweza Kujitahidi Jimboni.

Wakati tukiwa ni 'Viherehere' tena tuliojaa 'Unafiki' mwingi leo hii tukiwa tunauliza Halima Mdee kafanya nini ndani ya miaka yake 10 kama Mbunge na Sisi pia tujiulize je, kwa miaka yetu zaidi ya 25 hadi 30 katika 'Tasnia' zetu fulani fulani za 'Kijamii' na Sisi tumefanya lipi la maana ambalo tunavyoelekea 'Uzeeni' sasa Watanzania 'watatuumbuka' na kuonekana uwepo Wetu umeleta Tija na Kuchangia katika Maendeleo ya Taifa letu hili.

Halafu siku zingine tuwe makini na 'Kuhoji' kwetu kwani ni aibu pia kwa Mwanaume mzima mwenye 'Akili' zako tena Baba wa Familia kabisa 'Kuhoji' Ufanisi wa Mwanamke ambaye kwa 'takribani' miaka yake yote Kumi (10) kama Mbunge wa Kawe aliweza Kuchaguliwa na 'Kura' zipatazo 107,989 (2015) wakati wengine kama akina Sisi GENTAMYCINE katika 'Kura' za Utiaji Nia tu pekee 'tumeambulia' Kura Moko (Moja) pamoja na 'Umaarufu' wetu wote Mitandaoni humu (siyo JamiiForums) na Mitaani pia.

Ushauri wa bure tu tukisaidie Chama chetu CCM 'Kushinda' ila 'tukome' kuhoji 'Mafanikio' ya Watu wakati wengine yetu tu Watanzania hawayajui.
 
Hivi mbunge huwa ana "vote" ama huwa anakusanya kodi ktk jimbo lake? Kama jibu ni hapana hili swali "Halima Mdee kafanya nn kwa miaka 10 ktk Jimbo la Kawe msing wake ni nn?

Msingi wake Mkuu ni kwamba aliyeuliza ni Mwanaume katika 'Kutia Nia' tu kapata 'Kura' 1 wakati 'anayemuhoji' Mwanamke alipata 'Kura' Laki Moja.
 
Ni 'Akili' ya kawaida tu isiyotaka ujihangaishe sana tu Kujua kuwa Kukaa Kwako Kawe ambako pengine kutokana na 'Unafiki' wako kama 'Mdau' kama hakuna Maendeleo basi haimaanishi kuwa Kawe nzima hakukuwa na Maendeleo. Tena nadhani Mbunge Halima Mdee anastahili Kongole / Pongezi nyingi tu kwani pamoja na 'Kuandamwa' mara kwa mara na Kesi zisizo na Kichwa, Miguu na Kiuno mara Kusumbuliwa na Spika Ndugai huku akikosa 'Ushirikiano' wa Serikalini lakini bado tu Dada wa Watu ameweza Kujitahidi Jimboni..
Big up!
 
Ni 'Akili' ya kawaida tu isiyotaka ujihangaishe sana tu Kujua kuwa Kukaa Kwako Kawe ambako pengine kutokana na 'Unafiki' wako kama 'Mdau' kama hakuna Maendeleo basi haimaanishi kuwa Kawe nzima hakukuwa na Maendeleo. Tena nadhani Mbunge Halima Mdee anastahili Kongole / Pongezi nyingi tu kwani pamoja na 'Kuandamwa' mara kwa mara na Kesi zisizo na Kichwa, Miguu na Kiuno mara Kusumbuliwa na Spika Ndugai huku akikosa 'Ushirikiano' wa Serikalini lakini bado tu Dada wa Watu ameweza Kujitahidi Jimboni...
Wadau nafikiri tuwe wakweli, pamoja na kuwa kuna mtu alipata kura moko kwenye kura za maoni lakini yeye kama mkazi wa kawe anayo haki ya kuhoji mbunge wake ameleta maendeleo gani?

Haya mengine ya kujipendekeza au yeye ameisaidia vipi Tanzania ni hayahusiani kabisa na alichouliza. Hapa ilitakiwa mumjibu vizuri tu huyu Halima amefanya nini cha kimaendeleo? Tena kwa vielelezo.
 
Back
Top Bottom