Tunapoteza pesa kura za maoni ya katiba mpya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunapoteza pesa kura za maoni ya katiba mpya.

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Wimbo, Oct 30, 2012.

 1. Wimbo

  Wimbo JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2012
  Messages: 376
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kinachonishangaza kura za maoni marumbano ni Uislamu na Ukristo, Waislamu wanataka kadhi kana kwamba kuna aliyewazuia kuwa nao, Madai Mpaka iingie kwenye katiba, wakristo nao wana hofu ya madai hayo kwamba yataleta mbaguano wa kidini ambao kwa miaka khamsini ya uhuru haikuwepo.

  kama wakristo wameandaa waraka wao na kuusambaza kwa waumini wao wote katika mambo ya msingi watakayoyaandika kwenye maoni au kuyasema endapo watapata nafasi na Waislamu vilevile wamesambaza waraka nchi nzima kuna haja gani ya tume kuendelea na mizunguko ya kupoteza pesa na muda?

  katika mikutano hiyo kumekuwepo na ujazaji wa fomu nyingi kwa majina bandia ili kufanya upande furani ushinde upuuzi mtupu! hatutapata katiba yoyote ya maana endapo mfumo ni huo na kama maoni hayo yatazingatiwa.
   
 2. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,746
  Likes Received: 8,007
  Trophy Points: 280
  Wewe toa maoni yako, kususa hakusaidii. Yale ni maoni na sio katiba. Kuna watu mule wanadai haki ya kuruhusiwa kufuga ndevu, kuna watu wanataka polisi waruhusiwe kuvaa hijab n.k, hayo ni maoni tu.

  Na wewe toa yako ila naomba ujikite kwenye mambo muhimu ya kulisaidia taifa badala ya kukaa kulaumu wengine. Kila mtu huongea kwa kadiri ya uwezo wa ubongo wake
   
 3. Wimbo

  Wimbo JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2012
  Messages: 376
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nimekusoma
   
Loading...