Tunapoteza muda kujadili vitu vidogo vidogo mno, tuweni serious tafadhali

Haya mambo hayaendi kwa utashi wala hisia, bunge (wananchi) wamejadili kwa kujiridhisha na kuipitisha.

Bahati nzuri ilikuwa hoja ya mbunge, wala halikuwa wazo la serikali. Wabunge kazi yao, pamoja na mambo mengine…. ni kuishauri serikali.
Hili genge la low IQ waliopelekwa huko Bungeni, unaliita nalo ni Bunge? Nani aliwachagua? Hata ndani ya CCM, hao waliopo huko, robo tatu hawakuchaguliwa na wajumbe ambao ni wawakilishi wa wananchama wa CCM.

Marehemu alipenda kufanya kazi na watu wenye low IQ, wanafiki, ambao hawakuwa na uwezo wa kuhoji wala kukosoa, na hao ndio waliojaa huko bungeni, wakijiita wabunge. Watu wa namna hiyo wanaweza kufikiri na kuamua chochote kinachohitaji uelewa na akili?
 
Ndugu zangu!

It’s too much of pity issues. Imagine kama Taifa tunapiga kelele kupinga tozo za miamala! Jamani?

Uzalendo uko wapi?

Imeshatolewa ufafanuzi kuhusu dhamira ya serikali kukusanya mapato hayo, lakini bado ni kelele ambazo tunajua kabisa hazina faida yoyote.

Bunge limeshapitisha, haikuhitaji mawazo ya kila mwananchi. Na haiwezi kufutwa kwa utaratibu huu, sasa ni nini hiki?

Kama una mawazo mbadala yenye tija basi kuna namna ya kuyawasilisha ili kusaidia vyanzo vya mapato kwa serikali yetu sikivu.

Hebu tuweni siriazi ndugu zangu, kodi ni kwa maendeleo ya Taifa lolote huru.

Kwa kupenda kujadili matukio kila siku litaibuka jipya ili turukie, hakuna lililowahi kufika mwisho.

Inatosha.
Pity na petty ni vitu tofauti.Uzi wako una maana gani mkombe?
 
Mtoa hoja ameleta fikra za kipuuzi. Unaposema suala la tozo ni dogo, unaupima udogo kwa kipimo kipi?

Suala la tozo ni kubwa sana, ndiyo maana hata Serikali imekaa na kutafakari njia zote za kupata hela ikakosa, mahali pekee ilipoona inaweza kuokoa miradi inayoweza kusimama kujengwa, ni kwa kuingiza tozo kwenye miamala.

Unataka kuwahadaa watu kuwa na Serikali imeamua kupata hela kwenye kutoka kwenye jambo dogo?

Kama hujui, chochote kinachoweza kuwagusa wananchi wengi kwa kiasi kikubwa, positively au negatively, ni jambo kubwa.

Sababu nyie wachache mnajifanya hamuoni umuhimu wa kulipa kodi, wakati huo mnahitaji huduma!

Muone aibu, Rais kapigilia msumari hivyo hizi kelele ni mboyoyo tu. Tuwe positive, tutoe kwa moyo.
 
Back
Top Bottom