Tunapoteza imani sisi wenyewe kwa wenyewe

mkandumbwe

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
424
371
Salaaam wakuu.

Nimeona niwashirikishe ninyi katika hili.

Kama wiki mbili zilizopita nikiwa maeneo ya kituo cha mwendokasi shekilango nilikutana na jamaa mmoja (hawa ndugu zetu wanaookota chupa za plastic). Alikua amekaa karibu na mlango wa kuinhilia jirani na mkata tiketi. Alikua anaomba pesa ya maji huku akilalama ana kiu.
Nilishawazoea watoto wa mjini hivyo nikampuuza nikiamini ni walewale wasiotaka kufanya kazi wakitegemea kuomba, lakini nilipompita kama hatua kadhaa nikatafakari na nikaona hapana inaweza kuwa kweli huyu bwana ameshikika sababu anaonekana si ombaomba bali ni mtu aliyejiajiri kuokota chupa ila mambo yamekua magumu leo.
Nikapatwa imani nikampa 5000 nikitegemea itamtosha si kwa maji tu bali hata mlo mmoja.

Cha kustaajabu, baada ya kumpa 5000 jamaa aliendelea kukaa tena palepale akiendelea na wimbo wake ule ule wa kuomba maji.

Niliumia lakini nikawa sina namna nikaachana nae huku nikiwa nimepata funzo.

Jana tena nikiwa mitaa ya msimbazi polisi tena katika kituo cha mwendokasi nikakutana na bwana yuko karibu kabisa na mkata tiketi. Mkononi ameshika 200 huku akilalama kuomba msaada mtu wa kumuongezea ile 200 yake iliapate tiketi alisema anaenda kimara.

This time nikasema sifanyi makosa niliyofanya wiki 2 zilizopita...nilichofanya nikamwambia anipe ile 200 yake..nikaongeza na 1100 ikawa 1300 nikanunua tiketi 2; moja yangu na moja ya yule bwana.
Huku nimijifariji nikaona nimemsaidia mtu.

Unajua nn kilitokea??

Ile nampa tiketi yake tu jamaa akabaki palepale, tena ile tiketi akaiuza muda ule ule kwa abiria waliokua wamepanga foleni. Akaingia tena mfukoni akatoa 200 nyingine akaendelea na wimbo wake wa kuomba msaada aongezewe nauli.

My take;
Kwa mwendo huu si tunaweza kuwaacha watu katika shida bila kuwasaidia tukidhani labda nao ni matapeli.

Tunaharibiana wenyewe kwa wenyewe hata tutakosa imani ya kusaidia wenye mahitaji.
 
Back
Top Bottom