Tunaposujudu Sanamu...na Kuzitoa Zaka...

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,520
Sanamu inaweza kuwa ni picha, kinyago,kikaragosi au kitu tuu kinachofurahisha, kukonga moyo na hata kujenga imani ambayo huwa ni vigumu kubadilika.

Nawaangalia Watanzania wengi waliopoteza haki yao ya kuwa huru kwa kusujudu sanamu na kufurahia uzuri wa sura iliyokonga mioyo yao, kiasi cha kusujudu na kuamini kila sarufi, kiambishi, kiunganishi, kivumishi, neno, ahadi na hata tungo zilizojaa matumaini ya bandia zilizotoka kinywani kwa huyu anayeabudiwa na kusujudiwa.

Yawezekana ni limbwata au ulevi wa gongo, mirungi au kule kuelea baada ya kupata msokoto wa bangi ambako hufikia mtu kufanya mambo yasiyoeleweka kwa watu wenye akili zao timamu na hivyo hisia kuwa huyu aliyelewa au kupumbazwa hanazo huongezeka.

Lakini, waliolewa kilevi ni wasomi, wenye taaluma, upeo na uwezo wa kukokotoa kati ya shayiri na mtama. Na ni hawa ambao huwapa tumaini butu na bubu wale wengi ambao elimu yao ya haki zao kikatiba imefunikwa na gamba la furukombe nao huishia kushangilia kulishwa makombo na kutolea zaka sanamu.

Inastaajabisha na kushangaza wimbi na wingu la wanaosujudu Sanamu na kuitolea Zaka wanavyopiga vifua vyao makonde ya kujenga hisia chanya za mapenzi yasiyo na kikomo, kuwa sasa Amani na utimilizi wa njozi zao unatimia. Hata machozi ya furaha na makamasi yanawatoka kwa kurukwa na fahamu za kufurahia uzuri wa taswira na umaridadi wa kinyago wanachokiabudu na kukitukuza.

Tena kwa nyenzo za hali ya juu, kwa hali na mali kwa ushirika wamekubali na kuenzi Sanamu na kuiabudu, kuisujudu wakiipigia magori na wakiwa tayari kutoa uhai wao kuitetea sanamu. Wanahubiri uzuri wa sanamu yao, kusifia ilivyo na haiba ya kutamanisha na jinsi inavyowafurahisha mithili ya kikaragosi kinachoutwa kamba na kunyanya mabega na kifua na kupumbaza watu na kuwa kichekesho.

Kwa udi na vumba hawa ndugu wamesujudu na kutukuza Sanamu na kuifanya Mungu wao. Wanapita kila kona ya himaya wakihubiri habari za kusifia sanamu yao na kuipamba kwa manukato na mafuta ya uto.

Wala si kwa masikhara, ni wakali mno wakiitetea Sanamu yao na kuibeba juu na ukikataa kuisujudu, nafsi yako hupigwa mhuri wa kuwa msaliti na mchokozi usiyependa Kushikamana na nduguzo ambao kwao wao, Sanamu ni tumaini la maisha mema.

Utulivu wao huja kwa kuirembesha Sanamu na kuipa uhai bandia ambao wanautembeza kila mtaa na kona na kudai kila mtu aisujudu Sanamu ili neema ijae katika Maisha ya mtazamaji na mwabudu sanamu naye kugeuka kuwa muumini Bora.

Lakini wanasahau, sanamu ni sanamu, haina uwezo wa kuwa na fahamu, imechongwa, imependezeshwa lakini haina uhai binafsi wa kujirembesha wala kujiuza. Imechongwa na aliyepata maono na kuona haja ya kuuza Sanamu hii kama Imani.

Sanamu hii inayosujudiwa, si Mungu, bali inalazimishwa iabudiwe kuwa Mungu ambaye aliumba dunia kutokana na kazi yake na uwezo wake wa kufikiri na uumbaji. Lakini wanayoipenda Sanamu na hata kudiriki kudai wao ni wamiliki, wanashurtisha kila mtu apige goti, atoe zaka na kuahidi kula kiapo cha utii kuisujudu na kuitumikia Sanamu, ilhali Sanamu imekaa kama mlima au kifusi cha mchanga kisicho na uhai wowote.

Ajabu, hawa wanaoipaka manukato Sanamu hii ili inukie na kuvutia, wameshindwa kuoonyesha mazao ya kweli ya sadaka na sala zao za maombi kutoka kwa Sanamu. Wanaamini tukiendelea kuitazama Sanamu kwa kukazia macho kwa nguvu na kuendelea kuisujudu kwa kasi, basi ari ya kuwa na wokovu itatimia na hovyo wote tunapaswa kuamini wanachokiamini.

Najiuliza, ni ulevi gani huu wa kupindukia wa kuamini kuwa Sanamu yaweza leta uhai? Je hata ikirembwa namna gani, si bado ni Sanamu na kamwe haiwezi yenyewe kuwa na Uhai wa kweli wa kuamsha mioyo na kuihamasisha?

Sasa kwa nini kama yule mlevi wa pombe ya Pingu tulazimike kuishangilia, kuiabudu na kuipigia magoti kama si kuanguka kifudifudi kuitukuza na kuisujudu Sanamu huku tukitoa zaka za haki yetu kuifanya Sanamu Mungu?

Kuna dhambi gani kuikataa Sanamu au kukataa kuburuzwa na makuhani wanaolazimisha Ibada ya kafara na kuisujudu Sanamu?
 
Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
65,930
89,013
Hapa unawazungumzia watu gani wanaoabudu sanamu? Hebu kuwa muwazi kidogo.
 
Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,467
1,164
Rev. this is a bit philosophical, I'll read it again though I think kiasi nimeelewa...............
 
DoubleOSeven

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
661
132

............... the agony of a very dark country, darkness in the mindset of the supposedly faithful, stalwarts and what have you. The agony of profound uswahili (that thing of no-good doers, con artistry, fulani kasema..., laziness, illiteracy, practice and belief in jujumen and the Sheikh Hayahayas etc etc not forgetting UVIVU wa kufikiri! Bootlicking as well.

Bootlickers hawawezi KUKATAA sanamu. Wanajua fika kwamba kwa kusujudu wanafaidika na nini, potelea mbali anaumia nani kwa usaliti huo!

e pluribus unum!
 
Akthoo

JF-Expert Member
Nov 5, 2007
953
933
Rev. bila shaka huo ni Mwenge wa Uhuru!!!
Unaodaiwa kuleta umoja, amani na utulivu kwa kuukimbiza nchi nzima! Au...
 
Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,520
............... the agony of a very dark country, darkness in the mindset of the supposedly faithful, stalwarts and what have you. The agony of profound uswahili (that thing of no-good doers, con artistry, fulani kasema..., laziness, illiteracy, practice and belief in jujumen and the Sheikh Hayahayas etc etc not forgetting UVIVU wa kufikiri! Bootlicking as well.

Bootlickers hawawezi KUKATAA sanamu. Wanajua fika kwamba kwa kusujudu wanafaidika na nini, potelea mbali anaumia nani kwa usaliti huo!

e pluribus unum!

Comrade, you said it well...
 
Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,615
Rev. Kishoka Usisahau kwamba MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO - Akisema Nyani Ngabu wepesi wa kubisha..
 
X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,624
1,768
Hii pia ni ibada ya msingi katika nchi nyingi za Kiafrika ambapo sala za waumini wake huwa hazitimii bila ya kuomba na kuabudu masanamu. Masanamu yanayohusishwa zaidi katika ibada hizo ni pamoja na sanamu la Kiongozi mkuu, na wasaidizi wake pamoja na familia ya ilo sanamu kuu. Hii inatokana na kutojitambuwa kwa wananchi kuwa wana nguvu kubwa sana za kuamua hatima yao...!

Kwenye baadhi ya maandiko tunasoma hivi:

"...Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao"

Inawezekana sababu za umaskini na kutojitambua zimesababishwa na hao wasomi ambao kwa usomi wao walitarajiwa kufanyakazi ya ziada kuamsha umma mzima wa waabudu sanamu, ili wapate kujitambua na kukataa ikiwa kwa hiyari au kwa nguvu kuabudu icho wanacho kiabudu sasa.

Nachelea kusema kuwa inawezekana adhabu ya Mungu Mwenyezi ya kuwapatiliza vizazi na vizazi imewakumba hawa waabudu sanamu.
 
Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,520
X-Paster,

Umejenga hoja nzuri sana kuonyesha relation ya kuabudu sanamu na umasikini wetu. Ni lini basi watu watang'amua kuwa sanamu hii haileti neema?
 
Gurta

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
2,238
530
X-Paster,

Umejenga hoja nzuri sana kuonyesha relation ya kuabudu sanamu na umasikini wetu. Ni lini basi watu watang'amua kuwa sanamu hii haileti neema?

sanamu yenyewe ni kubwa m, nzuru na imewekwa mahali pukuu. Inaonekana na kila mwabudu, inavutia. Makuhani wake ni werevu, wamekwisha tuaminisha hivyo. Bila kusahau woga kuacha, kuna wakati sanamu hutoa miujiza yake. Kila mmoja anatamani, anasubiri.
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,620
5,564
Naam, ambao hawakujua Insha hawawezi kujua imra!! ambao hawakujua kuzidisha kamwe hawatogawanya!!! LAZIMA FIKRA ZIFANYE KAZI PEVU KUPAMBANUA. GREAT
 
Azimio Jipya

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
3,363
1,117
Nina tatizo na sanamu yenyewe!

Ndio!.. waumini wa sanamu ni tatizo..lakini mimi ninatatizo na sanamu yenyewe kwani ni tatizo zaidi!

Ingekuwa imejengwa na kisiki cha mpingo... ingekuwa gheri... kwani: kuiona tungewatoza vijisenti..watalii wa Italia na marekani na wanetu wangapata mapeni ya kwendea shule..na kulipia tiba huko kwa Bwana mganga...lakini si hivyo..

Nina Tatizo na sanamu yenyewe... na si wafanya ibada...

Sanamu ya damu na nyama sio ya mpingo wa porini...yatembea...yapanda na kuteremka...madege na magari huko majuu!

Sanamu ina kiu, ...kiu kuu ya kuabudiwa... hata kwa gharama yeyote...kwa wataalam haka ni kaugonjwa ..jina la kitaalamu silikumbuki... Sanamu Yapenda na imejengwa kuwa na hamu na kiu kali ya kusujudiwa...imewapumbazi maelfu na malaki kwa peremende kijiti...ili waiabudu na ifikie lengo kuu la miaka takribani kumi ...katika kuambudiwa..!..Na nikweli nasikia shangwe kuu zikitoka kila upande...Sanamu imedanganya na wamedanganyika...imepata ibada ya kuabudiwa..iliyofaraja ya miungu yote ya kisanamu..

Sanamu...! yakaa kwenye kiti cha enzi... Yaimba...Kwa sauti ya juu na kali kabisa..

Mungu ibariki..Tanzania...

Yapaaaza sauti hadi majirani wanasikia...waja kujumuika...Mugabe alikuwako, Kibaki, Xuma, na...na...

Tatizo langu....kuuimba mwimbo mtukufu wa Taifa...Unaotamka MUNGU..

Nani ni mungu hapo? sanamu au Maulana mweneywe?.. muumba wa Mwanzo na mwisho wa vyote?

Nina taarifa..tangu utotoni..kuwa Neno hili MUNGU ni kuu lipitalo yote...

Iweje sanamu ijilingalishe nalo..alafu .... Inavikwa utukufu wa Mizinga 21..na mwimbo wa MUNGU...IBARIKI TZ...NA AFRIKA PIA!!!?

Hii Ni kufuru... Taifa kuingizwa kwenye giza kuu...giza tororo...waumini wafanya ibada wala hawaonani..wanapapasa..hawaoni, hawana maono..ndani ya Taifa lao wenyewe...hah hah..sanamu na makuhani yachekelea..! Tulikuwa na maadui 4 wa Taifa lakini kwa kicheko hicho maadui..waongezeka..udini...ukabila..maadui wafika sita sita kimchemchezo..!!

Taifa...linaongozwa na giza lililo ijenga na kuipa sanamu utukufu...na kila mwibo huu mkuu ukipigwa..na sanamu ikiimba..Mungu ibariki T...Ah! Ghadhabu ya Mungu Mkuu..inaogezeka juu ya Taifa... Mafisadi..waongezeka...Upendo unapungua..haki inakimbia Taifa, kura zinajibadilisha kwenye masanduku ya kura, NEC inaona kulia ni kushoto na kushoto ni kulia, aliyeshinda kawa mshindwa na mshindwa kawa..ahhh..kisa...Sanamu iliyokalia kiti cha enzi..imejifanya mungu..sanamu.... sanamu..sanamu wee!

Mungu wa kweli twaa Taifa lako kwa Maujanja yako tusiyojajua....muonyeshe sanamu ukuu na utukufu wako ... na kuwa MUNGU HADHIHAKIWI na vijisanamu vya mpingo wa porini!
 
mnyikungu

JF-Expert Member
Jul 26, 2009
1,946
2,438
Naam na tazama watu wakiiabudu hiyo sanamu mara ghafla MUSA anakuja na kanuni na sheria ili watu wasiabudu tena hiyo sanamu.ona wanaabudu sanamu pasipokujua kwa nini wanaabudu sanamu,wengi wao wanaabudu sababu baba zao wamewarithisha kuiabudu, wengine wanaabudu kwa sababu hawajaona kitu kingine cha kuabudu zaidi ya hiyo sanamu.LAKINI MKOMBOZI WA KWELI MUSA AMEKUJA/ATAKUJA KUIBADIRISHA MIOYO NA FIKRA ZA WATU NAO PIA WATAACHA KUISUJUDU HIYO SANAMU KWANI WATAONYESHWA NA KUFUNDISHWA NINI WAABUDU.
AMANI IWE NANYI
 
Kinyau

JF-Expert Member
Nov 24, 2006
907
680
Ubaya wa sanamu hii haitoi hata asante
hata ukijipitisha hupati hata mkate
uabudu, usujudu kwake yeye si lolote
mwisho wake utachoka na neema usipate

macho yao hayaoni kuwa hilo bovu gogo
akili zimewaganda kwa kujaziwa uongo
mawazo yamewajaa nakuwaletea msongo
ni kwa nini hawaoni hii sanamu ya uongo?

Sanamu hii inazidi kuwapeleka kuzimu
ni kama baya jinamizi linaloleta wazimu
mambo yake ni hatari kama nyoka mwenye sumu
ni kwa nini hawoni ubaya wa hili zimwi?

Nawalilia waamini waloichagua sanamu
wamefungwa kila kona , kwao kesho si muhimu
wanatembea gizani kwa vicheko kemukemu
ni kwa nini hawoni ubaya wa hili zimwi?

Nakulilia mwanangu sanamu itakuponza
nakulilia rafiki furaha yako itaoza
nakulilia jirani maisha kwako ni kiza
naililia jamii kwa kutoswa kama pweza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom