Tunaposheherekea miaka takribani 50 ya uhuru wa Tanganyika, tunajivunia nini?

Je, uhuru tulioupata mwaka 1961 umetusaidia kujikwamua na maadui watatu?

  • Ndiyo

    Votes: 1 6.7%
  • Hapana

    Votes: 14 93.3%

  • Total voters
    15

Keynes

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
533
89
Tarehe 9 disemba kama kawaida tutaalikwa pale uwanja wa taifa kwenda kusheherekea sikukuu ya uhuru na kuangalia ndege za mitumba za jeshi kutoka nchi za magharibi tukiwa na mafanikio yafuatayo

  1. UMEME - ni asilimia 14% tu ya watanzania milion 40 wanapata umeme ambao pia ni wa mgao
  2. MAJI- Ni asilimia 55% tu ya watanzania wanapata huduma ya maji safi
  3. AFYA- mhudumu mmoja wa afya anatakiwa kuhudumia watu laki 1 na pia kitanda kimoja cha hospitali kinatakiwa kulaza watu 1,500
  4. ELIMU- Asilimia 30% ya watanzania wenye umri wa kwenda shule hawajui kusoma wala kuandika
  5. KIPATO- Hakuna ajira..ni asilimia 30% ya watanzania tu wanaofanya kazi katika sekta iliyo rasmi
  6. VIWANDA- kwa asilimia 95% tunatengeneza tusivyonunua na kununua tusivyo tengeneza.
  7. MISAADA- Asilimia 35% ya bajeti ya serikali inategemea misaada kutoka nje.

Je tumlaumu nani? Au tukadai uhuru Upya?
 
Mkuu,

Tunasherehekea uhuru wa nchi gani?

Tunasherehekea!!?? au Tunaomboleza kuipoteza nchi yetu?

Tusitishe sherehe hizi kwanza hadi pale tutakapoirejesha nchi yetu kwanza?

sisi wenyewe tunaona haya kutaja jina la nchi yetu..kujivunia utaifa wetu!!! Tumekuwa watu wa ajabu kweli hapa duniani. Hatujijuwi hatujitambuwi. Tumo tu!!!

Kama umelisahau jina la nchi yetu au kama umezaliwa baada ya 1964 itakubidi umtafute Mchungaji Mtikila atakusaidia jibu.

Usijiunge tu katika mkumbo wa kusherehekea usichokijuwa. usipoteze muda wako kwenda uwanja wa Taifa kuangalia mchezo wa kuigiza/maigizo.

Tuimbe kwa pamoja tafadhali!

Tanganyika, Tanganyikaaaaaaaaa!!!!
Tanganyika nakupenda kwa moyo woteeeee.
Tanganyika nchi yangu, Nchi ya mwitu na njika nakupenda kwa moyo wote!!! Machozi yanimwaika ninapokuwaza wewe!!

Ahsanteni.

Kuna siku tutakupulizia uhai tena. Haya hima Wadanganjika!!! Tudai katiba mpya na tuupitie tena mkataba wa Muungano wa Jamhuri ya Tan(nganyika) na Zan(zibar). Hii -ia- tumzawadie Jaji Warioba. Mwenyewe Mwalimu ndiyo hatunae tena!! Yalimtosha haya ya Tanzania akajiondokea zake, mzee wa watu. Ametuachia sisi mradi wa "white elephant" amabao unatutowa roho. Hatuelewani. Hatufahamiani.

On a serious note wanaJF, ni lazima atokee mtoto amwambie mfalme kuwa yuko uchi!! Mfalme hana nguo, mfalme yuko uchi. Tusipoziba ufa ....

Tutasherehekea Uhuru wa nchi gani?
Hii ni sawa na kusema itafika siku tutasema ,bila ya kujitambua kuwa, tunasherehekea uhuru wa Umoja wa Afrika Mashariki. Jee kutakuwa na nchi itakayoitwa Muungano wa Afrika Mashariki?

Tufumbue macho tuone. Tutumie akili kwa kufikiri na kutafakari.
Wajemani, wadanganyika wenzangu, mambo yamechanganyika sana.
 
Mkuu,

Tunasherehekea uhuru wa nchi gani?

Tunasherehekea!!?? au Tunaomboleza kuipoteza nchi yetu?

Tusitishe sherehe hizi kwanza hadi pale tutakapoirejesha nchi yetu kwanza?

sisi wenyewe tunaona haya kutaja jina la nchi yetu..kujivunia utaifa wetu!!! Tumekuwa watu wa ajabu kweli hapa duniani. Hatujijuwi hatujitambuwi. Tumo tu!!!

Kama umelisahau jina la nchi yetu au kama umezaliwa baada ya 1964 itakubidi umtafute Mchungaji Mtikila atakusaidia jibu.

Usijiunge tu katika mkumbo wa kusherehekea usichokijuwa. usipoteze muda wako kwenda kuangalia mchezo wa maigizo.

Tanganyika nchi yangu, nakupenda kwa moyo wote!!! Kuna siku tutakupulizia uhai tena. Haya hima Wadanganjika!!! Tudai katiba mpya na tuupitie tena mkataba wa Muungano wa Jamhuri ya Tan(nganyika) na Zan(zibar). Hii -ia- tumzawadie Jaji Warioba. Mwenyewe Mwalimu ndiyo hatunae tena!! Yalimtosha haya ya Tanzania akajiondokea zake, mzee wa watu. Ametuachia mradi wa "white elephant" unatutowa roho.

On a serious note wanaJF, ni lazima atokee mtoto amwambie mfalme kuwa yuko uchi!!

Tutasherehekea Uhuru wa nchi gani?
Hii ni sawa na kusema itafika siku tutasema ,bila ya kujitambua kuwa, tunasherehekea uhuru wa Umoja wa Afrika Mashariki. Jee kutakuwa na nchi itakayoitwa Muungano wa Afrika Mashariki?

Tufumbue macho tuone. Tutumie akili kwa kufikiri na kutafakari.
Wajemani, wadanganyika wenzangu, mambo yamechanganyika sana.

Saa zengine tukubali wazungu wanaposema hatujaweza bado kujitawala. Ukiangalia ni kweli na ndio maana tutaendelea kuwa maskini mpaka tutakapoamka wala tusimlaumu mtu.
 
Tarehe 9 disemba kama kawaida tutaalikwa pale uwanja wa taifa kwenda kusheherekea sikukuu ya uhuru na kuangalia ndege za mitumba za jeshi kutoka nchi za magharibi tukiwa na mafanikio yafuatayo

  1. UMEME - ni asilimia 14% tu ya watanzania milion 40 wanapata umeme ambao pia ni wa mgao
  2. MAJI- Ni asilimia 55% tu ya watanzania wanapata huduma ya maji safi
  3. AFYA- mhudumu mmoja wa afya anatakiwa kuhudumia watu laki 1 na pia kitanda kimoja cha hospitali kinatakiwa kulaza watu 1,500
  4. ELIMU- Asilimia 30% ya watanzania wenye umri wa kwenda shule hawajui kusoma wala kuandika
  5. KIPATO- Hakuna ajira..ni asilimia 30% ya watanzania tu wanaofanya kazi katika sekta iliyo rasmi
  6. VIWANDA- kwa asilimia 95% tunatengeneza tusivyonunua na kununua tusivyo tengeneza.
  7. MISAADA- Asilimia 35% ya bajeti ya serikali inategemea misaada kutoka nje.

Je tumlaumu nani? Au tukadai uhuru Upya?

2. MAJI- Ni asilimia 55% ya watz wanapata maji safi. Kama hii ni kweli kwa upande wa maji basi itakuwa ni rekodi nzuri sana.
Mkuu unauhakika na hiyo figure?
 
Kuongezeka kwa Umaskini
Ukosefu wa Ajira, Umeme, Matibabu, Chakula cha kutosha, Uchakachuaji wa kila kitu, na hatimaye Ongezeko la Uporaji wa Mali za Umma
 
Wazungu wanamsemo mmoja kwa Waafrika, "Nyie Waafrika mnafanya vizuri pale tu mnaposimamiwa na Mzungu" Je haya maneno yana ukweli ndani yake?

Mfano, nchi kama S. Afrika, Marekani kuna Waafrika wengi ambao wamefanikiwa kimaisha, elimu, siasa nk. Wazungu ndiyo wanaotawala ktk secta nyingi za uchumi, biashara, nk.
Zimbabwe iliweza kufanya vizuri wakati wazungu walipokuwa wanamiliki sehemu nyingi tu za biashara, kilimo nk. Lakini sasa hivi, ndiyo ni moja kati ya nchi inayoongoza kwa matatizo; kwa sababu wazungu hawapo tena.

Je maneno ya wazungu ni ya kweli?
 
Saa zengine tukubali wazungu wanaposema hatujaweza bado kujitawala. Ukiangalia ni kweli na ndio maana tutaendelea kuwa maskini mpaka tutakapoamka wala tusimlaumu mtu.

Not quite!

Wanatutalawa ndo maana hatuendelei inabidi tutafute viongozi wa kutuongoza ili tuwekze kuendelea vinginevo imekula kwetu!
 
Kila mtoto wa ki Tanzania aliefikia umri wa kwenda shule ana fursa ya kwenda shule.

Sekondari kila kata within the first 4 years of Kikwete.

Kikwete tripled, idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu in how many years?

Zahanati, kila kata.

Kwa mara ya kwanza katika wakati wa JMK, bajeti yetu inategemea chini ya asilimia 40 kutoka kwa wafadhili.

Hivi, Nyerere alifanya nini kwa miaka aliyokaa madarakani. Huyu ndie aliyeiangusha hii nchi.
 
Miaka 50 ya uhuru bado tunategemea nchi wa hisani waje kutujaza mapesa,me nadhani hii sherehe ingesitishwa.
 
Kila mtoto wa ki Tanzania aliefikia umri wa kwenda shule ana fursa ya kwenda shule.

Sekondari kila kata within the first 4 years of Kikwete.

Kikwete tripled, idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu in how many years?

Zahanati, kila kata.

Kwa mara ya kwanza katika wakati wa JMK, bajeti yetu inategemea chini ya asilimia 40 kutoka kwa wafadhili.

Hivi, Nyerere alifanya nini kwa miaka aliyokaa madarakani. Huyu ndie aliyeiangusha hii nchi.

Hapa hatujadili Nyerere versus JK wewe Dar-se.Salaam, wacha kupindisha hoja, watu kama nyie ni hasara kwa taifa, bora ukae kimya maana kila kitu kwako na wengineo kama wewe lazima kiwe twisted to address you devious plans of udini...rais mkristo versus rais mwislamu. Hizo hoja hazitusaidii, kumbuka kuwa maslahi ya wananchi ni zaidi ya dini, hizo zinaweza kutekelezwa kwenye nyumba za ibada, na pia asilimia kubwa pia ni watu ambao si wakristo wala waislamu; so acha ku-mix watu hapa. Tunazungumzia uhuru and if that word means anything to Mtanzania after almost 50 years; are we really free, and if so free from what? Mbona hali za watu wengi ni mbaya sana after of these years of the so called freedom? Why are many Tanzanians living below the poverty line? Why are we among the most poorest countries of the world, we are 148 out of 169 poorest countries, wakati our country is full of resources that is more than enough for every Tanzanian!!! Where have we failed? Shall we celebrate or mourn on 9/12?
 
Kwa wengine habari za ufisadi ni zenye kuchosha kwao. Sio kwa sababu hazina maana katika ujenzi wa taifa, au kwa sababu zimesikika sana ila tu kwa sababu zinagusa hisia zao na wapendwa wao. Hata hivyo hatuwezi kuacha kuziongelea maana nchi yetu miaka 49 sasa huku tukiwa bado tunasota. Sio kwa sababu hakuna fursa na uwezo wa kujitoa kwenye umasikini, ila kwa sababu kuna madhaifu na changamoto ambazo tunaweza kuziondoa pale tutakapoamua kufanya hivyo. Ufisadi ni moja kati ya changamoto ambazo kwangu nimeziweka kama agenda ya juu. Huu unaunganisha kila aina ya ukwapuaji wa "mali" na "hali" za Watanzania kwa faida ya watu wachache au kikundi cha watu fulani

Wengi wetu tulidhani baada ya sekeseke lililomtoa Waziri Mkuu na rafiki zake kadhaa madaraka ingekuwa ni mwanzo wa mwisho wa issue za ufisadi Tanzania. Hata hivyo hii ni kinyume cha matarajio yetu, bado wapo, wanatamba na kila siku tunaendelea kusikia jeuri yao katika kila nyanja ya nchi hii wakitaka kutafuna kila kidogo cha ‘watoto' na kutuacha tukila ‘majani'.

Ni kweli kuwa kila nchi ina ufisadi, tofauti tu ni viwango na jeuri za wale wanaofanya ufisadi. Tanzania yetu wanaotawala ni hawa mafisadi. Hawa ndio wamebeba maamuzi yetu, wakiamua kitu kifanyike kitafanyika, tena kwa style yao, na wakiamua kisifanyike hakitafanyika. Wanajua wananchi wanawafahamu kuwa ni mafisadi lakini bado wanatembea na kufanya kana kwamba wao ndio watakatifu zaidi ya wote katika nchi hii. Hapa ndipo ninapojiuliza swali, Je ni nini source ya Jeuri ya mabaka uchumi haya?????

Hapa nikakumbuka msemo mmoja maarufu sana wa Kabila la Fang kule nchini Gabon unaosema "The Chimpanzee fights because he counts on the help of the Gorilla". Hapa ndipo ninapogundua jambo moja, fisadi ni mtu dhaifu na hapaswi kuwa na uso uliochangamka mbele ya umma unaojua kuwa yeye ni fisadi, lakini je ni kwa nini bado nguvu wanayo ya kupambana kutetea na kulinda na kuendeleza ufisadi wao?? Haiwezekani hivi hivi, lazima kuna nguvu ya Gorilla inayowapa jeuri hii. Hawa Magorila ni wale wanaowapa uhakika "IBA NASI TUTAKULINDA, TUTAUAMBIA UMMA WEWE NI SAFI NA IKIZIDI TUTAWAAMBIA MWACHENI MZEE APUMZIKE KWA AMANI".

Kwa muda sasa naendelea kujiuliza swali, nani ni Gorila (those who vest power and guarantee security to mafisadi) katika nchi hii??
· Je ni system (kwa maana ya katiba na mfumo wa uendeshaji serikali kwa ujumla wake)
· Je ni Chama Tawala (kwa maana ya wanachama na uongozi wa chama)
· Je ni watanzania kwa ujumla??
· Au ni nani basi ambae ndie Gorila wa Machimpanzee hawa wanaobaka uchumi wetu???

Na je, kuna kitu gani Tanzania yetu inaweza kufanya ili turudi kwenye mstari na kuondoa Jeuri ya Ufisadi (kama njia ya kuondoa ufisadi wenyewe). Mambo haya ni muhimu ili tuweze kurithisha vizazi vyetu vijavyo Tanzania yenye neema ambayo itatawaliwa na wananchi na sio mafisadi waliojawa na Jeuri.

Miaka 49 ya Uhuru, Ni nini Asili/Chanzo cha Nguvu na Jeuri ya Mafisadi Tanzania???

TAFAKARI, JADILI, ELIMISHA NA PAMBANA KUONDOA JEURI YA MAFISADI
 
Wazungu wanamsemo mmoja kwa Waafrika, "Nyie Waafrika mnafanya vizuri pale tu mnaposimamiwa na Mzungu" Je haya maneno yana ukweli ndani yake?

Mfano, nchi kama S. Afrika, Marekani kuna Waafrika wengi ambao wamefanikiwa kimaisha, elimu, siasa nk. Wazungu ndiyo wanaotawala ktk secta nyingi za uchumi, biashara, nk.
Zimbabwe iliweza kufanya vizuri wakati wazungu walipokuwa wanamiliki sehemu nyingi tu za biashara, kilimo nk. Lakini sasa hivi, ndiyo ni moja kati ya nchi inayoongoza kwa matatizo; kwa sababu wazungu hawapo tena.

Je maneno ya wazungu ni ya kweli?

Bila Wazungu hakuna maendeleo mkuu hujakosea! Nahisi tunahitaji kudai UHURU kwakua huu uhuru tulionao si wakweli!
 
Maisha bora kwa kila mtanzania haiwezekani bora tukadai UHURU mpya! miaka 50 bado watanzania wanalalia vitanda vya TEMBE na vyoo vya Passportsize?:help:
 
Sina cha kujivunia, sana sana mfumo mbovu wa utawala umenifanya nianze kujiona ka mkimbizi asie na uhuru kwenye nchi yake.

Pia mkasi kati ya maskini na tajiri umepanuka saana. Kuna matajiri wa kutisha TZ ambao ni wafanyakazi wa umma. TGS..... haiwezi kukufanya uwe bilionea, hakuna wa kuwauliza walikozitoa. Sababu zao ni mara waliokota gunia la hela.... mara mikopo benki, yaani wana sababu kibao.

Miaka 50 uchumi upo pale pale.
 
Itakapofika tarehe 9/12/2010 tunatimiza miaka 49 ya uhuru wa Tazania. Bado nasikitika kua bado tunaishi maisha ya kwenye giza bila kua na sababu zinazoeleweka kutoka Tanesco na wadau husika wanaoshughulika na nishati hii ya umeme! yaani imeshafikia hata wao Tanesco kuchoka kuwatangazia wananchi kwenye viombo vya habari kua watazima umeme kwasababu fulani, watanzania tumeshazoea kwamba tukiwa na mgao wa umeme ni kua kina cha maji kule nyumba ya Mungu na kwingineko vimepungua maji au bwawa limejaa matope! kweli tunafikisha nusu karne bado tunaishi kwenye giza? maisha ya mlo mmoja kwasiku?kila kukicha bidhaa kupanda bei? haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania au ni maisha duni kwakila mtanzania naweka hoja mezani nisaidieni niweze kuyaona maisha bora ndani ya hii nusu karne!!:angry:
 
Ndugu wana JF kwanza napenda kuwashukuru kwa michango mizuri na ya msingi sana katika kuleta mabadiliko ya kweli katika kumkomboa mtanzania.Lakini pamoja na hayo yote naomba kuuliza swali lifuatalo:" hivi hata baada ya miaka 49 ya uhuru bado watanzania tupo gizani?"Ndugu zangu watanzania bado hutuwezi kuona kinachoendelea katika nchi yetu hii.Kwa mfano leo hii watanzania wanafurahia net za bure zilizogawiwa hivi karibuni,hivi nyuma ya pazia la net hizi za bure kuna nini?Nakumbuka aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA DR.W.Slaa akiwa kwenye kampeni mkoani Kagera mjini Bukoba alitoa kauli ifuatayo" Rais Kikweti anapokuwa ktk ziara nje ya nchi wakati wa kurudi akiwa hewani kwenye ndege anapishana wenzake nao wakiwa hewani kwenye ndege wakati yeye anarudi na NET kwenye ndege wenzake wanarudi kwao DHAHABU kutoka kwake"

Naomba tusiwe tunakubali vitu bila kujiuliza nyuma kuna kitu kimejificha matokeo yake tunapewa net halafu wao wanabeba rasirimali zetu kama madini(URANIUM,GOLD etc).Naomba watanzania tufunguke macho nchi hii yetu ndio maana Mungu ametupa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
MAGEUZI YA KATIBA NI LAZIMA.
 
Back
Top Bottom