Keynes
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 533
- 89
Tarehe 9 disemba kama kawaida tutaalikwa pale uwanja wa taifa kwenda kusheherekea sikukuu ya uhuru na kuangalia ndege za mitumba za jeshi kutoka nchi za magharibi tukiwa na mafanikio yafuatayo
Je tumlaumu nani? Au tukadai uhuru Upya?
- UMEME - ni asilimia 14% tu ya watanzania milion 40 wanapata umeme ambao pia ni wa mgao
- MAJI- Ni asilimia 55% tu ya watanzania wanapata huduma ya maji safi
- AFYA- mhudumu mmoja wa afya anatakiwa kuhudumia watu laki 1 na pia kitanda kimoja cha hospitali kinatakiwa kulaza watu 1,500
- ELIMU- Asilimia 30% ya watanzania wenye umri wa kwenda shule hawajui kusoma wala kuandika
- KIPATO- Hakuna ajira..ni asilimia 30% ya watanzania tu wanaofanya kazi katika sekta iliyo rasmi
- VIWANDA- kwa asilimia 95% tunatengeneza tusivyonunua na kununua tusivyo tengeneza.
- MISAADA- Asilimia 35% ya bajeti ya serikali inategemea misaada kutoka nje.
Je tumlaumu nani? Au tukadai uhuru Upya?