Tunaposhangilia sheria ya kumrejesha binti aliyezaa shuleni, tusisahau kuuliza haki ya yule mtoto mchanga aliyezaliwa anayebaki nyumbani

Naomba ile sheria ya kwenda jela miaka 30 pia ifutwe ili mama mtoto akiwa shule, baba mtoto abaki na mtoto

Unadhani mwanaume mwenye akili ya kumtia mtoto wa miaka13 mimba ana akili ya kulea kweli!?
Mimi nadhani wengi wao ni matatizo tuu
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Mama D watu wamekuelewa point yako sema wanajitoa ufahamu tu.!
Kuna mambo ambayo inabidi wakae wayajadili mfano kama binti na kijana wa kiume wote wanafunzi je mtoto wa kiume hatoshitakiwa maana naye inabidi asome.!
 
Mama D watu wamekuelewa point yako sema wanajitoa ufahamu tu.!
Kuna mambo ambayo inabidi wakae wayajadili mfano kama binti na kijana wa kiume wote wanafunzi je mtoto wa kiume hatoshitakiwa maana naye inabidi asome.!


Watu wanajitoa ufahamu hadi unaweza kujiuliza wao haswa lengo lao ni nini!? Ni watoto wapate mimba halafu wazae kisha warudi shule? Ni vichanga vibaki popote pale ila tuu mama zao warudi shule? Au ni watoto wanaorudi shule washindwe kuwa na utulivu sababu ya kukosa uhakika wa usalama wa watoto wao!?

Hii issue ni pana sana ila tunaichukulia kirahisi sababu hivyo viatu hatujavivaa

Ndio maana huu ni mjadala, tunaweza punguza hili tatizo kwa kusaidia kupunguza vichocheo na mazingira hatarishi yanayopelekea watoto kupata mimba. Hii itapunguza pia vichanga vitakavyoachwa bila mama zao.

Tunawezajadili vichanga vinavyotarajiwa kuachwa nyumbani vinaishije bila mama zao. Na mama zao wanaweza vipi kupata utulivu wa kukaa darasani kwa imani kwamba watoto wao wako salama
 
Acha kuhaha.Watoto wa kike wakipata mimba wana haki ya kurudi shule.
Hujaelewa mada. Mtoa mada hajakataa watoto hao kurudi shule ila anachouliza, hao waliozaliwa watalelewa na nani?
Kwanza ujue kuwa mtoto anatakiwa anyonye ziwa la mama kwa miezi 6, hivyo lazima shule iwe karibu ili huyu mzazi apate muda wa kwenda nyumbani kunyonyesha. Pili kuna sheria nasikiaga inasema mtoto lazima akae na mama yake hadi atimize miaka 7!
 
Kwani ambaye kaajiriwa au kajiajiri akishajifungua si anaandaa mazingira ya kumuacha mtoto ili arudi kazini?

Na huyu binti naye ataandaa mazingira ya yeye kurudi shule.

Au ulikuwa unapendekeza serikali ifanyaje? Iwapatie wadada wa kazi mabinti wote kabla ya kurudi shule?
Umetoa majibu mwenyewe. Je huyu binti ana uwezo sawa na huyu aliajiriwa au aliyejiajiri? Kumbuka huyu mtoto alikuwa mwanafunzi, si mwajiriwa wala hajajiajiri!
Labda sentensi yako ya mwisho yaweza kuwa sehemu ya suluhu, na si kuwapa mabinti wa kazi tu, bali na kuwalipa pia
 
Mimi namuongelea yule mtoto aliyezaa mtoto wske. Haki ya kile kichanga anapewa na nani?

Na siwaongelei hawa wenye wazazi walio na uwezo wa kuwalea, naongelea wale watoto wasio hata na wakuwalea. Wala sijasema wasirudi shuleni, nimeuliza hivyo vichanga vyao inakuwaje?
Watu wanajitoa ufahamu sidhani kama Kuna mzazi ataacha mwanae na kuendelea na shule vile vile hata walio kwenye ndoa maisha ni magumu ijekuwa mwanafuni?
 
Umetoa majibu mwenyewe. Je huyu binti ana uwezo sawa na huyu aliajiriwa au aliyejiajiri? Kumbuka huyu mtoto alikuwa mwanafunzi, si mwajiriwa wala hajajiajiri!
Labda sentensi yako ya mwisho yaweza kuwa sehemu ya suluhu, na si kuwapa mabinti wa kazi tu, bali na kuwalipa pia
Yaani Serikali iandae utaratibu wa malezi kwa kuweka wafanyakazi wa ndani wa hao watoto?
Aisee.
Kuna watu mna busara sana za kipekee sana.
 
Mtoto wa kike aliyejifungua licha ya kupewa ruhusa bado naona utekelezaji wake kwa waathirika utakua mdogo kwani kisaikolojia hili suala litamtesa.

Kwa upande mwengine mimba pia zitaongezeka kwani mafataki na hata vijana wanaweza kuutumia mwanya huo kuwarubuni kwa kuwaambia , "una wasi wasi gani hata ikitokea mimba inaingia shule itaendelea usijali binti kula raha".

Kitu kingine huwa najiuliza siku zote tumekua tukihubiri usawa wa kijinsia ya kwamba watoto wa kiume na kike ni sawa.

Kwanini mtoto wa kike anaonekana dhaifu asiyeweza kuwa na msimamo wa kuweza kutokushiriki mapenzi mpaka baada ya masomo. Na hili hutetewa hata na wanaharakati wa usawa wa kijinsia pindi inapohojiwa kwanini anaadhibiwa kijana wa kiume anayempa mimba mwanafunzi na hali ya kuwa wamekubaliana? Majibu huwa binti amehadaliwa! Amerubuniwa!
Je mnakubaliana na wale watu wa mfumo dume wanaodai kwamba binti ni dhaifu na hawezi kujisimamia?

Achana na wale wanaobakwa! Hawa wametezwa nguvu

Haya yananifikirisha sana
 
Rais wetu SSH amefanya jambo jema wala hakuna lawama kwake.
Ninachouliza vipi kuhusu vile vichanga vunavyobaki mtaani?? Kama huyu wa miaka13, 15 ameweza kuwa kwenye sehemu hatarishi hadi kupata mimba. Vipi kuhusu kile kichanga ambacho tambui kabisa??

Na siongelei hawa waliokua kwenye mazingira bora bali wale wengi walio kwenye mazingira magumu
Wewe unahisi kichanga hicho unachokitetea kitapatwa na matatizo yapi?

Yaainishe kisha usaidiwe kimawazo.
 
kwani wewe ukizaa na unakuwa umeenda kazini asubuhi hadi jioni, nani anakilea kichanga chako? halafu, ukimnyima elimu msichana huoni kama umemnyima pia huyo mtoto maisha yake mazuri ya baadaye kwasababu mamake atashindwa hata kuja kumlea baadaye. wakibaki wote nyumbani iyo cycle ya poverty itaisha? wewe ni mwanamke mwenye uke kabiswa unawaza namna hiyo dhidi ya wanawake wenzio? hayo ilitakiwa tuwaze sisi wanaume lakini sio wewe.
Hio elimu ipi mnayoipigia chapuo ambayo ina msaada kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom