Uchaguzi 2020 Tunaposhangilia Ahadi za Uongo toka kwa Wagombea, Tusitegemee Muujiza wa Unafuu wa Maisha. Tupambane na hali Zetu

UCL

Member
Aug 18, 2020
8
6
Kampeni zinaendelea nchini. Wagombea wanajitambulisha kwa wananchi huku wakiahidi kuwaletea wananchi maendeleo ya dhati sambamba na kuboresha hali zao za kimaisha. Hili ni tukio muhimu sana katika Taifa letu linalotoa dira ya maendeleo ya Taifa na maendeleo ya wananchi kwa muda wa miaka mitano ijayo.

Mbali na umuhimu huo, bado baadhi ya wagombea wanathubutu kuwarubuni wananchi kwa ahadi zisizotekelezeka ili tu wachaguliwe.

Hii ni hatari kubwa kwa maendeleo ya Taifa letu. Uelewa mdogo walionao wananchi juu ya uchaguzi, hugeuzwa fursa na mtaji wa kisiasa kwa wagombea.

Wanapochaguliwa hakuna wanachokifanya. Mwisho wa siku wananchi hawa huanza kujutia maamuzi yao huku wakimshutumu Mungu eti hawaoni.

Niwakumbushe wananchi. Msikilizeni mgombea kwa umakini tena wa hali ya juu. Mtathmini kama ana nia ya dhati tena itokayo moyoni mwake juu ya ahadi anazojitahidi kukuaminisha. Kisha chukua maamuzi sahihi.

Mnapofanya maamuzi kwa misingi ya USHABIKI msiwe wa kwanza kulaumu hali inapokuwa imebana. Tulieni kwani mnavuna mlichokipanda kipindi cha Uchaguzi. AMANI NA IWE KWENU.
 
Back
Top Bottom