Tunapomsifia sana Nape tukumbuke yeye ndiyo chanzo cha haya...

msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,766
5,902
Naona Baada ya kutumbuliwa watu mnamsifia sana kana kwamba alipokuwa Waziri alifanya vitu vya msingi sana..

Mmesikia Kuhusu watanzania kuzuiwa kuangalia filamu za nje.?
yaani eti sasa filamu za nje hazitauzwa nchini ili kwa lazima tununue zile filamu mbaya na za ajabu ajabu za Bongo Movies..

Mnajua ni wangapi watakosa ajira.?
Mnajua wananchi tutajisikiaje kwa kuwa na serikali inayotuamulia kuhusu kitu cha kutizama kwenye Runinga zetu.?

Sasa basi mwanzilishi wa yote haya ni huyu shujaa wenu 'Nape Nnauye' .!!
Punde tu baada ya kuwa waziri alifanya operation ya kukamata cd za nje kariakoo..

Na kibaya zaidi akakamata za muingizaji wa filamu hizo hapa nchini mzigo ambao ulilipiwa kodi na ushuru bandarini..

Mpaka muuzaji akaacha biashara hiyo..

Leo hii watu mnamponda makonda huo ni unafki mwanzilishi wa hicho kitu ni nape..

Daima nitamlaani nape kwa jambo hilo,mtu anayefikiri vyema lazima angejiuliza kwanini za kanumba(rip) zilikuwa zinanunuliwa ila hizi za sasahivi hazinunuliwi.?

Namalizi kwa kusema Nape Sio Shujaa kila alipopita ameacha Tatizo..

Refer:-
*Uchaguzi UVCCM..
*Bao La Mkono..
*Bunge Live..
*Sheria Mpya Ya Vyombo Vya Habari..
*Kuzuia Muvi Za Nje..
 
Bado sijaelewa hii dhana ya kupambana na utandawazi kwa kushuka chini.

Ninaomba watunga sera, wasanii, na kila mtu anayetaka kuboresha soko la bidhaa yake dhidi ya bidhaa za kigeni, waache kabisa kulazimisha mambo kwa ubabe.

Ningefurahi kama serikali ingewaambia waboreshe products zao ili watu wasinunue vitu vya nje.

Hii si kwa wasanii tu bali haa wazalishaji wa bidhaa mbali mbali.

Pengien kama kuna vifaa maalumu vya kuboreshea kazi kutoka nje ya nchi, vipunguziwe kodi ili wavipate kirahisi lengo likiwa ni kutengeneza products za kiwango kwa gharama itakayomithilika na soko la ndani.

Lakini pia wakiboresha products, wataexport na kutuongezea pato la taifa.

Hii ya kuwashusha chini kwa kulazimisha watu wasipate bidhaa za nje ili waishie kununua za bongo, haitendi jema kwa mtu yeyote. Wanunuzi hawatanunua kwa kuw ahawakidhi mahitaji yao, serikali haitapata kitu,na hao wasanii na wazalishaji watazidi kudoda.
 
Naona Baada ya kutumbuliwa watu mnamsifia sana kana kwamba alipokuwa Waziri alifanya vitu vya msingi sana..

Mmesikia Kuhusu watanzania kuzuiwa kuangalia filamu za nje.?
yaani eti sasa filamu za nje hazitauzwa nchini ili kwa lazima tununue zile filamu mbaya na za ajabu ajabu za Bongo Movies..

Mnajua ni wangapi watakosa ajira.?
Mnajua wananchi tutajisikiaje kwa kuwa na serikali inayotuamulia kuhusu kitu cha kutizama kwenye Runinga zetu.?

SASA BASI MWANZILISHI WA YOTE HAYA NI HUYU SHUJAA WENU 'NAPE NNAUYE' .!!
PUNDE TU BAADA YA KUWA WAZIRI ALIFANYA OPERATION YA KUKAMATA CD ZA NJE KARIAKOO..

NA KIBAYA ZAIDI AKAKAMATA ZA MUINGIZAJI WA FILAMU HIZO HAPA NCHINI MZIGO AMBAO ULILIPIWA KODI NA USHURU BANDARINI..

MPAKA MUUZAJI AKAACHA BIASHARA HIYO..

LEO HII WATU MNAMPONDA MAKONDA HUO NI UNAFKI MWANZILISHI WA HICHO KITU NI NAPE..

DAIMA NITAMLAANI NAPE KWA JAMBO HILO,MTU ANAYEFIKIRI VYEMA LAZIMA ANGEJIULIZA KWANINI ZA KANUMBA(RIP) ZILIKUWA ZINANUNULIWA ILA HIZI ZA SASAHIVI HAZINUNULIWI.???

Namalizi kwa kusema Nape Sio Shujaa kila alipopita ameacha Tatizo..

Refer:-
*Uchaguzi UVCCM..
*Bao La Mkono..
*Bunge Live..
*Sheria Mpya Ya Vyombo Vya Habari..
*Kuzuia Muvi Za Nje..


ACHENI KULALAMAIKA, SULUHISHO NI:

Download YTD Video Downloader free - latest version
 
Mkuu Bei Za Vifurushi Zimepanda..

After all utamwambiaje mama wa pale manzese a- Download Udan.??wakati inawezekana kupatikana kwenye vibanda vya kukodishia..

Kaka kwa utaratibu wa hii nchi sasa - (IRRATIONAL), mambo ni ya ajabu mkuu .....
 
NASEMAJE KAMA NILINUNUA TV, LAPTOP AU SIMU KWA PESA YANGU SIWEZI KUTAZAMA BONGO MOVIE KAMWE !!!!

SIJAONA WANACHONIFUNDISHA TOFAUTI NA KUVAA VIMINI.

SITAZAMI BONGO MOVIE
 
mkuu hivi hii ya bunge live si nasikia Rais alisema yeye ndiye alitoa amri hiyo au?
 
mkuu hivi hii ya bunge live si nasikia Rais alisema yeye ndiye alitoa amri hiyo au?
Mimi Na wewe hatujui..
Tunachojua Ni Nape Alisema Public..

Kama aliagizwa au Lah.! Ni ngumu kujua..
 
sawa lakini rais alitamka hadharani kuwa wabunge wanapiga porojo tu bungeni na ndio maana aliagiza bunge lisiwe live.
 
ukweli siku zote huwa unasimama zido ya uongo NAPE yote hayo kavulunda ,alipokumbuka shuka kumbe pamekucha akakutana na za uso chali
 
Aliamini hakuna wa kumzuia,kumbuka akitamba na ushindi wa bao la mkono,kana kwamba sheria zetu zinaruhusu wizi wa kura.
Lakini hakujua kwamba atakutana na kizingiti hadi kunyoshewa bastola mbele ya umati wa vyombo vya habari,mchana kweupe,walimfananisha na mwizi au gaidi.
 
Yap yap Kama kaida nikushusha tu mamovie mtandaoni Mimi sijawahi kununua CD zaidi ya kuweka tu mb zangu alafu mambo mengine yanaendelea labda wafute movies za nje za kwny mitandao
Ni wachache wenye uwezo huo.
 
Back
Top Bottom