Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,029
- 3,478
Wala hustahili kujitokeza kumsemea mhusika, ajitokeze yeye binafsi katika hili hakuna atakayekuunga mkono kwa kuwa wanajamvi na wananchi kwa ujumkla wana uelewa mkubwa tu.RAIS MAGUFULI ALIMWEKA "JELA" MAKAMU WAKE SAMIA SULUHU HASSAN
Na Bollen Ngetti
MWANAMUZIKI Ndanda Kosovo aliwahi kuimba, "Jela..jela ni mbaya, jela..jela ni mateso". Ndanda hakukosea. Aliimba uzoefu alioupata jela hapo Ukonga. Ninamuunga mkono Ndanda kwa uzoefu nilioupata nikiwa jela Keko na Segerea. Jela ni mbaya. Ukiwa jela umezungukwa kuta nene ndefu huwezi kuona nje kwa kifupi unakuwa umenyimwa uhuru wako.
Hata hivyo hakuna jela mbaya duniani kuliko hata Gwantanamo kama jela ya fikra. Yani jela ambapo huwezi kutoa mawazo yako hadharani. Hii ni jela mbaya inayojengwa na shetani tu.
Niliwahi kudokezwa huko nyuma lakini sikuandika maana nilikosa ushahidi kwamba kuna wakati Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alitaka kujiuzulu nafasi ya Umakamu kujiondoa kwenye gereza la fikra lakini wenye hekma na busara walimshauri asifanye hivyo.
Kwa namna Rais Samia Suluhu Hassan alivyoongoza nchi hii kwa siku 100 ni dhahiri alikuwa jela la fikra. Ni ukweli kwamba hakukubaliana na mambo mengi ya Rais Magufuli hata kama leo anasema "Mimi na Magufuli ni kitu kimoja" lakini matendo ni tofauti.
Mama Samia hakukubaliana na uendeshaji wa demokrasia nchini. Alikuwa jela na ilimtesa ndio maana amechukua njia tofauti kuendesha dhana nzima ya demokrasia. Hakuwa na jinsi wala namna. Bila shaka alilia kimya kimya gerezani.
Mama yetu Samia hakupenda uminyaji wa Uhuru wa Habari. Ilimtesa ndio maana "Fundi" alipomwondoa duniani Pombe naye kuchukua hatamu waandishi wa habari wakashangweka. Akaruhusu Uhuru wa Habari na dunia imeshuhudia maana enzi hizo za jela hata andiko hili lisingetoka maana ningekwenda jela la majengo.
Mama Samia hakufurahishwa na kesi za kubumba. Ilimtesa, ilikuwa ni jela kwake ndio maana alipoingia madarakani akafyatua kesi 147 zilizobumbwa na TAKUKURU. Hali hii ilimtesa. Lakini kuachiwa kwa viongozi wa dini wa Uamsho waliosota kwa miaka 9 jela nayo ilimweka jela kisaikolojia Samia. Hakupenda uonevu.
Huyu mama ni swala 5. Ni Muislamu Safi. Hapendi mali za dhulma iwe ni kwa mtu binafsi au Serikali. Hakupenda fedha za dhulma zilizotokana na kesi za kubumba za uhujumu uchumi na ML ndio maana tunaendelea kushuhudia watuhumiwa wakichomolewa magerezani kwa makundi. Lilimuumiza lakini hakuwa na lakufanya maana hakuwa Mkuu wa Maamuzi, Rais. Kitendo cha Mahakama Kuu kuamuru Serikali kurudisha fedha za dhulma kwa kina Mbowe ni ishara nyingine ya kuwa mama yetu aliumia sana kwa matendo hayo. Alikuwa jela.
Makamu wa Rais Samia (sasa Rais) hakupenda watu kuishi kwa hofu na woga. Alitamani watu wawe huru ndani ya nchi yao ila waheshimu Sheria za nchi. Ndio maana leo hata mama lishe, bodaboda nakadhalika wanakwambia, "nchi inafunguka". Wanahisi uhuru walioukosa miaka 5 tuliyoipa kisogo.
Kumbe hata mradi wa Bandari ya Bagamoyo (BEZ) iliyopigwa vita na Pombe ilimkera. Ilimweka jela la kifikra. Hakupenda lakini leo ameamua tufanye mazungumzo mradi ufanyike.
Ndugu zangu, tumuunge mkono Samia kuondokana na gereza la kifikra ili tulisongeshe mbele gurudumu la maendeleo ya nchi.
Binafsi nimejitoa sadaka kumlinda na kumtetea Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan. Mniunge mkono.
Bollen@2021
#MguseMamaNinuke
Hilo eneo kuanzia chuo cha Mbegani, Zinga kwa Mtoro, Pande na Kiromo inasemekana watu wameanza kujisajili kulipwa fidia mara mbili. Wamasai na Wamang'ati wanaoishi kwenye pori hilo wanatishiwa kila siku kwamba wahame haraka vinginevyo watachomewa vijumba vya na mifugo-hofu imetanda.
Kuna kitu kimejificha kwenye mradi wa Bagamoyo sio bure mtathibisha hivi karibuni maana wako tayari kutumia nguvu kuuanzisha bila kuzingatia shuku ya dhuluma iliyokuwepo.