MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,752
- 5,497
Miongoni mwa Jamii ya watu walionyanyasika na kupitia hali ngumu hapa duniani ni Mtu Mweusi.
Mtu mweusi alikusanywa kama kumbikumbi kutoka moyoni mwa Afrika na kupelewa kutumikishwa Marekani.
Mwaka 1619- Meli kubwa liltia nanga amerika likiwa limejaza Mabibi na Mababu zetu kwenda kutumiwa kama vifaa na sio binadamu wa kuheshimiwa kwa Muda wa miaka 244.
Baadae Mtu mweusi akapitia miaka mingine 100 ya kubaguliwa na kutumikishwa kifikra kama kitu duni, kisicho na akili na tegemezi, Namshukuru Mungu Kwa wazee wetu wakiongozwa na Nyerere walikabidhiwa taifa hili ili angalau tuanze kujisimamia 1961 na hii ilikuwa ni changamoto kubwa kwa mtu mweusi wa Tanzania. Lakini Machozi ya Mtu Mweusi yaliendelea Kumwagika kusini mwa Afrika, Ashukuliwa Mungu kwa Mandera Wakapata nafuu.
Sasa Changamoto inakuja kwa Mtu Mweusi, Pamoja na Watu kama Martin Luther Jr, Malcom x, Mandela, Nyerere na wengine kutoa maisha yao kwa ajili ya mtu mweusi, Bado tukiwa huru ni Wazembe,wavivu, Tunachukiana na kuoneana wivu, tunabaguana, Ubinafsi,Tunahujumiana, tunatesana,Tunauzana na hata tumeamua kuwa tegemezi kwa kodi za binadamu wenzetu ulaya.
FURSA Tanzania zilifunguliwa rasmi 1961 na baadae 1964. tunaenda mwaka wa 56 bado tunajivuta na kujikongoja kama mtu anayeogelea kwenye bwawa la gundi ya maji.
Mwaka huu unaokuja uwe ni Mwaka wa kila mkazi wa Tanzania na Wanajamiiforum wenzangu Tujitafakari na kutumia Fursa zilizopo Kutoka huku tuliko kwama. Hebu dini,siasa,makabila,Matabaka ya kiuchumi yageuzwe kuwa kichocheo cha maendeleo na sio Kamba zinazotuvuta nyuma kwenye dimbwi la chuki,husuda,umasikini na ufukara.
Tukusanye nguvu zetu,zote mmoja mmoja kupambana kwa uwezo wake wote kujikwamua na kukwamua taifa hili, Yawezekana kuna wakati 2017 itakuhitaji usilale siku nzima ili kitu fulani kiende, KESHA. Tulete michango ya kibunifu kwenye familia,vijiji, mikoa na taifa letu. Tujiheshimu na Kuheshimu wengine, Upendo utamalaki miongoni mwetu, Tuushinde ubaya kwa Wema.Dunia inamwaga fursa maelfu mwaka 2017 maelfu zaidi wenda kuliko miaka yote, Usikubali kubaki nyuma Kimbia kwa spidi kuliko aliye mbele yako kielimu,kifedha,kisiasa,kimaendelea fanya kitu kwa Tanzania yako.
Matakwa ya kihistoria hayamuhitaji Mtu mweusi wa tanzania kuangalia nyuma na kutupa lawama kwa Nyerere,Babu yake,Jk,Mwinyi,JPM,Wazazi, Bali chochote tukifanyacho Tufanye kwa bidii zote kana kwamba hutapata Fursa tena. Ni fursa kubwa sana kwa mwanadamu Kuzaliwa Tanzania, na sisi kama watanzania tunapaswa kufanya kazi sio kwa bidii tu (WORK HARD) bali zaidi Kwa Umaridadi (WORK SMART).
Kama ikikuhitaji Graduate Kuuza Vitumbua kutokana na milango ya ajira kufungwa, Uza vitumbua Kwa umakini na bidii kana kwamba hakuna muuza vitumbua mwingine duniani ila wewe.
Wenu
Mseza Mkulu
Katika Kujitafakari Kijijni KIBBUTZ