Tunapima Legacy ya Awamu ya Nne na Tano kwa Uzani: Mfano wa karatasi v/s Chuma

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Mtapima wenyewe. Kanuni ya maumbile ni moja tu. Kilo 1 ya karatasi ni sawa na Kilo 1 ya chuma.

Awamu ya Nne v/s Awamu ya Tano
i. Kuweka mazingira ya uwekezaji kuwa ya kuvutia v/s Kuweka mazingira ya udhibiti zaidi
ii. Kuwepo Demokrasia kwa kiasi fulani v/s Kudhibiti Demokrasia
iii. Kuwepo uwazi kiasi fulani kuhusu sheria, mikataba n.k v/s Kubana Uwazi na mikataba.
iv. Sheria kutoa mianya fulani v/s Sheria kubana na kulalamikiwa
v. Kuwepo kiasi fulani cha uzembe serikalini. v/s Uzembe kupungua na kuongezeka hofu serikalini.
vi. Kukaribisha zaidi mafungamano ya kimataifa. v/s kuondoa baadhi ya mafungamano ya kimataifa
vii. Diplomasia katika utatuzi wa changamoto. v/s Ubabe na lugha zisizofaa katika utatuzi wa changamoto.
viii. Nidhamu hafifu ya kazi na kuwajibika v/s Nidhamu ya uoga na hofu.
ix. Siasa za majadiliano na hoja v/s Siasa za kulazimisha na kuteza.
x. Mijadala na uvumilivu katika kukosoana v/s Amri na vitisho, kukosa uvumilivu wa kukosoana kwa hoja.
xi. Sekta binafsi kupewa kipaumbele v/s Serikali kudhibiti baadhi ya shughuli.
xii. Dhana ya mwenye uwezo kumiliki v/s Dhana ya wazawa kumiliki.(Upendeleo kwa wazawa)
xiii. Dhana ya Ushirikishwaji v/s Dhana ya umiliki wa kidola.
xiv. Mzunguko wa kifedha na fursa za uchumi. v/s Kubana fedha na fursa, kushamiri mfumo dola.
xv. Furaha na umoja ndani ya Mfumo wa kifisadi. v/s Kuwepo chuki na uhasama katika mfumo mpya wa kifisadi (New Corr)
xvi. Viashiria vya umoja wa kitaifa v/s Viashiria vya kuvunjika umoja wa kitaifa, Chuki na Hasira

Nimejaribu kuweka hizo, zipo nyengine nyingi kwa namna ambayo msomaji anaweza kuweka anavyoona inafaa.

Legacy ziko nyingi, Lakini awamu hizi zinaweza kupimwa kwa namna nyingi.

Kwa upande wangu. Kilo 1 ya karatasi = kilo 1 ya Chuma.

Tunahitaji Katiba Mpya.

Kishada.
 
Mnatumia nguvu nyingi sana kuonesha ubaya wa magufuli, lakini ukweli ni kwamba pamoja na utumbo mwingi uliondika hapa,wanaomkumbuka magufuli kwa mazuri ni wengi ata mwaka haujaisha kuliko nyie mnaokumbuka mabaya mkidhani magufuli alikuwa malaika.
 
Mkuu usilalamike. Elewa hio mada. Mnatupumbaza tu. Leteni Katiba Mpya
 
Mezani ya kupimia uadilifu wa utendaji kazi ndani ya CCM vs CCM hakuna ulinganifu unaoutafuta hapo mkuu...... Watanzania tukishikamana vizuri tunaiweka hii chama chakavu pembeni
 
Kila Awamu na ya kwake. Kuna CCM moja lakini kuna wana CCM wengi. Kila Mtu na Utawala wake. Utashangaa Hizo taarifa za Kutumbuliwa kwa Kupiga kwenye Mafuta KWA GIA ya Uzawa. Kila Awamu na ufisadi wake.

Kuna wakati kuna makundi yanapata nafuu dhidi ya wengine kwenye kila awamu. Lakini ukimpima gharama ngoma droo. Kama nchi tumeganda.

Kilo 1 ya karatasi = Kilo 1 ya chuma.
 
Mezani ya kupimia uadilifu wa utendaji kazi ndani ya CCM vs CCM hakuna ulinganifu unaoutafuta hapo mkuu...... Watanzania tukishikamana vizuri tunaiweka hii chama chakavu pembeni
Mkuu pitia vizuri. Tuko pamoja mbona.
 
Mikatabq iliyokawekwa wazi awamu ya nne ni hipi?
Walau uliona mizozano ya sheria kule bungeni awamu ya 4 kupitia TBC . Awamu ya tano Giza licha ya kujinasibu na uzalendo. Hakuna ya makanikia wala ya Korosho. Mwisho kilo 1 ya karatasi = kilo 1 ya Chuma.

Leteni Katiba mpya, Tuanze upya.
 
Yani hueleweki unachotaka! Au tukafukue nyuzi za awamu ya nne uone mkivyolia? Tatizo wepesi mno kusahau
 
Hiyo awamu ya nne mi nilikuwa naitumikia Chadema, napigiwa simu na Tumaini Makene anqniqgiza kazi naenda kuifanya. Yani awamu ya nne ambayo Daudi Mwangosi alitawanyishwa na Bomu..!!
 
Yani hueleweki unachotaka! Au tukafukue nyuzi za awamu ya nne uone mkivyolia? Tatizo wepesi mno kusahau
Unajibiwa kwa mujibu wa swali lako. Wewe ndio hujaelewa. Kama ukiamua kufukua nyuzi za awamu ya 4 na kubainisha huo uozo maana yake ni sawa na kilo 1 ya karatasi = kilo 1 ya Chuma.

Msitusumbue na maigizo
 
Hiyo awamu ya nne mi nilikuwa naitumikia Chadema, napigiwa simu na Tumaini Makene anqniqgiza kazi naenda kuifanya. Yani awamu ya nne ambayo Daudi Mwangosi alitawanyishwa na Bomu..!!
Kwa hio wewe uliunga mkono juhudi sio? Kwa nini umekuwa mateka kiasi hicho. CCM ni ile ile kaka.
 
Legendary John Joseph Pombe Magufuri haupo ila unatajwa sana kuliko Rais yeyote aliyepo au asiyekuwepo, pumzika baba 😁!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom