Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,549
Hey, asalaam alaykm! Kwema kabisa comrades na makamanda humu?
Kwa jicho langu lenye uoni wa mbali naona kabisa Mama hakua na details na hii kesi inayomkabili mwanasiasa mkubwa na mkongwe nchini Kamanda Mbowe na wenzake. Kwa alivyokua akihojiwa na BBC, majibu aliyoyatoa kwa haraka haraka unaona kabisa kua yeye alikua mtu wa kusimuliwa tu lakini siyo kwamba alikua anajua nature na source ya hii kesi. Naona kabisa master minds wa hii kesi ni watendaji ambao kimsingi walianza maandalizi toka 2020 ambapo yawezekana yeye alikua hajui kabisa.
Kwa ushahidi unaotolewa mpaka sasa kwa Mama alivyo na huruma kama mwanamke, inaonekana kabisa haifurahii hii kesi lakini anafungwa na kitu kimoja tu cha kwamba ule ni mhimili mwingine yeye hana maamuzi nao, anachosubiri ni kuona mahakama inatenda haki.Hata yeye kama muumini safi wa dini ya Kiislam naamini anajua kabisa hii kesi ni ya kutunga yenye lengo la kumkomoa mtu.
Mtihani mkubwa ni kwa DPP aliyepo ambaye kwangu mimi mpaka sasa naamini ni mtu anayependa haki, naye naona hakua anaijua hii kesi chanzo chake ameamua naye kuitazama mwenendo wake hadi mwisho na ndiyo maana amejali muda kwa kuipeleka mahakamani haraka ili maamuzi yafanyike na haki ya mtu ipatikane. Ukitaka kujua kua hata yeye DPP ameistukia hii kesi, angalia kuna ushahidi wa madawa ya kulevya lakini hayapo kwenye hati ya mashtaka.
Huu mzigo inaonekana kabisa ni wa kina Kingai,DCI Mstaafu na timu yake na hawa inaonekana wanajua kabisa hii kitu ni wapi inaanzia. Haiwezekani kuna watu wanaotajwa kama viungo kwenye hii kesi kina Sabaya,Kaaya na ASP Jumanne mpaka sasa wana walishakumbwa na tuhuma za utovu wa nidhamu na tuhuma za unyang'anyi tena wengine wanashughulikia vifungo. Hawa wote niliowataja watatu walitajwa kua walikua na shutuma za utapeli.
Walishindwa nini kutengeneza kesi za uongo? DCI mstaafu, Kingai na wengine nani atawaamini? Ushahidi wanaoutoa mahakamani unatofautiana kwa kiasi kikubwa sana, haihitaji digirii kujua kua hii kesi ni ya kuchonga.
Ninachoomba na ndicho pekee cha muhimu, Mahakama itende haki pasina kumuonea wala kumuogopa Mtu. Hii kesi ni maarufu, ikihukumiwa kwa misukumo flani yenye hisia za kisiasa madhara yake ni makubwa nchini mno.
Tunafahamu Sekeseke la Masheikh la uamsho lilivyoitesa serikali, Mbowe si mtu mdogo,ukitaka kulijua hilo fika mahakamani uone ni kina nani wanahudhuria kusikiliza kesi yake.
Sina sababu ya kumlaumu na kumshambulia Mama kwenye hii kesi. Wakutazamwa na kulaumiwa ni watendaji wa chini yake akiwemo IGP hawezi pia kukwepa lawama hizi na hata akistaafu Mbowe akiwa gerezani lawama hazitamuacha salama.