Tunapenda kumuuliza Mh.Waziri Mkuu

Indian

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
821
708
Tunapenda kumuuliza Waziri mkuu na yeye aje atuambie au atusikilize hiki kilio chetu kuhusu hii kampuni ya uzoaji taka Kariakoo, inayoitwa "MOTO INVESTMENT" kwakua tunapotafuta njia ya kukufikia sio rahisi inatubidi tuangushe kilio chetu hapa jf tunaamini hata wasaidizi wako watakuaarifu kwa njia wanzozijua wao.Mara ya mwanzo tumewahi kulalamika hapa jf kuhusu malipo yaliyopangwa na kampuni hii ya uzoaji taka eneo la maduka ya simu mtaa wa aggrey na tulikwenda kwa mtendaji na yeye akatuomba tuende kwa mwenyekiti wa mtaa wa Mchikichini ili yeye ndio mwenye uwezo wa kutusikiliza. Hatujui nani anaidhinisha malipo haya katika taasisi zenu za serikali, kwakua ushirikiano ni mdogo sana baina ya ofisi hizi za serikali na wafanyabiashara wetu huwa unaona tu mwisho wa siku unaambiwa ulipe kiasi kilichopitiswa. Malipo yalikua kwa kila duka moja linalipa sh.10000 kwa mwezi kwa ajili ya uzoaji taka na sio ufanyaji usafi, kwanza hapa kuna vitu viwili tofauti ambavyo hii kampuni inasema yeye kazi yake ni kuzoa tu na sio kufanya usafi, Mh. Waziri mkuu huoni kwamba hapa kuna mwanya wa watu kuendelea kuzitafuna kodi zetu na kwanini kampuni hii iwe inazoa tuu, tukiliacha hilo tunapenda kujua sheria hizi munazipanga mukishirkiana na nani ya kuongeza gharama hizi kwa asilimia 100. Tuliambiwa tulipe sh.60000 kwa mwezi kila duka au kichochoro kuanzia mwezi wa august2012, tulilalamika na mwisho wametuambia tulipe sh.30000, je serikali yetu ina nia njema kabisa na wafanyabiashara? Mnataka tuwalipe wazoaji,wafagiaji, watupaji, na wachomaji moto kweli muna nia njema? Kwa mfano hapa kwenye maduka ya simu peke yake pana maduka 385 mbali ya vichochoro? Mh. Tuambie pesa hizi zote zinakwenda wapi ni nani anaekusanya hizi nguvu zetu kwa kutumia mabavu ya serikali iliyopo madarakani, sisi tunapolalamika huku tunaambiwa mfuko huu au taasisi zinasosimamia mambo haya zikochini ya ofisi za Waziri mkuu,je unalijua hili?
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    657.5 KB · Views: 67
mbona kama waziri mkuu ni mtu wa mbali sana viongozi wengine wote wameshindwa?
 
Back
Top Bottom