Tunapenda kudanganywa?????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunapenda kudanganywa??????

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Felixonfellix, Jun 20, 2010.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Je watanzania wanapenda kudanganywa?
  Je watanzania ni wavivu kweli wa kufikiri?
  Je watanzania hawana uwezo wa tenganisha ukweli na uwongo?

  Nimesukumwa na hasira kuleta maswali haya, baada ya kusoma kwenye gazeti moja kuhusu ndoto mpya ya Raisi Kikwete. Ndoto yenyewe inahusu mpango wa serikali (ambao tayari umekamilika) wa kumwezesha kila mwalimu katika nchi hii kuwa na laptop yake, katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Hivyo ndivyo serikali inapanga vipaumbele.
  Laptop kwa mwalimu wa Iponyaholo, Bulungwa, Ushetu kwa mfano itamsaidia nini?
  Laptop kwa mwalimu asiye na nyumba imara itaitunza wapi?
  Laptop kwa mwalimu ambaye bado hajafunza matumizi yake?
  Ni Laptop isiyotumia umeme?
  Laptop itachangia asilia ngapi katika kuboresha elimu?
  Hivi kumbe tatizo kubwa la walimu wetu ni ukosefu wa computer?

  Binafsi naelewa kuwa hiyo ni siasa tu ya kutafuta kura za walimu. Lakini swali ni je walimu wetu wanapenda kudanganywa? Kwanini mtu atumia a very cheap lie kuwanasa walimu? Maana yake viongozi wetu wanajua kuna tatizo la ujinga na uvivu wa kufikiri na kutenganisha uwongo na ukweli.

  Mimi naona "Tanzania beyond tomorrow" kama inavyoitwa ndoto hiyo ya Raisi ni tusi kwa walimu wetu na kwa watanzania.

  Nafikiri tunahitaji wakina "Kamau" wengi na "matusi" yao.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Si Watanzania tu, watu karibu dunia nzima wanapenda kusikia uongo mzuri zaidi kuliko ukweli mbaya.Sema inawezekana huko kwetu tumezidi.

  Watu wangetaka ukweli tu mbona dini zingekosa waumini, na watu kibao wangekosa wake.
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha!Veri funi but ukweli mtupu!Maisha bora kwa kila mtanzania....Inasikitisha sana tu.....Ila sisi nadhani tatizo letu ni kusahahu mapema,hatuwawajibishi warongo.
   
Loading...