Tunapata reli ya SGR lakini cha moto tunakiona

Mwendokasi umewashinda kuendesha ndio mtaweza SGR?
Mjerumani alijenga reli Dar to Kigoma 1400 km kwa miaka mitano kwa technologia ya wakati huo.
Ninyi Dar mpaka Morogoro km 160 miaka 3. Inamaana mpaka Kigoma iyawachukua miaka 9.
Rekebisheni mwendokasi inayohudumia watu wengi kuliko SGR.
 
Jamani, hivi hicho kijiji si kina wananchi wenye nguvu ya kujenga madarasa bora kwa ajili ya watoto wao? Hata kamani kwa miti , mawe na nyasi lakini wakijenga kwa umakini na ustadi hapawezi kujaa maji, huu ni uzembe wa wazazi! Serikali haiwezi kufanya kila kitu.
ndio ajabu yake, hivi hakukuwa hata na mbunge, madiwani, wenyeviti, hata ukapitishwa mchango wa bukubuku mkoa husika, hakika pesa ingepatikana ya kujenga hilo darasa
 
Kwanza Tanzania ni nchi kubwa kieneo, pili Tanzania hatukusaidiwa kujengewa viwanda na mashirika na hao mabeberu kama walivyosaidiwa nchi jirani, tatu tuliingia vita na Uganda ilitugharimu sana sidhani kama madeni ya silaha yalishaisha.

Kwa hiyo Serikali ya awamu hii imejitahidi na bado inajitahidi kuiinua nchi yetu, kwa hiyo suala la kua na shule kama hizo tusishangae litamalizika taratibu.
Hadi miaka 200 ijayo sababu za kujijitetea ni hizohizo.
 
Mwaka 1999 wananchi wa kijiji fulani kwenye wilaya ya Magu kipindi hicho tulijitolea kujenga nyumba ya mwalimu, na vyoo vya wanafunzi na waalimu na ujenzi wa nyumba za waalimu karibu wote wananchi ndio ambao walikuwa wanachangisha.

Watanzania tubadilike watoto tunafyatua wenyewe halafu wajibu tunataka kuukwepa
 
Maendeleo ya vitu sio maendeleo ya watu.
Mzee baba atatushindisha njaa tutakufa muda si wetu...
 
Back
Top Bottom