Tunapaawaajiri watu kufanya kazi majumbani, tunawafundisha nini watoto wetu??

Bee hive

Senior Member
Feb 22, 2012
146
54
Salaam wana jamii. Kuna jambo kidogo linanitatiza kwa wazazi wa sasa hivi au miaka hii (2000- mpaka sasa), hivi tunawalea vipi vijana wetu?.

Una kuta mzazi nyumbani una vijana ambao wanaweza kufanya shughuli ndogo ndogo za usafi wa mazingira yako kama, kufyeka, kupalilia maua na bustani, kufagia nk.

Cha kushangaza hawafanyi hizo shughuli na badala yake unaajiri mtu kuzifanya. Tunawafundisha nini hawa vijana?, hii nazungumzia zaidi kwa watu wa kati na huku uswazi. Tujitahidi kuwapa malezi bora vijana wetu kama tulivyopewa sisi na wazazi wetu enzi hizo isije ikawa balaa hapo siku za usoni.

Shughuli ndogo ndogo za nyumbani huwajenga vijana kiakili na kiafya. Tubadilike kwa manufaa ya vijana wetu!
 
Wanawapeleka shule..
Shule sawa ndg, ila tulienda shule na hizo shughuli tulizifanya enzi hizo na hakuna lililo haribika. Cha ajabu shule za sekondari (za bweni), wameajiri wafanyakazi kufanya usafi na shughuli kama hizo badala ya wanafunzi.
 
Mashuleni kuna stadi za kazi...
 
Back
Top Bottom