kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
Kutenganisha mchele na pumba katika itikadi hapa nchini kumeanza kutokana na hatua za Rais John Magufuli kubadili kanuni za uendeshaji wa bunge hasa kuhusiana na aslahi ya wabunge
Baada ya kuwaondoa wabunge katika bodi za mashirika ya umma, utaratibu umewekwa wa kusaini kuingia na kutoka bungeni, yaani asubuhi na jioni tena kwa vidole kadhaa na si kwa dole gumba pekee.
Isitoshe fedha za kujikimu za wabunge ambazo tayari zimeshapunguzwa kutoka laki tatu hadi 120.000 na inaelekea hali imekuwa tofauti. Zimekatwa hadi kufikia 30.000 kwa siku.
Kwa mtu anayezifaham mbwembwe na heshima ya bunge kwa miaka 10 au 20 iliyopita, hatua hivi ni aina ya mapinduzi katika maisha ya wabunge wetu na inawezekana wengi wao hawakudhania kama hali hiyo inaweza kutokea kamwe katika maisha yao ya uheshimiwa.
Tumezoea kusikia baadhi ya wabunge kukatb posho kwa madai kwamba ni unyonyaji kwa wananchi masikini sasa amekuja Rais Magufuli amcye ana hisia hizo na anazitekeleza bila kuwauliza
Historia za uwakilishi Afrika mashariki inaonyesha uwakilishi wa bunge umekuwa na gharama kubwa na zikiongezeka kila leo. Tanzania haikuwa na gharama kubwa ilinganisha na Kenya na Uganda licha ya utafiti kuonyesha kuwa serikali hizo Tanzania ikiwemo zimeonesha kuelewa na kuridhika na upandajishaji wa malipo ya wabunge, iwe posho au mishahara.
Ndio maana Tanzania chini ya Rais Magufuli inafanya bunge kuwa la wananchi kama ambazo kimsing inatakiwa lakini haipo hivyo kutika nchi za Afrika kama katiba zao inavyosema.
Ni mazingira ya bunge kuondolema katika hadhi ya washiriki utawala ngazi za juu na kuwekwa katika tabaka la kati.
Wabunge wetu wamekuwa wakitetea itikadi ya kimapinduzi wakati maslai yao wenyewe ya mwelekeo tofati na itikadi hiyo.
Labda tuwafahamishe wale wanaosema hatua kama hivi za Rais Magufuli ni uingiliaji wa shughuli za bunge, Magufuli na serikali yake hawajaingilia kazi za bunge isipokuwa kinachofanyika ni kurekebisha mazingira ya ajira na marupurupu au mishahara ya utumishi wa umma, ambapo katika hilo serikali ina mamlaka na suala hilo.
Kwa maana nyingine tangu miaka ya 1990 wabunge walikuwa hawaweshi kuonyesha mapenzi yao kwa azimio la Arusha, lakili kuna uwezekano kuwa uungaji mkono kwao ha tkuwa unafana na kile kinächoitwa 'mkuki kwa nguruwe.
Inawezekana kabisa wabunge wanataka nyenzo za Azimio la Arusha ili kuwabana watu wengine wakiwamo wafanyabiashara, bila kuathiri maslahi mapana ya bunge, pamoja nastahili zao za uwakilishi, nk.
Kwa mfano ujumbe wa bodi katika ashirika ya umma siyo biashara mbele ya wabunge, bali kwa hisia za Azimio la Arusha, ilikuwa ni mwanya wa kupokea mishahara miwili kwa visingizio vya vikao, safari nk.
Inapofikia mahali mahali ambapo Azimipo la Arusha linatafsiriwa kwa maana ya kutopata mishahara miweili, au kipato cha kiongozi (mbunge) kisipishane na sana na mwananchi wa kawaida (sh. 30,000 za posho kwa vikao vya kawaida ni ya chini kwa kawaida ya mikutano hapa nchini kwa sasa) suala linakuwa tofauti.
Mwisho natoa Rai kwa wote tuliokuwa tunalitaka azimio la Arusha tumuunge mkono Rais Magufuli kwa kuwa ameonyesha nia na hisia za kulikubali na kulitekeleza kwa kuwabana na wanaofuja fedha za umma na kubana matumizi ya serikali na kuzielekeza fedha kwenye maendeleo.