Tunaosoma na tuliosoma kitabu cha 'I Can I Will I Must' cha Mzee Reginald Mengi njooni tujadili

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,012
8,358
Kwanza,naomba nianze andiko langu kwa Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumleta mtu aliye itwa Mengi Tanzania,pili nishukuru kwa kumchukua kwa wakati huu.

Pili naomba niwape dondoo kidgo dhidi ya ninachoendelea kukutana nacho katika kitabu cha i can i will i must.

Kwanza,kitabu ukurasa wa Tano,kinaonesha madhara ya mfumo wa ujamaa ulivyokuwa na mchango mbaya sanaa wa ukuaji wa taifa letu kiuchumi.

Pili kitabu kinaonesha UWOGA WA MWALIMU NYERERE KWA WAWEKEZAJI WAZAWA KUWA WAFANYA BIASHARA WAKUBWA,mengi anaonesha alivyompiga kbsa kwa uamuzi wake wa kuanzisha kiwanda cha vinywaji Boniite.

Aliweza kumkosoa Mengi ila alishindwa kuwakosoa wahindi.

Tatu, Mzee mengi anaonesha alivyopata mtaji wa biashara.

Niliyoyakuta,

Nyerere aliua ushirika akiofia matajiri walio zalishwa kwenye ushirika wangempora madaraka.

Nyerere, na ujamaa wake ulikuwa mzuri kutengeza viongozi with ethical ila ulikuwa mbaya kiuchumi kwa taifa hasa alipoamua kuua ushirika.

Suala zima la vijana wetu wanao maliza vyuo vikuu wanapoandika proposal na kupeleka Benk wapewe mikopo ya kuanzisha project,halikuanza leo Tanzania hata Mengi alinyimwa Mtaji na Benki ya NBC iliyokuwa ikimilikiwa na serikali pase.

Ambatana na mimi ukurasa wa Tano sasa.

Jaman kitabu cha i can i will i must,ukurasa wa Tano ndiko mzee wetu Mengi anaelezea alikopata mtaji wa kuanzisha biashara ya kununua na kuuuza peni

Je wajua kuwa NBC ilikataa kumpa mkopo pamoja na kupeleka andiko makini ili ali benki ilikuwa inamilikiwa na serikali?

Je wajua kuwa nyerere alikuwa ampendi Mengi?

Wakati nikiendelea na kukisoma kitabu cha I Can I Will I Must, nimejifunza mengi sana kauli ya mzee Mwinyi yaani Ruksa iliweza kumtoa Mengi katika mfumo wa kuajiriwa mpaka kujiajiri kwa kuanzisha viwanda vyake.

Najua watanzania wengi hatupendi kusoma basi jitaidi wewe unayesoma hapa soma ukurusa wa Tano tu.

Kama ningekuwa mwandishi wa kwenye gazeti,basi ningeandika makala nzito,kutoka ukurasa wa Tano wa kitabu hiki cha Marehemu Mzee Mengi.

Katika ukurasa wa Tano, mzee Mengi anaonesha jinsi Kauli ya mzee Mwinyi alipoingia Ikulu ya RUKSA ilivyompa imani ya kupambana na kuamua kujitoa katika kuajiriwa na kuingia katika ujasiriamali.

Mzee Mengi anaonesha kabisa kuwa mfumo wa ujamaa ulikuwa mzuri sana kwa ajili ya kutengeneza maadili ya viongozi na jamii ila kiuchumi ulikuwa ukididimiza nchi kiuchumi.

Zaidi funzo liliopo hapo,mfumo wa ujamaa ulikuwa ni mfumo wa maisha ila Mzee Mwinyi alivyoingia madarakani yeye alikuwa na neno tu RUKSA,halikuwa mfumo lilikuwa just a neno tu. Lakini lilikuwa na madhara positive sana kwa uchumi wa nchi yetu kuliko mfumo,hapo nina maana kuwa,HAPA KAZI TU NI NENO SIO MFUMO sasa lazima tujue fanya kazi inatamkwa katika mfumo gani?je ni mfumo wa ujamaa au mfumo wa ubepari?

Funzo kubwa zaid ni kuwa kauli za viongozi wetu wapo watakao nufaika nazo wapo watakao ummia

Je, kauli ya hapa kazi tu inaweza zalisha bilionea kama neno ruksa lilivyomuibua mengi?
 
Jaman kitabu cha i can i will i must,ukurasa wa Tano ndiko mzee wetu Mengi anaelezea alikopata mtaji wa kuanzisha biashara ya kununua na kuuuza peni

Je wajua kuwa NBC ilikataa kumpa mkopo pamoja na kupeleka andiko makini ili ali benki ilikuwa inamilikiwa na serikali?

Je wajua kuwa nyerere alikuwa ampendi Mengi?
Nyerere alimchukiaje Mengi? Mbona unatuuliza maswali badaya ya kutufafanulia kwa kina??
 
kwa viwanga vya kimataifa vya kuitwa bilionea , The late Dr. Mengi hana ila vya kiwango vya kibongobongo anaitwa bilionea. ili uwe bilione unatakiwa uwe na mali za dola bilioni moja na zaidi( net worth $1bn), Mengi alikuwa na net worth ya $550 million.
Bilionea pekee bongo ni Mohammed Dewji ambaye katengenezwa na JK na JPM kaendeleza kumtengeneza zaid
 
Hili ndilo linapaswa lifanyike , kiukweli tanzania ya sa iv vikwazo vimekuwa vingi sana. Serikali inapaswa ifungue milango ya uwekezaji hta mgeni akiwa na $50000 aruhusiwe kuja kuwekeza ....tumeweka masharti magumu ya uwekezaji matokeo yake uwekezaji hamna na ajira hamna
 
Sasa umekuja kukitangaza au.??

Mi nilijua utayaandika hayo, ila umeandika dibaji tu ambayo wote tuliijua siku anayozindua kitabu..
 
Akitamka neno moja tu kesho yake matajiri wanafilisika na kuanza kuishi kama masikini, ni uchuro
Mimi ningekuwa rais ningeruhusu mtu yoyote bila kujali rangi yake na anapotokea km ana uwezo wa kuwekeza na kuajiri watu zaidi ya 5 basi apewe leseni haraka sana......hya masharti ya kutaka mwekezaji mpaka awe na dola laki tano yanatukosesha wawekezaji wengi wenye mitaji midogo ambao wangeweza kubadilisha maisha ya watu wengi
 
Kwanza,naomba nianze andiko langu kwa Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumleta mtu aliye itwa Mengi Tanzania,pili nishukuru kwa kumchukua kwa wakati huu.

Pili naomba niwape dondoo kidgo dhidi ya ninachoendelea kukutana nacho katika kitabu cha i can i will i must.

Kwanza,kitabu ukurasa wa Tano,kinaonesha madhara ya mfumo wa ujamaa ulivyokuwa na mchango mbaya sanaa wa ukuaji wa taifa letu kiuchumi.

Pili kitabu kinaonesha UWOGA WA MWALIMU NYERERE KWA WAWEKEZAJI WAZAWA KUWA WAFANYA BIASHARA WAKUBWA,mengi anaonesha alivyompiga kbsa kwa uamuzi wake wa kuanzisha kiwanda cha vinywaji Boniite.

Aliweza kumkosoa Mengi ila alishindwa kuwakosoa wahindi.

Tatu, Mzee mengi anaonesha alivyopata mtaji wa biashara.
Acha papara ukurasa wa tano tu tayari unaona nyerere hafai. Tulia soma kitabu hadi mwisho ndio useme kitu...Kwa akili yako unafikiri kila mtanzania aki i can i will i must atakua tajiri kama mengi. Wengi wanabaki tabaka la kawaida ndio ujamaa ulikua na maana hapo.
 
Back
Top Bottom