Uchaguzi 2020 Tunaoona mbali tulionya jambo hili halina siha kwa ustawi wa Taifa

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,064
Wadau,

Kuna kipindi ambacho Press conference zilifanyika kwa wingi na nyingi zikiwa kuwatangaza watu waliounga mkono Juhudi JUHUDI. Tunasikia (hatuna ushahidi bado) kuwa kuna watu walilipiwa madeni na wengine kuahidiwa vyeo ili waunge mkono juhudi.

Halmashauri zilivurugwa, mameya wa majiji waliondolewa kwa nguvu, chaguzi ndogo zilifanyika na wabunge walirudishwa kwa hila za wazi (Mollel huko Hai, Mtulia na wengine)

Tunaoona mbali tulionya ya kuwa jambo hili halina siha kwa ustawi wa Taifa lakini waliotaka kumfurahisha mkuu walitukejeli. Sasa tufanye evaluation ya uwekezaji huu ulifanywa na Polepole na timu yake kwa kujibu maswali machache yafuatayo,
  1. Je, umerahisisha kampeni?
  2. Tuliowanunua watarudi?
  3. Tumependwa zaidi?
 
Kubwa zaidi ni waliopanga mkakati wa kumuondoa TAL, wakajua wameshamaliza mchezo. Hawakuwahi kuwaza kwamba angesalimika na kuja kuwa mwiba wakati huu.

Nimesikitika Mama ambae kidogo alikua na heshima kwa mbali kuropoka kwamba askari waliopitia mafunzo wakikosa mtu kwa risasi tatu wanawajibishwa. Hivi serikali yao yenye dhamana ya usalama wa raia kushindwa kuwatia hatiani au kuwakamata hao wazembe waliofyatua risasi 16 sio fedheha zaidi kwa serikali?
 
Mpango wa kuwanunua wanasiasa ulidhihirisha ujinga wa Polepole na Bashiru. Yawezekana Mwenyekiti alishiriki katika kupanga au ulikuwa ni mpango wake. Kama usingekuwa mpango wake, nina hakika Bashiru na Polepole wangefurushwa kwa mpango huo wa kijinga ambao haukuwa na faida kwa yeyote - iwe ni CCM, Taifa, kwa vyama vya upinzani au hata kwa taia mmoha mmoja.

Mpango ule wa kununua watu unadhirisha ni kwa kiwango gani uongozi wa juu wa CCM awamu hii unekaliwa na watu wenye maono butu na IQ ndogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kubwa zaidi ni wakiopanga mkakati wa kumuondoa TAL, wakajua wameshamaliza mchezo. Hawakuwahi kuwaza kwamba angesalimika na kuja kuwa mwiba wakati huu.

Nimesikitika Mama ambae kidogo alikua na heshima kwa mbali kuropoka kwamba askari waliopitia mafunzo wakikosa mtu kwa risasi tatu wanawajibishwa. Hivi serikali yao yenye dhamana ya usalama wa raia kushindwa kuwatia hatiani au kuwakamata hao wazembe waliofyatua risasi 16 sio fedheha zaidi kwa serikali?


TAL hana jipya tena, keshachuja, atapata kura kiganjani hazijai.
 
Ivi tuwasomushe watoto mpaka ngazi gani ili tufute ujinga na kuwajengea uwezo wa kujitegemea? Nauliza ivi kwasababu mipango ya kununua madiwani na wabunge iliratibiwa na Dr, Bashiru sijui ingepangwa na kina Kinana tungesingizia Elimu?

Upumbavu wa msomi ni ushindi wa wasio na Elimu a.k.a Wajumbe. Twende na Lissu tuokoe Taifa.
 
Nadhani waliomshauri mzee kwamba kuwanunua wapinzani, kuzuia mikutano ya hadhara, kutawadhoofisha na kuwafanya wadogo kutamfanya apendwe, walimpotosha sana.

Nadhani kasoma somo moja kubwa sana in a hard way, akiifanikiwa kupata tena nafasi nadhani atayasema yoooote, kwa sababu kuwa anapeda kusema ya sirini.

Nadhani kajifunza kuwa kuwekeza kwenye mema mioyo ya watu kuna faida zaidi kuliko kuwekeza kwenye visasi na ubabe.
 
TAL hana jipya tena, keshachuja, atapata kura kiganjani hazijai.

Mie siongelei atapata kura ngapi, na kuchuja au kutokuchuja, hilo wataamua wananchi. Nimeandika kauli ya mama mwenye wadhifa aliyoutoa hivi majuzi.

Na huu uzi unajadili baadhi ya mambo yaliyofanywa kwa lengo la kuhujumu upinzani.
Unatumia kipimo gani kujua maamuzi ya watu watakayoyafanya?
 
Wadau,
Kuna kipindi ambacho Press conference zilifanyika kwa wingi na nyingi zikiwa kuwatangaza watu waliounga mkono JUHUDI. Tunasikia (hatuna ushahidi bado) kuwa kuna watu walilipiwa madeni na wengine kuahidiwa vyeo ili waunge mkono juhudi..
Mission imefeli vibaya mnoo ..na kati ya vitu ccm wanajutia ni huu ununuzi wa madiwani na wabunge kutoka upinzani ..umefeli kwa %
 
Back
Top Bottom