Tunaongeza vijana wavaa tai tunawasahau wasukuma uchumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaongeza vijana wavaa tai tunawasahau wasukuma uchumi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mjenda Chilo, Aug 11, 2012.

 1. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Elimu yetu ya juu imelipuka (Mushrooming), ghafla bin vuu, chini ya muongo mmoja tumeotesha vyuo vikuu sambamba na kubadili vyuo vya kawaida kuwa vyuo vikuu. Kwa suala la wingi tumefaulu haswa. Quality sasa ndo kitendawili. Vijana wametapakaa mtaani na vyeti vyao wanataka kazi wafunge tai, wanunue magari na wajenge nyumba zao, shughuli! My point ni je huu mkazo wa kuandaa wafunga tai na kutokuweka msukumo wa kutosha kwa mafundi watakaoendesha na kutengeneza mitambo ya ujenzi, matrekta ya kilimo kwanza nk nani atafanya? au ndo tumewaachia wachina waje wanyooshe magari na kupaka rangi? Kila mtu anataka kiyoyozi ili awe manager, nani atakuwa managed sasa? Time bomb, magraduate wenyewe ukimsikiliza unajiuliza mara mbilimbili. University sasa ni ya kila mtu, haijalishi we ni kiazi kiasi gani sanasana ni suala la hela yako tu. Lazima tutengeneze watenda kazi, vinginevyo tutakuwa wapiga siasa woooote.
   
Loading...