Tunaomuunga Mkono Magufuli Hatufurahishwi na hizi "Distractions"

Hapa nawaza 2020 itafika lin maana nshakata tamaa na hili zombie...
Hana focus wala priorities anafanya mambo kwa interest zake binafs tu...
Hv ile mirad ya chato ilikuwepo kwny ilani ya chama gan??? Bajet yake imepitishwa kwny kikao kipi cha bunge lipi???
Huu ni ubinafs wa std gauge hatuwez kuendelea kwa uongoz wa aina hii...
 
Unajua kuna watu WANALAZIMISHA Kutaka kuendesha nchi kutokea kwenye MEDIA na kwenye SOCIAL NETWORK - Yaani MTU YUKO JF au kwenye GAZETI, Analazimisha KUELEKEZA NAMNA YA KUENDESHA NCHI - Mara RAIS AMCHAGUE FULANI, RAIS MTUMBUE FULANI HAFAI, RAIS FANYA HIVI NA VILE - UKIFANYA HIVI AU VILE UNAKOSEA. INAMAANA HUYO RAIS NI ROBOT ?? - YAANI Hakuna mtu mwenye AKILI TIMAMU, MWANAMUME ALIYEKAMILIKA Atakayekubali UMSAIDIE KUENDESHA NCHI Kutokea JF ( Na hata akikubali atakuwa ni mpumbavu ) ni sawa na FAMILIA Unapoona Baba mwenye nyumba anaendesha nyumba kutoka kwenye mawazo ya vijiweni HAFAI.
Naomba nikuelemishe kidogo mkuu kuhusu watu kutumia Social Media kutoa maoni yao kuhusu ili lkn kama utakua tayari
 
Ondoa porojo zao hapa, kama hamumtaki msimpigie kura 2020! Kinyume na hapo ni wivu tu unaowazalishia chuki inayoleta fitina na Majungu!
Uumh! Tuliza kichwa uchangie kwa hekima.

Kuna viongozi Duniani hapa waliwahi kushinda chaguzi kwa kura nyingi lakini hata kabla ya vipindi vyao kwisha walilazimika au mifumo nchi zao ya kiutawala ililazimisha kufanyika kura za maoni ili kuamua kama viongozi hao waendelee au waondolewe. Kiongozi wa kisiasa hana tofauti na mfanyakazi wa kawaida. Mfanyakazi kabla ya kumwajiri unamfanyia interview, unaridhika kabisa atakuwa mfanyakazi mzuri lakini baadaye unakuja kugundua ni mwizi, mvivu, hajiamini, mwoga, mwongo, n.k. Kuna mwingine atahitaji ushauri, mafunzo au maonyo lakini mwingine atahitajika kufukuzwa. Utakuwa mwajiri mjinga kabisa kama utasema siwezi kufanya chochote kwa vile tu nilikwishamwajiri.

Rais ni binadamu, anahitaji ushauri, kukosolewa na hata kushirikiana na watu mbalimbali ili kufikia malengo ya Taifa. Haiwezekani tuone dosari halafu tusiseme eti tusubirie kumwondoa kwenye uchaguzi.

Hii ni nchi yenye watu waliopo kwenye hatua mbalimbali, kuna makosa mengine yakifanyika, hata ukiyarekebisha baada 2020, hutapata nafasi ya kuondoa athari zake kwa walioathirika au hata kwa Taifa. Taifa halitakiwi kuwa na mda wa kuruhusu mtu kuharibu, wakati wote linatakiwa kutembea kuelekea mbele.
 
Mzee Mwanakijiji

Hoja uliyoweka ni muhimu sana kuijadili, lakini kama unavyofahamu hoja kama hizi hakuna anayetaka kuzijadili. Kama unavyofahamu mimi sina chama lakini napenda kuona Tanzania yenye maendeleo chanya ya kutufikisha kwenye neema. Kasi anayokwenda nayo JPM nimeipenda sana, lakini hawa wapinzani uchwara wanataka kumchelewesha na yeye anayo meno makali ya kuwang'ata na watanyooka tu.

JPM ameandaa progamme yake kwa miaka kumi inayokuja, panapo majaliwa hawa wote pimbi wanaopiga kelele watakuwa wanalialia kutaka aongeze muda.
Believe me hatua ambayo atakuwa amepiga itakuwa ni aibu kubwa sana kwa marais watatu waliomtangulia na hawa ni kikwazo kikubwa sana hivi sasa. Kama wakileta fyoko asiwape marupurupu yao ambayo yanawafanya wawe na kiburi.

Hatuwezi kuwapa nchi hawa wapinzani uchwara wanaoongozwa na cartel ya wezi wa kimataifa.
Unaposema huna Chama yabidi uwe smart sana Katika comments zako... But your content tayari ishaonesha ni mwanachama wa Chama gani... Sio lazima kudanganya kuelezea hisia zako... Ungeelezea tuuuh bila kuanza na mbwembwe za sina chama
 
Ukitaka kumuunga mkono Magufuli wewe muunge kwa hali yeyote ila kama unaona ni ngumu binafsi naona ni bora ukaachana naye kabisa ILI UWE NA AMANI.

- Tatizo kubwa la binadamu ni moja; WAMESHAKUKABIDHI USUKANI UENDESHE GARI, LAKINI HAWAISHI KUKUELEKEZA KILA WAKATI NAMNA YA KULIENDESHA GARI LENYEWE - NA KIBAYA ZAIDI Ukiwasikiliza na mkakwama LAWAMA ZOTE UTAPEWA WEWE.

- Ukishamkabidhi USUKANI Mwacheni aendeshe anavyojua ili hata AKIKWAMA Unazo HAKI ZOTE ZA KUMLAUMU MPAKA KIAMA
Nilidhani una report kwa traffic police... hii yako itakuwa sheria mpya
 
pic+magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Sielewi kwanini serikali inapojaribu kusimamia mabadiliko na nidhamu katika utumishi wa umma inajigongelea misumari yenyewe. Ninavyoona ni sawa na fundi seremala mashuhuri anayejaribu kutengeneza samani nzuri lakini haishi kujigonga nyundo vidoleni yeye mwenyewe! Anataka tuone uzuri wa samani zake ili tuzipende lakini wakati huo huo hatukosi kumuona anavyolia kila nyundo inapotua kwenye kidole ambacho angeweza kukiepuka kama angekuwa makini. Anajigonga mwenyewe kwa sababu wakati huo huo anafanya ufundi wake bado anazungumza mambo yasiyohusiana, mara ashike kitabu kusoma, mara asikilize muziki n.k kiasi kwamba anaonekana hana focus.

Binafsi ningependa sana serikali ya Magufuli ioneshe nidhamu yenyewe (self discipline) na kutulia mkazo wanachofanya(focurs) badala ya sasa ambapo hadi baadhi ya vitu hatujui vinaendelea vipi kwani mazungumzo ya kitaifa yamebakia kwenye mambo yasiyo ya msingi au ya lazima (irrelevant issues).

Kuna msemo kuwa "neno la muungwana ndio dhamana yake". Msemo huu unamaanisha tu kwamba mtu muungwana akisema neno, au akitoa ahadi fulani basi haitaji kuweka rehani kitu chochote ili kuaminika; yaani neno lake ni rehani tosha kwa yeye kupewa dhamana. Mtu muungwana anapotoa ahadi basi anaaminika kwa sababu neno lake linaaminika.

SIKUMBUKI (na nimeweka herufi kubwa kwa mkazo tu) kama Magufuli wakati anatoa ahadi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 alisema jambo lolote ambalo liliashiria kuwa ama angekuwa na ugomvi wa kudumu na wapinzani au kwamba atajaribu kuingilia au kushawishi mihimili mingine ya dola. NINACHOKUMBUKA ni kuwa aliahidi kati ya vitu vingi (hasa kwenye hotuba yake ya uzinduzi wa kampeni pale Jangwani mwezi Augusti 2015) kwamba ataheshimu mawazo ya watu mbalimbali hata kama ni upinzani na kuwa ataheshimu uhuru wa mihimili mingine.

Sasa inapotokea kuwa vyombo vya dola vinahangaika sana na vitu ambavyo vinaangukia kwenye himaya ya uhuru wa maoni au mawazo inasikitisha. Nimewahi kusema hapa miaka karibu kumi sasa kwamba haki ya uhuru wa maoni na uhuru wa mawazo hailindi mawazo mazuri au yenye kufurahisha. Mawazo mazuri na yenye kufurahisha hayahitaji kulindwa; kinacholindwa ni mawazo mabaya, mabovu, ya kuudhi na wakati mwingine ya kukera kabisa. Magufuli alipokubali kutaka kugombea Urais na kusimama kugombea maana yake ni kuwa alikuwa tayari kusemwa, kukejeliwa, kufanywa kituko, kuchorwa vibaya, na hata kufikiriwa vibaya. Alikubali kwa sababu aliaminisha umma kuwa ana ngozi ngumu (tough skin). Na sisi tuliomuunga mkono na ambao bado tunamuunga mkono tunaamini ana ngozi ngumi hivyo tunaposikia ati mtu kakamatwa kwa sababu kamsema vibaya Rais, au sijui kasema jambo lenye kumkera Rais inatuudhi!

Sasa inawezekana ni watu wa chini tu ambao nao wanafikiria wanamtendea Rais hisani kwa kufuatilia watu wanasema nini juu ya serikali au nini. Hizi ni distractions! Leo hii sijui kuna kesi ngapi zinahusiana na mambo ya kipuuzi na watu wazima na akili zao kuchwa kucha wamekaa wanahangaika hadi kama ni burudani inaanza kufanya watu wasinzie. Watu gani hawachoki kutafuta kesi za kila namna, asubuhi na mchana, hadi watu kwenye mitandao wanaanza kutunga vitu vya uongo ili kuwajaza watu hofu! Juzi kuna message inatembea ati serikali inarekodi mazungumzo yote ya kwenye simu na watu wanaanza kuhofia hata kuzungumza kwenye simu, huu ni upuuzi gani?

Kama kweli Magufuli anaumia sana moyoni, anakereka kirahisi rahisi, anakwazika na kila kibaya kinachosemwa juu yake kiasi kwamba anaona wanamzuia kutekelezas wajibu wake au anaona kuwa kazi hii ni ngumu sana kwake kuifanya binafsi nina ushauri mzuri tu; Katiba imeweka utaratibu wa hiari kwa Rais akujiuzulu. Si LAZIMA awe Rais. Kwa sababu tunaomuunga mkono tunaamini yeye ni Rais ambaye Tanzania ilimhitaji sasa na tuliamini kuwa akiweka mkazo (focus) na kusimamia nidhamu (self discipline) ya serikali yake basi katika miaka hii mitano mambo makubwa yanaweza kufanywa kuliko yaliyofanywa miaka hamsini iliyopita!

Hivyo basi, ushauri wangu ni kuwa Serikali ikae chini na kujiuzuli kwanini inachekelea hizi distractions? Kwanini inazunguka zunguka kwenye mambo yasiyo na msingi badala ya kuwashawishi wananchi kwa uongozi wake kuonesha mambo makubwa yanayofanywa au yanayopangwa kufanywa?

Magufului ni lazima ahakikishe mambo yafuatayo nayatokea:

a. Kuheshimu mahakama kwa gharama zote - demokrasia na utawala wa demokrasia vinasimama au kuanguka na uhuru wa mahakama. Kama kuna viongozi wanaitwa mahakamani ni LAZIMA watii! Na binafsi hilo peke yake ni sababu tosha ya kumfukuza mtu kazi kwa kutokutii mahakama. Na Rais mwenyewe aepuke kwa nguvu zake zote undue influence ya mahakama.

b. Rais atumie ushawishi wa nguvu za hoja kuliko ushawishi wa hoja za nguvu. Watu ni lazima waone mantiki ya kinachosimamiwa kuliko hofu ya kutokukisimamia. Katika hili ni lazima Rais ajioneshe kuwa ni mtu wa tafakari na siyo mtu wa munkari. Ukali uliopo ni wa lazima na binafsi naamini kati ya vitu vilivyokosekana kwa muda mrefu ni viongozi wakali; lakini ukali hauondoi ushawishi.

c. Kesi dhidi ya wapinzani na ambazo zinaonekana ni za kisiasa zifutwe ili taifa lirejee kwenye mijadala ya kisiasa bila hofu ya kumuudhi Rais. Na labda hili litawafanya polisi wafocus na wenyewe kwenye mambo ya msingi - kama vita dhidi ya madawa ya kulevya, ufisadi n.k Sasa hivi ni kana kwamba vita dhidi ya ufisadi imeenda picnic! Magufuli aliungwa mkono na baadhi yetu kwa sababu alikuwa ni chaguo sahihi kupambana na ufisadi kwani tulijua ana uthubutu wa kuugusa ufisadi. Hadi hivi sasa kasi ya kupambana na ufisadi haijaleta matumaini sana. Na kinachosikitisha ni kuwa kesi kadhaa hadi hivi sasa zinaonekana haziendi popote kwa sabbabu hazioneshi kama zimefikiriwa vizuri na mawakili wa serikali wanatia aibu! Ni rahisi zaidi kumkamata mtu kuliko kuthibitisha kwanini umemkamata! Watu wakamatwe pale ambapo kuna uthibitisho wa uhalifu hasa lakini hizi kesi nyingine zinafanya serikali ionekane haina mawakili wabobezi au wenye ujuzi wa kusimamia kesi nzito matokeo yake tunatengeneza precendence za ajabu sana!

d. Wakati umefika kwa Magufuli kulihutubia taifa na kulishawishi (persuade) lielewe anataka kufanya nini na anafanya nini vitu hivyo. Ni hotuba ya kuliamsha taifa pia ili kila Mtanzania afanye nini katika nafasi yake. Kitu kibaya ambacho kimetokea (na nilidokeza kwenye makala yangu wiki mbili nyuma) watu wanaitegemea sana serikali hakuna moyo wa kujitolea (kwa kiasi kikubwa). Ni lazima kuamsha roho ya kujitolea katika taifa badala ya watu kusubiria serikali ifanye. Magufulia anatakiwa kuamsha roho ya ujenzi wa taifa; watu wajitolee kulijenga taifa lao kuliko kusubiria kila kitu serikali ifanye. Je, ni vitu gani Watannzania wanaweza kufanya wenyewe bila serikali kuwafanyia? hii ndio changamoto ya kiuongozi!

Kwa ufupi, tuachane na distractions na vitu vinavyopoteza mwelekeo au hata mjadala wa kitaifa. Ni muhimu serikali ioneshe ina nidhamu katika watendaji wake ikibidi hata kupangua baraza la mawaziri kwani kuna watu wanapwaya kupita kiasi sasa hadi inakera. Kama kuna jambo lolote Rais anaona haliendi sawa au linahitaji sheria ngumu ni muhimu serikali iende Bungeni na mabadiliko ya sheria ili jambo hilo lishughulikiwe kisheria.

Tunaomuunga mkono Magufuli tunataka uwajibikaji, utawala wa sheria, kuheshimu tunu za kidemokrasia, ushawishi wa hoja, kuwa makini na wenye mkazo na kuepuka kupoteza muda kwenye mambo yasiyo ya msingi. Muda uliobakia na mchache na tusipoteze nafasi kwa mambo yanayopoteza fedha za umma na muda wa wananchi kujadili mambo ya msingi.

"Managers get things done by others" mkuu wetu hili ndilo analopaswa kufundishwa hata kwa ujiti ili ajue kuwa presidaa ni kupambana, kufikiri, kuhamasisha wengine wafanye kazi sio huu utaratibu wa I wish I could be IGP. Hapa ndio udhaifu mkubwa jamaa aliuficha wakati wa campaign, akubali wengine wafanye kazi kwa style zao lakini ahakikishe malengo ndio yanafikiwa sasa hivi hata mkuu wa wilaya anapambana kuiga wrong approach za mkuu. Tulimwambia wapo watu katika sector binafsi, vyama vya upinzani na NGO ambao wangemsaidia kupata matokeo, amekuwa input based leader badala ya kutazama outcomes.

Ukali na kunyoosha unaweza ukafanyika bila ya kuathiri kazi zilizofanywa na watangulizi wake, Sifa kwa mkuu imekuwa ndio kipimo kikuu cha utendaji kazi. Kila mteule anapambana kumfurahisha traffic wanaua sector ya usafiri ambayo imekuwa miongoni mwa sector zinazokuwa na kuongeza kipato lakini mkuu anawatumia kuua biashara ya usafiri. Tuliwahi kusema kuhusu "Doing business rodmap report ya word bank" barriers barabarani zinafanya safari zinakuwa ndefu na hazina tija kwa ukuwaji wa sector huyu bwana hasikii kabisa yuko too mechanical mpaka biashara zinaanguka sasa. Yeye anajua tertially ni Air Tanzania tu anasahau zile zinazogusa watu wengi tena bila uwekezaji mkubwa amegawia machine za kukusanya pesa traffic police ili wafanya biashara wa usafiri waishi kama mashetani. Toa traffic barabarani watu wasafiri kwa uhuru na wahusishe wadau katika kupunguza ajali barabarani hizi ni quick wins aruhusu usafiri wa usiku sababu nchi yetu ni transit iwe rahisi kwa majirani wengi wapite kusubiri uchumi wa viwanda bila tertially anafanya hata taaluma zetu kuwa hazina maana, anatumia nguvu kubwa na muda mwingi katika vitu visivyo na tija katika uchumi bali vinampa sifa yeye binafsi.

Kilimo ndio msingi wa uzalishaji mali katika nchi hii, mabadiliko ya hali ya hewa ilitakiwa nguvu kubwa itumike ili kupunguza athari wenzie walifanya yeye ilikuwa kupigia mstari tu lakini anatoa kejeli na majibu ya ovyo badala ya dira kwa mfano wakulima wakisema njaa haina maaana awape chakula hata kuhamasisha ukulima wa mazao mbadala kama Mtama tu ungetosha kuwa back up yeye akiongea hovyo wateule wake ndio sasa wanaonyesha umahiri kama kuna mkuu wa Wilaya Kahama alimweka ndani Afisa kilimo kwa kugawa vibaya kg 90 za mtama katika kata ya Bugarama hii maana yake kugawa kg 90 ambazo wakulima wananunua wenyewe kwa kijiji cha zaidi ya kaya 6,500 ni utani lakini kwa kuwa kiongozi anataka kusikia watu wanafukuzwa kazi na kudhalilishwa basi hii ni habari njema kwa mkuu.

Hii nchi ni ya kwetu sote lakini sababu yeye ndio presidaa amegeuza ni ya kwake peke yake na aliwateua ni kwa ajili ya kumsaidia yeye. Hizo billioni 10 anazotoa katika kujengea askari nyumba, atumie mfumo huo kuwapatia wafanyabiashara pesa wazungushe ili uchumi uende mbele, majengo ya askari hayatolipa kodi mbeleni, rasilimali watu ndio silaha huyu bwana angekuwa msikivu ingemsaidia haraka sana lakini nafsi yake haina mahaba na watu.
 
Kwa hili Mzee Mwanakijiji kula like yangu.

Tukiacha unafiki na kuwa wakweli kisha kuheshimu wengine na kufuata sheria na taratibu za nchi. Hakika tutapiga hatua.

Vinginevyo tutarudi kule kule kwy wana mtandao ndio wanaostahili kusema, kuamua, kutenda na hata kula hiyo keki peke yao. Kama si wa kundi lao basi haustahili baadhi ya haki zako za msingi hata kama zinatamburika kisheria.

Uzuri wa Watanzania, ni wepesi sana kutoa taarifa pale wanapoona mambo hayaendi mswano. Vyama vya siasa, mitandao ya kijamii, vyombo vya habari na maoni mbalimbali ya watu binafsi vingeachwa viwe huru ilimladi tu havivunji sheria.

Hiyo ingesaidia kufichua mabovu na pia kujua wananchi wanataka nini. Kazi ya kiongozi wetu ingekua rahisi sana na wala asingehitaji kampeni huko mbeleni maana ange tenda kulingana na matakwa ya wananchi waliomchagua.

Kutegemea interejensia peke yako haitoshi na nchi ni kubwa sana hii. Watu wanaweza fanya yao kimya kimya na mpaka kujakugundulika tayali keki imeishaliwa liwa nusu. Lakini uhuru wa habari ungesaidia sana pale mtu akiigusa tu hiyo keki tayali anatajwa hivyo tungeilinda kabla haijaliwa.

Wakatabahu!
 
pic+magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Sielewi kwanini serikali inapojaribu kusimamia mabadiliko na nidhamu katika utumishi wa umma inajigongelea misumari yenyewe. Ninavyoona ni sawa na fundi seremala mashuhuri anayejaribu kutengeneza samani nzuri lakini haishi kujigonga nyundo vidoleni yeye mwenyewe! Anataka tuone uzuri wa samani zake ili tuzipende lakini wakati huo huo hatukosi kumuona anavyolia kila nyundo inapotua kwenye kidole ambacho angeweza kukiepuka kama angekuwa makini. Anajigonga mwenyewe kwa sababu wakati huo huo anafanya ufundi wake bado anazungumza mambo yasiyohusiana, mara ashike kitabu kusoma, mara asikilize muziki n.k kiasi kwamba anaonekana hana focus.

Binafsi ningependa sana serikali ya Magufuli ioneshe nidhamu yenyewe (self discipline) na kutulia mkazo wanachofanya(focurs) badala ya sasa ambapo hadi baadhi ya vitu hatujui vinaendelea vipi kwani mazungumzo ya kitaifa yamebakia kwenye mambo yasiyo ya msingi au ya lazima (irrelevant issues).

Kuna msemo kuwa "neno la muungwana ndio dhamana yake". Msemo huu unamaanisha tu kwamba mtu muungwana akisema neno, au akitoa ahadi fulani basi haitaji kuweka rehani kitu chochote ili kuaminika; yaani neno lake ni rehani tosha kwa yeye kupewa dhamana. Mtu muungwana anapotoa ahadi basi anaaminika kwa sababu neno lake linaaminika.

SIKUMBUKI (na nimeweka herufi kubwa kwa mkazo tu) kama Magufuli wakati anatoa ahadi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 alisema jambo lolote ambalo liliashiria kuwa ama angekuwa na ugomvi wa kudumu na wapinzani au kwamba atajaribu kuingilia au kushawishi mihimili mingine ya dola. NINACHOKUMBUKA ni kuwa aliahidi kati ya vitu vingi (hasa kwenye hotuba yake ya uzinduzi wa kampeni pale Jangwani mwezi Augusti 2015) kwamba ataheshimu mawazo ya watu mbalimbali hata kama ni upinzani na kuwa ataheshimu uhuru wa mihimili mingine.

Sasa inapotokea kuwa vyombo vya dola vinahangaika sana na vitu ambavyo vinaangukia kwenye himaya ya uhuru wa maoni au mawazo inasikitisha. Nimewahi kusema hapa miaka karibu kumi sasa kwamba haki ya uhuru wa maoni na uhuru wa mawazo hailindi mawazo mazuri au yenye kufurahisha. Mawazo mazuri na yenye kufurahisha hayahitaji kulindwa; kinacholindwa ni mawazo mabaya, mabovu, ya kuudhi na wakati mwingine ya kukera kabisa. Magufuli alipokubali kutaka kugombea Urais na kusimama kugombea maana yake ni kuwa alikuwa tayari kusemwa, kukejeliwa, kufanywa kituko, kuchorwa vibaya, na hata kufikiriwa vibaya. Alikubali kwa sababu aliaminisha umma kuwa ana ngozi ngumu (tough skin). Na sisi tuliomuunga mkono na ambao bado tunamuunga mkono tunaamini ana ngozi ngumi hivyo tunaposikia ati mtu kakamatwa kwa sababu kamsema vibaya Rais, au sijui kasema jambo lenye kumkera Rais inatuudhi!

Sasa inawezekana ni watu wa chini tu ambao nao wanafikiria wanamtendea Rais hisani kwa kufuatilia watu wanasema nini juu ya serikali au nini. Hizi ni distractions! Leo hii sijui kuna kesi ngapi zinahusiana na mambo ya kipuuzi na watu wazima na akili zao kuchwa kucha wamekaa wanahangaika hadi kama ni burudani inaanza kufanya watu wasinzie. Watu gani hawachoki kutafuta kesi za kila namna, asubuhi na mchana, hadi watu kwenye mitandao wanaanza kutunga vitu vya uongo ili kuwajaza watu hofu! Juzi kuna message inatembea ati serikali inarekodi mazungumzo yote ya kwenye simu na watu wanaanza kuhofia hata kuzungumza kwenye simu, huu ni upuuzi gani?

Kama kweli Magufuli anaumia sana moyoni, anakereka kirahisi rahisi, anakwazika na kila kibaya kinachosemwa juu yake kiasi kwamba anaona wanamzuia kutekelezas wajibu wake au anaona kuwa kazi hii ni ngumu sana kwake kuifanya binafsi nina ushauri mzuri tu; Katiba imeweka utaratibu wa hiari kwa Rais akujiuzulu. Si LAZIMA awe Rais. Kwa sababu tunaomuunga mkono tunaamini yeye ni Rais ambaye Tanzania ilimhitaji sasa na tuliamini kuwa akiweka mkazo (focus) na kusimamia nidhamu (self discipline) ya serikali yake basi katika miaka hii mitano mambo makubwa yanaweza kufanywa kuliko yaliyofanywa miaka hamsini iliyopita!

Hivyo basi, ushauri wangu ni kuwa Serikali ikae chini na kujiuzuli kwanini inachekelea hizi distractions? Kwanini inazunguka zunguka kwenye mambo yasiyo na msingi badala ya kuwashawishi wananchi kwa uongozi wake kuonesha mambo makubwa yanayofanywa au yanayopangwa kufanywa?

Magufului ni lazima ahakikishe mambo yafuatayo nayatokea:

a. Kuheshimu mahakama kwa gharama zote - demokrasia na utawala wa demokrasia vinasimama au kuanguka na uhuru wa mahakama. Kama kuna viongozi wanaitwa mahakamani ni LAZIMA watii! Na binafsi hilo peke yake ni sababu tosha ya kumfukuza mtu kazi kwa kutokutii mahakama. Na Rais mwenyewe aepuke kwa nguvu zake zote undue influence ya mahakama.

b. Rais atumie ushawishi wa nguvu za hoja kuliko ushawishi wa hoja za nguvu. Watu ni lazima waone mantiki ya kinachosimamiwa kuliko hofu ya kutokukisimamia. Katika hili ni lazima Rais ajioneshe kuwa ni mtu wa tafakari na siyo mtu wa munkari. Ukali uliopo ni wa lazima na binafsi naamini kati ya vitu vilivyokosekana kwa muda mrefu ni viongozi wakali; lakini ukali hauondoi ushawishi.

c. Kesi dhidi ya wapinzani na ambazo zinaonekana ni za kisiasa zifutwe ili taifa lirejee kwenye mijadala ya kisiasa bila hofu ya kumuudhi Rais. Na labda hili litawafanya polisi wafocus na wenyewe kwenye mambo ya msingi - kama vita dhidi ya madawa ya kulevya, ufisadi n.k Sasa hivi ni kana kwamba vita dhidi ya ufisadi imeenda picnic! Magufuli aliungwa mkono na baadhi yetu kwa sababu alikuwa ni chaguo sahihi kupambana na ufisadi kwani tulijua ana uthubutu wa kuugusa ufisadi. Hadi hivi sasa kasi ya kupambana na ufisadi haijaleta matumaini sana. Na kinachosikitisha ni kuwa kesi kadhaa hadi hivi sasa zinaonekana haziendi popote kwa sabbabu hazioneshi kama zimefikiriwa vizuri na mawakili wa serikali wanatia aibu! Ni rahisi zaidi kumkamata mtu kuliko kuthibitisha kwanini umemkamata! Watu wakamatwe pale ambapo kuna uthibitisho wa uhalifu hasa lakini hizi kesi nyingine zinafanya serikali ionekane haina mawakili wabobezi au wenye ujuzi wa kusimamia kesi nzito matokeo yake tunatengeneza precendence za ajabu sana!

d. Wakati umefika kwa Magufuli kulihutubia taifa na kulishawishi (persuade) lielewe anataka kufanya nini na anafanya nini vitu hivyo. Ni hotuba ya kuliamsha taifa pia ili kila Mtanzania afanye nini katika nafasi yake. Kitu kibaya ambacho kimetokea (na nilidokeza kwenye makala yangu wiki mbili nyuma) watu wanaitegemea sana serikali hakuna moyo wa kujitolea (kwa kiasi kikubwa). Ni lazima kuamsha roho ya kujitolea katika taifa badala ya watu kusubiria serikali ifanye. Magufulia anatakiwa kuamsha roho ya ujenzi wa taifa; watu wajitolee kulijenga taifa lao kuliko kusubiria kila kitu serikali ifanye. Je, ni vitu gani Watannzania wanaweza kufanya wenyewe bila serikali kuwafanyia? hii ndio changamoto ya kiuongozi!

Kwa ufupi, tuachane na distractions na vitu vinavyopoteza mwelekeo au hata mjadala wa kitaifa. Ni muhimu serikali ioneshe ina nidhamu katika watendaji wake ikibidi hata kupangua baraza la mawaziri kwani kuna watu wanapwaya kupita kiasi sasa hadi inakera. Kama kuna jambo lolote Rais anaona haliendi sawa au linahitaji sheria ngumu ni muhimu serikali iende Bungeni na mabadiliko ya sheria ili jambo hilo lishughulikiwe kisheria.

Tunaomuunga mkono Magufuli tunataka uwajibikaji, utawala wa sheria, kuheshimu tunu za kidemokrasia, ushawishi wa hoja, kuwa makini na wenye mkazo na kuepuka kupoteza muda kwenye mambo yasiyo ya msingi. Muda uliobakia na mchache na tusipoteze nafasi kwa mambo yanayopoteza fedha za umma na muda wa wananchi kujadili mambo ya msingi.
Serikali ya ghiliba, visasi, visa, majungu, uhasama, uonevu, kukurupuka, kuonea , kupakazia, kuzusha, kukamata na kufunga bila ushahidi, kupambana na mawazo huru ya wananchi wake huwezi kupata moyo wa kujishughulisha nayo. Utawala huu umeuwa kabisa uhuru, haki, na utu wa mwananchi. Sijui ni kitu gani kinawafanya watawala kuwa waoga kiasi hiki.
 
Kinachoendelea sasa KWA MSIO NA MACHO ni mikakati mubashala ya CCM katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi ujao, rejea tathmini yao ya uchaguzi uliopita (2015) na namna ya kuongeza imani kwa wapiga kura wao na kuwapata wale wengine ambao hawakuwapigia. Mkuu alikabidhiwa tathmini hii ya chama na mapendekezo kibao nini kifanywe kukabiliana na yaliotokea NUKTA
 
Kati ya watu ninaowashangaa siku hizi ni wale wanaojaribu kujibizana na Barbarossa; kwa ujumla wake kuanzia unyayo mpaka utosi hana hadhi ya kujadiliwa yeye au hoja zake. Ni mtu wa kiwango cha chini mno katika hoja, wewe mfuatilie hata post tano tu kuanzia sasa utakubliana nami kuwa hajawahi na hatawahi kuwa na hoja ya maana anapopinga au anaposapoti kitu.
Asante mkuu ngoja niwaache waendelee na yao
 
Raisi Magufuli siyo Superhuman ni Binadamu kama Binadamu wengine hivyo hawezi kuwepo kila mahali na kutimiza kila hitaji la kila Binadamu, kama hamumkubali kuna njia ya kufanya hivyo nayo ni 2020 msimrudishe Ikulu, vinginevyo kaeni pembeni na mwachieni Uwanja na Timu yake wafanye yale wanayaoona yanafaa na kama mnaona ni Udikteta au huo mnaouita Utawala ya Sheria haufatwi basi Watanzania tutaammua 2020, lkn binafsi namuunga mkono Raisi Magufuli na kwanza ukiniuliza mimi hawa wanaojiita Upinzani siyo watu wa kuwachekea kabisa, ni watu wabaya, kama nikikuuliza
Ben Saanane yuko wapi? Na kwa nini hamumuongelei tena? Kwa nini mlisema Serikali yetu imemuua na kufukia maiti yake Mto Ruvu halafu leo muko kimya? Hizo shutuma zilikuwa na lengo gani? Mlitembea kwa Wazungu Ulaya kuwaambia kwamba Serikali yetu imeemua Ben Saanane, Je ninyi ni watu wazuri wa kuchekewa chekewa? Raisi Magufuli bana hapo hapo usirudi hata milimeta 1 nyuma, nchi haijengwi kwa ulele mama, Historia itakuwa hakimu!
Mambo ya kipuuzi sana! Tumefikia kila mtu akitoa hoja chanya kama ya mwanakijiji umekuwa mtu wa kwanza kuelekeza kwa Chadema! Mwanakijjji si Chadema! Na amekiri na makala yake tangu mwaka juzi ni kumpamba rais Magufuli! Iweje leo Barabosa anahusisha na Chadema? Hizi ndizo distractions ambazo anazungumzia Mwanakijiji! We have lost the focus somewhere! Kama ndo mawazo ya yako na watu wa aina yako, miaka mingine zinapita bila kuona maendeleo chanya! Labda ahadi yake ya kuua upinzani ndo kama itakuwa maendeleo atafanikiwa, ila miaka mitano inaisha Rais anapambana na vivuli vyake!
 
Mzee Mwanakijiji

Hoja uliyoweka ni muhimu sana kuijadili, lakini kama unavyofahamu hoja kama hizi hakuna anayetaka kuzijadili. Kama unavyofahamu mimi sina chama lakini napenda kuona Tanzania yenye maendeleo chanya ya kutufikisha kwenye neema. Kasi anayokwenda nayo JPM nimeipenda sana, lakini hawa wapinzani uchwara wanataka kumchelewesha na yeye anayo meno makali ya kuwang'ata na watanyooka tu.

JPM ameandaa progamme yake kwa miaka kumi inayokuja, panapo majaliwa hawa wote pimbi wanaopiga kelele watakuwa wanalialia kutaka aongeze muda.
Believe me hatua ambayo atakuwa amepiga itakuwa ni aibu kubwa sana kwa marais watatu waliomtangulia na hawa ni kikwazo kikubwa sana hivi sasa. Kama wakileta fyoko asiwape marupurupu yao ambayo yanawafanya wawe na kiburi.

Hatuwezi kuwapa nchi hawa wapinzani uchwara wanaoongozwa na cartel ya wezi wa kimataifa.
Kwa hiyo hawa maraisi waliopita ni wapinzani wa JPM,think twice bro
 
Nimeipenda sana comment yako mkuu ina maana kubwa sana. Wakati Magufuli anaanza na kasi kubwa walisema kaiba ilani yao ya uchaguzi. Maana kufuatana na washabiki wa wanasiasa wa CCM B (ukawa), alichokua anakifanya Magufuli kilikua katika manifesto yao. Ikaja kufuta live TV ya bunge naona hii haikuwa katika ilani yao mambo yakaanza kubadilika. Wakaanza kususia bunge. Mara mada ikabadilika mpaka Udikteta uchwara (wamesahau kuwa walisema aliyekuwapo kabla ya JPM alikua mpore). Baada ya sinema ya bunge Live ikaja operation ambayo haikupata mwisho UKUTA. Mara wakasambaratika kila mtu akaleta tafsiri yake ya ilani ya UKAWA, Lema akaanza kuleta ilani ya kuchukua nafasi ya Sheikh Yahaya Hussein ya kutabiri vifo, na wengine kutafuta kesi za kupotezea mapungufu. Baada ya hapo ikaja kwanini rais hasafiri (hapa pia walisahau kuwa aliyemtangulia walimuita Vasco Dagama). Mpaka sasa sielewi nini hasa vipaumbele vya Upinzani wa Tanzania na pia sijui nini ni muelekeo wa serikali ya Tanzania....Ndiyo maana kwa sisi tusiyo na vyama tunakwenda na hisia zetu pale ambapo tunamuona JPM anafanya kwa manufaa ya Taifa hili tunamuunga mkono na pale ambapo anakosea tunamlima na maneno ana hatujajali kuitwa Nyumbu wala Lumumba maana siasa zetu za Tanzania ni bora hata tungeruhusu watoto wa chekechea watuonge ama wawe wanasiasa maana wangesingizia ni umri kuliko hawa wanasiasa tulio nao.......Mungu Ibariki Tanzania, Mungu mbariki Makonda asiteteleke na kelele za chura...
Huna chama wewe????? una tatizo mahali
 
Mzee Mwanakijiji

Hoja uliyoweka ni muhimu sana kuijadili, lakini kama unavyofahamu hoja kama hizi hakuna anayetaka kuzijadili. Kama unavyofahamu mimi sina chama lakini napenda kuona Tanzania yenye maendeleo chanya ya kutufikisha kwenye neema. Kasi anayokwenda nayo JPM nimeipenda sana, lakini hawa wapinzani uchwara wanataka kumchelewesha na yeye anayo meno makali ya kuwang'ata na watanyooka tu.

JPM ameandaa progamme yake kwa miaka kumi inayokuja, panapo majaliwa hawa wote pimbi wanaopiga kelele watakuwa wanalialia kutaka aongeze muda.
Believe me hatua ambayo atakuwa amepiga itakuwa ni aibu kubwa sana kwa marais watatu waliomtangulia na hawa ni kikwazo kikubwa sana hivi sasa. Kama wakileta fyoko asiwape marupurupu yao ambayo yanawafanya wawe na kiburi.

Hatuwezi kuwapa nchi hawa wapinzani uchwara wanaoongozwa na cartel ya wezi wa kimataifa.
Pumba.
 
Niliposikia Magufuli kaanza vita vya ufisadi, nilidhani ataanza na zile donda ndugu zinazotafuna taifa kama issues za IPTL, Tegeta Escrow, Ligumi, Commodity Supprt, mikataba mibovu ya madini na gesi, Meli mbovu iliyobadilishwa ya kijeshi,Richmond,Kiwira, mikataba ya barabara, n.k....Haya yaliyeyuka nilipomsikia anakitamka hatafukua makaburi! Leo hii wameanzisha mahakama ya mafisadi, iliyotungwa kwenye usimamizi wa mafisadi, ukaishia kuwa "white elephant" project! Watetezi watasema, anaaanzia alipoanza utawala! Hadi hapa tunaumia kwa mikataba na ufisadi wa miakanya nyuma! Na tutashtuka tumeumia.
Tumebaki na matamko, kkamata wapinzani, dharau mahakama, bunge weka kule kisa anawalipa mshahara! , demokrasia weka kule, diplomasia kuyumba pamoja na kuwa na waziri mbobezi wa diplomasia! Watanzania wanataka kuona mabadiliko chanya kwenye maisha,,,watumishi waone maslahi yao yanatekelezwa, wakulima waone serikali inafanya kitu kwenye kilimo kwa kuwapatia ruzuku na program zenye tija, wafanyabiashara na wajasiriamali wanataka ahueni kwenye kazi zao na.mazingira rafiki kupata na serikali ipate kodi yake! Leo sekta binafsi iko hoi! Mkiuliza,,, mlizoea kupiga dili! Hii dili ndo nani, nini na iko wapi? Wapiga dili wameondoewa? Wamefikishwa mahakamani? Nani kafungwa? Uchumi unazidi kudorora, elimu mashakani,mikopo elimu ya juu taabani!
Tumsifu Magu kwa lipi hadi leo? Bombadier au hiring or firing? Elimu bure bila.maarifa? Time will tell
 
Back
Top Bottom