Tunaomiliki magari ya mzungu tukutane hapa

Wale wamiliki na wanapoenda kumiliki magari ya Mzungu tukutane hapa Kwa ushauri na kubadilishana mawazo. Najua ni changamoto Sana kumiliki haya magari hapa Tz kuanzia mafundi,spare na uchumi vile vile. Nina uzoefu mkubwa sana kwenye haya magari.

Niulize chochote kuhusu magari haya nitakujibu kwa uzoefu wangu. Karibuni tujadiliane. Jitahidi kununua gari isiozidi miaka 10 kwasababu vitu vingi kwenye gari vinachoka baada ya miaka kumi.

Una ushauri gani kuhusu bmw mini cooper,kwa hapa bongo?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi nimetokea kuipenda sana VW Jetta 2006 option nilizonazo ni kati ya 2005-2006 BMW 320i ila jamaa zangu wananiambia Jetta itanipa shida sana kwenye spare, ninachoipendea Jetta ni urahisi wa kuipimp ina pimpika vizuri sana..
Hao wanaokwambia Jetta itakusumbua spares hawazijui hizo gari. Jetta ya 2006 ni sawa na VW Golf Mk5 au VW Touran au Audi A3 ambazo spares zake zipo Tz kibao na bei ni nzuri. BMW is more expensive to maintain than VW so go for Jetta.
 
Volkswagen Touareg nazikubali sana, changamoto za kumiliki gari hii ni zipi? ya 3100cc consumption yake ya mafuta ikoje?
 
Volkswagen Touareg nazikubali sana, changamoto za kumiliki gari hii ni zipi? ya 3100cc consumption yake ya mafuta ikoje?
Usiwe na hela ya mawazo tu. 3200cc usitegemee itumie mafuta kama Passo. Kifupi kumiliki hii gari usiwe na hela ya mawazo.
 
RRONDO,
Naomba kujua gari ya Toyota Isis ya mwaka 2008 Engine Oil ipi ni nzuri kwa ajili ya kuifanyia service? Halafu matairi yake ni 195/65/R15 kiasi gani cha upepo ni sahihi kwa magurudumu haya (tubeless)?
 
Naomba kujua gari ya Toyota Isis ya mwaka 2008 Engine Oil ipi ni nzuri kwa ajili ya kuifanyia service? Halafu matairi yake ni 195/65/R15 kiasi gani cha upepo ni sahihi kwa magurudumu haya (tubeless)?
Toyota Isis sina uzoefu nazo mkuu
 
Naomba kujua gari ya Toyota Isis ya mwaka 2008 Engine Oil ipi ni nzuri kwa ajili ya kuifanyia service? Halafu matairi yake ni 195/65/R15 kiasi gani cha upepo ni sahihi kwa magurudumu haya (tubeless)?
Kama sikosei Gari zote kuanzia 2002 oil nzuri ni synthetic Haswa ya Total
 
RRONDO, Mkuu hi td5 ulaji wake wa mafuta unaweza kuwa Kama TDI 200 au 300? Naomba ushauri Kuna moja td5 imesimama vyema imeua injini je overhaul, crankshaft na mengineyo ktk injini vyaweza cost bei gani?
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom