Tunaomiliki magari ya mzungu tukutane hapa

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,824
Wale wamiliki na wanaopenda kumiliki magari ya Mzungu tukutane hapa kwa ushauri na kubadilishana mawazo. Najua ni changamoto sana kumiliki haya magari hapa Tanzania kuanzia mafundi, spare na uchumi vilevile. Nina uzoefu mkubwa sana kwenye haya magari.

Niulize chochote kuhusu magari haya nitakujibu kwa uzoefu wangu. Karibuni tujadiliane. Jitahidi kununua gari isiozidi miaka 10 kwasababu vitu vingi kwenye gari vinachoka baada ya miaka kumi.

Maoni ya wadau:
Mungu amenijalia nimetumia VOLKSWAGEN KHARMANN GHIA (ya kizamani sana hii)
Peugeot 504 pick up, Land Rover 110 TDi, Mercedes Benz E190, ML500, E200 (W210),Volkswagen Golf MKIV, AUDI A4, na VOLKSWAGEN TOUAREG 2.5.

Hizi ni gari za ukweli, changamoto tu ni gharama za maintanance.

Mafuta pia inategemea na ukubwa wa engine, nyingi za 4 cylinders,ulaji wake ni kawaida sana.

Mfano hiyo Mercedes Benz E200 ni CC1990 bila kompressor ya mwaka 1998, full tank petrol ni 60 ltrs, natoka nayo Dar mpaka Arusha inasalia chini kidogo ya robo tank.

Hiyo ML500 ni almost 5000cc V8 petrol , full tank 95ltrs Dar - Arusha,taa ya mafuta itawaka na salio la lita kama 10.

Hapo zote mshale unacheka kati ya Kph 120 mpaka 160,kisha kidogo 180 na mara chacheee nafika mpaka 200 kwenye maeneo huria na barabara tulivu kama lami ya Korogwe mpaka Same.

Volkswagen ulaji wake wa mafuta naona ni chini zaidi kulinganisha na Benz,pia hata maintanance ya VW iko nafuu.

Kwa ujumla gari za mzungu wa ulaya Nzuri sana,kupata uhalisia,,, endesha au Basi hata safiri nayo ukiwa abiria,,, Safari ya masafa marefu utafurahia zaidi kuliko towntrip...

Na sasa nazimia sana Range Rover Autobiography toleo la kuanzia 2013 kuja mbele,na Bentley Arnage T2 (2007-2009) na Bentley Mulsanne.

One day Yes kwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu Muumbaji wa mbingu na nchi,bahari na chemchemi za maji na vyote vilivyomo.
Mkuu kuna hizi VW Touran Golf za cc 1600,1400 na 2000. Kwanza kati ya hizo,ipi ni nzuri. Wadau wengu wanasema hayo magari yanasumbua sana. Lakini kipekee nayapenda mwenokano wake pamoja na speed. Je gari hizo spea zipo!? Je hazina changamoto ya kusumbua mifumo ya umeme,engine,gia box? Mafundi wapo na ni wabobezi au ikoje? Zipo kuanzia 2005 na kibongobongo angalau 2010 inakua poa. Naomba info,nitashukuru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
X3 2.5i au 2.5si sio mbaya kama huna hela ya mawazo kwenye wese,spare kama kawaida gari za Mzungu zipo juu. X3 roho ya paka na zipo mjini kitambo so sio issue sana kwenye ufundi.
Kwenye wese unamaanisha kwamba mtu ajipange au? Kwamba consumption si ya kitoto?
 
Bavaria, Kijana amemaliza chuo, amekomaa na forex akapata 20'000$. $20,000 on the road? That's nearly Tshs 50m. Anaweza kupata 2008-10 VW Touareg Tdi au V6 Petrol, Mercedes M class W164 2007-10 diesel or petrol au BMW X5 E70 2008-10 3.0si
 
Naona unatutisha tukae mbali. Hio hata ukipewa bure inabidi uwe na hela otherwise mtoaji aendelee kuihudumia.
Napenda sana magari ila sipendi hadi bovu, bora nipaki nipande bajaji au Uber au daladala.

Mtoa zawadi ana fahamu kuwa zawadi ikishatolewa inatakiwa itunzwe....

Kwani Euro 900 ni sawa na Tsh ngapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom