Tunaomba wabunge wanasheria wawasaidie hawa vijana kwa hili: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaomba wabunge wanasheria wawasaidie hawa vijana kwa hili:

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kimboko, Sep 14, 2012.

 1. K

  Kimboko Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salaa, wanajukwaa.

  Naamini mko makini.

  Mwaka jana (2011) lilipita panga lisilo na haki pale TASAF, madereva karibu wote walivunjiwa mikataba yao kwa sababu ya kuuzwa magari chakavu.

  Waliahidiwa kurudishwa kazini punde nafasi zikitokea.

  Nimeshangazwa na taarifa ya bwana mdogo wangu ananiambia eti tasaf wanetangaza hizo ajira badala ya kurudisha wale wale madereava wa zamani!! Je hamuoni kuna hujuma zinataka kufanyika hapo ya kuweka watu wa vimemo sasa au la mtu mwenye rafiki yake, ndugu yake ndo anataka kutumia hiyo loophole ya uzembe wa madereva wa zamani kutojuwa mbele wala nyuma ili kudai haki zao.

  Nashangazwa sana na hawa jamaa kwa sabau ingekuwa ni mimi aisee ingekua kuna kesi kubwa sana inanguruma kudai hayo madolari.

  Naomba kama inawezekana kuwasaidia hawa vijana wakarudi kazini kwa wale at wenye sifa basi ili isionekane kwamba huyo mkurugenzi wao waliomweka kwa maslahi yao hana upendeleo na asipowarudisha kwa kweli ndo itajulikana kabisa alikuwa na kinyongo nao ata kbla hajapata hiyo nafasi.

  Naomba waheshimiwa muwakumbushe viongozi wenzenu dhana ya utawala bora ili hii nchi iende mbele na si kuirudisha nyuma kwa undugunisation na urafikinisation.

  Asante kwa kujali najua mtafanyia kazi ombi hili.
   
Loading...