mchumihalisi
Member
- Oct 8, 2015
- 28
- 98
Najaribu kuvuta kumbukumbu na kumbukumbu hizi zinanirudisha nyuma mpaka Oct 2018 wakati Rais wa awamu ya tano Dkt John Magufuli alipoagiza kukusanywa kwa Wakulima korosho zote na baadhi ya Wanunuzi kufungiwa kwa sababu ya mazingira mengi ya kutunyonya sisi wakulima ikiwemo ‘Kangomba’ ambayo sio tu haikua na afya kwetu lakini ilikua inalenga kutudidimiza zaidi Wakulima.
Wakati tukiwa kwenye giza totoro la Korosho zetu likiendelea ndio tukawaona watu wanaitwa SIBATANZA ambao hawa walikuja kununua Korosho ambazo watu walishindwa kununua kutokana na suala la bei, SIBATANZA walinunua hizi kwa mwaka 2018/2019 baadae mwaka 2020 walinunua Zaidi ya tani 100,000 na huyu ndie alikua mkombozi kwa sisi Wakulima wa Korosho kusini.
Tuko mwaka 2021 na kampuni inayonunua tani nyingi za Korosho huku ni hii SIBATANZA, Kinachouma Zaidi ni kuhusu ‘wapiga dili’ambao walizoea kutunyonya Wakulima wa Korosho kuanza kuwahusisha SIBATANZA na viongozi wakubwa wa Kiserikali. Nia yao nini? SIBATANZA wasuse waondoke ili wakulima turudi kuteseka tena na bei za ajabu? Au kumchonganisha Rais na Watendaji wake wanaomsaidia majukumu?
Kama kuna muda ambao Wakulima wa Korosho Kusini tumenufaika ni huu uwepo wa hawa SIBATANZA lakini kama tukiendelea na hizi chokochoko za sababu kikundi Fulani cha watu Fulani kinashindwa kupiga ‘deal’ na kuamua kuturudisha huko tulikotoka basi wanatukosea sana sisi Wakulima lakini ni Dhahiri tunaweza kuwakosa wawekezaji wengi kwa kuendekeza mdomo na kuwachonganisha Viongozi wakuu wa Serikali na Wawekezaji mbalimbali wanaokuja nchini.
Salum Hassani Nandonde
Nkunya, Newala.
Nov 23rd 2021.