Tunaomba msaada kwa wanasiasa na watu wenye fedha zao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaomba msaada kwa wanasiasa na watu wenye fedha zao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BabaH, Mar 2, 2008.

 1. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tunakuomba wewe mtanzania, Kiongozi mwanasiasa, Tajiri na mwenye uwezo wa aina yoyote ile, utuwezeshe kwa namna yoyote ile tuweze kuponya maisha ya huyu ndugu yetu, Pia tunakuomba raisi hawa ndo watu wa kuwasaidia

  Haya ni Maelezo ya Binti huyo na picha ziko chini hapo,
  Admin naomba kuiweka hapa utaitoa maana hapa watu ndo wanasoma sana  Ukimuona kwa sura, ni msichana mzuri mwenye macho ya kuvutia, lakini masikini hana raha ya maisha! Mtoto Sofia James Mwiga (17, pichani)mkazi wa Manispaa ya Tabora nchini Tanzania anaishi kwa mateso kufuatia ugonjwa wa ajabu wa kuvimba miguu hali iliyomfanya ajione mpweke machoni mwa jamii huku akishindwa kuanza shule.

  Licha ya baba yake kumtafutia matibabu kwa zaidi ya miaka 10 bado hajafanikiwa kwani kila Daktari anayemfanyia uchunguzi hutoa maelezo kuwa hapa Tanzania hawezi kufanyiwa oparesheni isipo kuwa nje ya nchi ambako kuna Wataalam na vyombo vya kitabibu vya kisasa..

  Kutokana na umasikini alionao baba mtu ameshindwa kumsaidia badala yake amebaki akisubiri miujiza ya mungu ishuke pengine atapata mfadhili atakaye weza kumsaidia kupata matibabu hivyo anawaomba wasamaria wema popote duniani waweze kumsaidia kuokoa maisha ya mtoto wake huyo.

  Hivi sasa mtoto huyu yupo katika hospitali ya Lugalo, jijini Dar es salaam akisubiri atakayeweza kujitokeza na kumsadia kupata matibabu sahihi nje ya nchi, kwa mujibu wa mdaktari, anahitaji operation ya kuondoa nyama hizo zilizozidi……………..mungu kama amekupa, basi kumbuka na wenye shida….naamini kunamtu hapo anaweza kubadili masiha ya msichana huyu kwa uwezo wake mola! namba ya simu ya baba mzazi wa msichana huyu ni

  +255 0753 916690

  Tunaomba msaada wenu ndugu na jamaa tunusuru maisha ya huyu mtanzania
   

  Attached Files:

Loading...