Tunaomba Mdahalo na Lowassa

respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,557
3,832
Wakuu salam

Naam kwasasa Jf inatakribani ya wapigakura laki sita (600.000) ambao wako active. Kwa mgombea atakayefanikiwa kuwashawishi member wa Jf ni wazi atakuwa na kura za kuanzia ambazo ndizo nilizoweka hapo juu.

Tumeona Watia nia wa Urais wakipita huko na huko kujaribu kushawishi Makundi mbali mbali ya Jamii ili wapate kuungwa mkono kwa nia yao hiyo.

Tumeona Ndg Edward Lowassa akiitisha press na Wahariri wa vyombo vya habari akielezea yale ambayo anaona yanaweza kumjenga ktk nia yake ya kuutaka Urais. Na akatoa ahadi ya kutia nia Rasmi huko Arusha tar 30/05/2015 kimsingi tayari amekwisha tia nia, ila siku hiyo anakwenda kuzindua rasmi

Kwa kuzingatia hilo tunaomba Mdahalo kati ya Lowassa na Member wa Jamiiforums, ili pamoja na mambo mengine tuweze kumuuliza maswali ambayo yamekuwa na dukuduku kwa wapiga kura wengi si tu hapa Jf, bali Tanzania kwa ujumla. Utengenezwe utaratibu uwe wa kumshawishi Lowassa mwenyewe kujisajili hapa au atumiwe maswali ambayo akiyajibu, majibu yake yawekwe hapa ili kukonga nyoyo za Watanzania member wa Jf.

Likifanikiwa hili tusiishie tu kwa Lowassa tuombe Midahalo kwa Watia nia wote wa ccm na Upinzani.

Wakuu nawasilisha

BACK TANGANYIKA
 
Huyo jamaa anaogopa macho ya watu
humu hawezi kuja kwa jina halisi ila anawezekana yupo kwa njia nyingine na wapambe wake wapo
 
Atawezaje kutembeza bahasha kwenye jukwaa huru kama hili?
Hamna shaka kuwa ombi lako halitekelezeki kabisa.
 
respect wa boda

Naunga MKono hoja lakini ina walakini kidogo, hapa naona kila mtu ameona mgombea urais amekua lowassa....!! kwa kweli katika chama chake kuna watia nia zaidi ya 10...mbona mchakato uko kwa level ya chama kwa sasa ambao kimsingi nadhan wanachama wa chama husika

kwa sasa wana kazi ya kuchuja mgombea na kumleta kwa watanzania....hapo sasa tuombe mdahalo atakae teuliwa na ccm, au UKAWA au chama kingine....midahalo iwe huko kichama kwa wakati huu....!! hapa naona tunavurugwa....sana naona ktk ccm kuna watia nia zaid ya 10 tunaitaji atakae tia nia na kukubaliwa na chama chake......!!
 
Last edited by a moderator:
Yaani mtukufu Rais mtarajiwa wa Tanzania aje kufanya mdahalo na misukule ya Bavicha kama mtoa hii mada?
 
Kinana ndiye Rais ajaye kwani yeye na Rais hawakukutana
11140344_976479889064364_1889046711097854598_n.jpg
 
Naunga MKono hoja lakini ina walakini kidogo, hapa naona kila mtu ameona mgombea urais amekua lowassa....!! kwa kweli katika chama chake kuna watia nia zaidi ya 10...mbona mchakato uko kwa level ya chama

kwa sasa ambao kimsingi nadhan wanachama wa chama husika kwa sasa wana kazi ya kuchuja mgombea na kumleta kwa watanzania....hapo sasa tuombe mdahalo atakae teuliwa na ccm, au UKAWA au chama kingine....midahalo iwe huko kichama kwa wakati huu....!! hapa naona tunavurugwa....sana naona ktk ccm kuna watia nia zaid ya 10 tunaitaji atakae tia nia na kukubaliwa na chama chake......!!

Mkuu tukishindwa kujua na kukosoa mawazo yao sasa wangali Watiania wa Urais kupitia vyama vyao wakiishakupitishwa na vyama vyao hatutakuwa na option nyingine zaidi ya kuchugua mbovu kati wabovu..!!!

Halafu mkuu naona umesoma nusu ya bandiko hili,Hapo chini nimeandika kwamba "Kama hili likifanikiwa tusiishie kwa Lowassa pekee, twende kwa wagombea wote wa vyama vyote" Kwahiyo utaona kwamba Lowassa ndiye ninayempendekeza kuanza na sababu za kufanya hivyo nimeziweka wazi kwenye hilo bandiko langu hapo juu.

Kuhusu kufanyika kwa Midahalo ya kivyama, hilo sinpingamizi nalo. Lakini hapa tukumbuke Tunakwenda kuchagua Rais wa Nchi si wa Chama fulani. Hivyo wakati midahalo ya kivyama ikiendelea kwenye vyama vyao pia isitunyime nafasi ya sisi kufanya midahalo kuwahusu wagombea haohao.

Hii itasaidia hata kwa vyama wanavyotoka kujua vile wagombea wao watarajiwa wanavyochukuliwa na hadhira ya Umma huku mitaani. Kwa kufanya hivyo utaona namna tutakavyowawezesha wenye vyama kutuletea mgombea bora zaidi.

BACK TANGANYIKA
 
Respect wa boda huna hadhi ya kufanya mdahalo na Lowasa

Ila wachoma mahindi, waendesha mikokotena na wanywa viroba wana hadhi ya kumpigia kura. Inakuwaje mtu apandishwe hadhi kwa kura za walala hoi halafu waliompandisha wakose hadhi ya kuongea na waliyemchagua?
 
Respect wa boda huna hadhi ya kufanya mdahalo na Lowasa

Kama kawaida yako, Kwahiyo wenye hadhi ya kufanya Midahalo na Lowassa ni Mataahira kama wewe? kwi kwi kwi...!!!!!

Kwahiyo laki si pesa, Lowassa hana hadhi ya.kupata kura yangu?

BACK TANGANYIKA
 
CCM hatufanyi mdahalo huku, kuna sehemu maalum na vyombo vyote vya habari vinakuwepo...ili wananchi wengi wasikie na kuona...

Umeandika kiukuda zaidi against Lowassa..., kwani JF kuna mgombea yeyote wa chama chochote alifanya mdahalo..!!? Coz sio sehemu sahihi kwa wengi na kwa maslahi ya nchi...nachoona ni ma.vi tu umeandika kumchimba Lowassa, ur not fair, as well this is not a right place for debate or direct questions..

It seems ur totally in a wrong place and fairness IF U WANNA HAVE DEBATE TO POLITICAL FIGURES LIKE LOWASSA AND OTHERS...!!!
 
Politically, socially and legally, tayari Lowassa kashaupata URAIS kwa scandal ya Richmond...sbb hakuchukua chochote...acha kuwa kipofu wa ubongo..heri uwe kipofu wa macho kuliko ubongo...utabeba boga upstairs..!!!
Tumsubiri Lowasa tarehe 30.05.2015 aweke ukweli kuhusu Richmond halafu Dr. Mwakyembe naye awake wazi yale aliyoyaacha ili kulinda heshima ya Lowasa hapo ndio mbichi na mbivu zitajulikana. Na tutajua kwa nini baba wa taifa mwalimu JK Nyerere alimkataa Lowasa
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom