Tunaomba kujua Wasifu wa Jenerali Kombe

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,783
Wasalaam,

Nimekuwa nikisikia taarifa mbalimbali zisizo rasmi kuhusu huyu Mzee wetu, Marehemu Jenerali Imran Kombe. Kuna wazee tofauti tofauti ambao waliwahi kukaa naye karibu wakati wa uzima wake: Wengine waliwahi kusoma naye shule, kuna moja aliwahi kusema "Kombe alikuwa ni moja kati ya Watanzania wenye akili sana sanaa" na mwingine alisema "Kombe alivyouawa kuna mambo mengi sana yameharibika kwenye ulinzi hapa nchini"

Binafsi ninapenda kujua wasifu (ALIKUWA NI MTU WA AINA GANI) wa huyu jamaa wakati wa Uhai wake. Maana alishika nafasi nyeti (Ukurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa) sana wakati nchi yetu iko katika kipindi kigumu cha mpito: (Kutoka kwenye mfumo wa Ujamaa na Chama kimoja kuelekea mfumo wa Kibepari na vyama vingi)

Nawasilisha!
 
Hayati Meja Jenerali Imran Kombe"Kamanda Ngono"-Alikusanya vikosi vyake kuingia Uganda kuvuka mto mkorofi wa Ngono(mgonjwa wa kwanza wa HIV duniani inahisiwa alitoka kando ya mto huu)Alipata sana shida ya vikosi vyake kushambuliwa na wadudu wahasa wakati wa usiku lkn akaingia Uganda tayari kwa mapambano!Gen Kombe aliuliwa na polisi kwa tuhuma kuwa ni mwizi sugu wa magari!!!!!
 
Hahahaa umenikumbusha kifo chake alifutiliwa kuanzia dar hadi moshi akaenda kupugiwa risasi kwenye shamba la mahindi
 
Hayati Meja Jenerali Imran Kombe"Kamanda Ngono"-Alikusanya vikosi vyake kuingia Uganda kuvuka mto mkorofi wa Ngono(mgonjwa wa kwanza wa HIV duniani inahisiwa alitoka kando ya mto huu)Alipata sana shida ya vikosi vyake kushambuliwa na wadudu wahasa wakati wa usiku lkn akaingia Uganda tayari kwa mapambano!Gen Kombe aliuliwa na polisi kwa tuhuma kuwa ni mwizi sugu wa magari!!!!!
Ana nyumba maili 6 moshi na ndio huko huko walienda kummaliza mbele ya geti lake akishuka garini.
nilikuwa mdogo kipindi hicho ndugu wakaenda msibani mi nikabaki kuangalia katuni
 
Hayati Meja Jenerali Imran Kombe"Kamanda Ngono"-Alikusanya vikosi vyake kuingia Uganda kuvuka mto mkorofi wa Ngono(mgonjwa wa kwanza wa HIV duniani inahisiwa alitoka kando ya mto huu)Alipata sana shida ya vikosi vyake kushambuliwa na wadudu wahasa wakati wa usiku lkn akaingia Uganda tayari kwa mapambano!Gen Kombe aliuliwa na polisi kwa tuhuma kuwa ni mwizi sugu wa magari!!!!!

Hapana , umemshushia heshima.

Imran Kombe alistaafu akiwa na cheo cha Luteni Jenerali.
 
Naikumbuka CV yake ya jeshini tu,

Kombe alikuwa miongoni mwa makamanda Cream waliowahi kutokea katika historia ya JWTZ.

Kama sijakosea yeye na Mayunga pekeyao ndio makamanda wa divisheni katika vita ya kagera ambao wamefikia cheo cha luteni jenerali.
 
Back
Top Bottom