Tunaomba Kanisa Katoliki na KKKT watusaidie kukemea uvunjaji wa Katiba unaofanywa na Spika wa Bunge na Naibu wake

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,155
2,000
Kwenu Maaskofu, Amani ya BWANA iwe nanyi,

Ni matumaini yangu, mnaendelea salama na kwa amani tele katika majukumu yenu ya kuwapa chakula cha roho kondoo wenu.

Nimeonelea leo niongee nanyi ili kuwaomba wazee wetu mtusaidie sisi Wananchi wenzenu ambao wengi ni kondoo wenu katika tatizo hili kubwa sana lililotokea katika nchi yetu ambapo kuna watu wamejiinua na kutenda udhalimu wa wazi wa kubomoa misingi ya nchi yetu kwa kuvunja Katiba waziwazi tena kwa kibri kikubwa! .

Ndugu Maaskofu: Sisi wananchi twawategemea nyinyi siku zote kusaidia kuwarudisha watawala katika msitari na mmekuwa mkitetea haki bila woga kwa sababu mtawala asiyekemewa akikosa basi hujiona kuwa yeye hakuna cha kumzuia katika nchi na hivyo huendelea kufanya ufedhuli juu ya ufedhuli hadi kufikia kuitumbukiza nchi mahali pabaya.

Ndugu Maaskofu: Mlisimama kidete kuukemea utawala wa Magufuli juu ya haki za binadamu na demokrasia, Japo utawala ule haukupenda hivyo vitu lakini ilisaidia kupunguza kwa kiasi fulani matendo ya watu wasiojulikana!

Na mlisimama kidete kwenye suala la Korona na kuwataka waumini waanze kuchukua tahadhari, na kwa kiasi kikubwa maagizo yenu yalisaidia kupunguza kiwango cha maambukizi ambacho kilikuwa katika viwango vibaya kabisa mwezi January hadi March mwaka huu

Ndugu Maaskofu: Katiba ya nchi ni jambo nyeti, sisi wananchi tunatambua wazi, kuwa kuchezewa kwa katiba huwa hakuna mwisho mwema.

Nawaombeni, kama vile mlivyokwisha kufanya kazi nzuri za kichungaji huko nyuma kukemea ujinga, ushenzi, uonevu na dhulma, Nakuombeni msimame sasa kwa ajili yetu tena MTOE NYARAKA ZA KUKEMEA UVUNJAJI HUU WA KATIBA UNAOFANYWA NA SPIKA WA BUNGE NA NAIBU WAKE kwa kuruhusu watu wasio wanachama wa chama chochote kuwa Wabunge!

Ndugu Maaskofu: Utaratibu uliotumika na chama cha CHADEMA kumjulisha spika juu ya kufutwa uanachama waliokuwa wanachama wake ndiyo huohuo uliowahi kutumiwa na vyama vya CCM na CUF katika suala linalifanana!

Ndugu Maaskofu: Pengine wapo watakaodhani hili ni suala la kisiasa tu liachwe hukohuko kwenye siasa. La hasha hili si suala la kisiasa, hili ni suala la KIKATIBA, na katiba ikivunjwa wazi huku nanyi mnashuhudia ba msiseme neno, basi mtakuwa mnasaidia uwezeshwaji wa uvunjifu wa katiba mkubwa zaidi huko mbele maana precedent imewekwa. Ila mkikemea hili, basi hata huko mbeleni wenye kukusudia kubunja katiba watafikirua mara mbilimbili

Ndugu Maaskofu: Nyie ni wadau wetu sisi wananchi katika kujenga taifa Huru zaidi na la Haki zaidi na la Maendeleo zaidi. Ninaleta ombi hili maalum kwenu mtusaidie wananchi, maana Spika na Naibu wake wameamua kutudharau na hatuna cha kuwafanya, Wana Kinga na hawashitakiwi popote!
 

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,362
2,000
Kama ndugai kawa spika wa bunge la Tanzania basi hamorapa anaweza akawa rais na akatupeleka uchumi wa kati wa juu.
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
7,051
2,000
Kwenye kichwa habari kinge someka viongozi wa dini wote. Usibague kwamba ni Katholic na Lutheran.
Hili jambo la Jobo lima hitaji kukemewa na kila mppenda demokrasia.
Tukikaa kimya kila kiongozi ataifanya hii nchi kama bakuli la pombe za kienyeji.
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
3,127
2,000
Tumechoka na ujinga wenu kama mnaona wanavunja katina si muende mahakamani itafsilie hiyo sheria?
Sasa mnawambia kanisa kazi yao ni kutafsili sheria?
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,155
2,000
Kwenye kichwa habari kinge someka viongozi wa dini wote. Usibague kwamba ni Katholic na Lutheran.
Hili jambo la Jobo lima hitaji kukemewa na kila mppenda demokrasia.
Tukikaa kimya kila kiongozi ataifanya hii nchi kama bakuli la pombe za kienyeji.
Tatizo BAKWATA wao wanatetea chochote cha serikali ndiyo maana sijawahusisha.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,155
2,000
Tumechoka na ujinga wenu kama mnaona wanavunja katina si muende mahakamani itafsilie hiyo sheria?
Sasa mnawambia kanisa kazi yao ni kutafsili sheria?
Mahakamani kuna akina Biswalo, walewale waliotumika kukandamiza haki za watu sasa wamegeuka majaji.

Pia kulinda KATIBA ya nchi si kwa ajili ya CHADEMA bali ninkwa ajili ya nchi nzima, kwa hiyo ni muhimu kila mpenda nchi hii kukemea Ujinga na udhalimu huu wa waziwazi
 

kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
1,359
2,000
Sisi Islam,Sabato,Kakobe,Jehovah Witness,Anglikana,Morovian,Mzee Wa Upako,TAG,EAGT,Mwamposa,Mwingira,Gwajima Answar Sunna,Bakwata na Wengi wengine tusingependa kulishuhudia Jambo hili kutokea..... Karne hii tulishasahau UDINI.
 

Mulama

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
2,789
2,000
Tanzania hakuna viongozi wa dini kuna viongozi wa serikali ya ccm wanaokaa na kufanyaia kazi kwenye nyumba za ibada usisumbuke ndugu yangu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom