Tunaomba julishwa:Kuna vijumba vidogo kama model vimejengwa nje ya nyumba za bagamoyo:ni vya nini?

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,260
7,195
Kwa waliotembelea nyuma za watu wa pwani,watakuwa wameona vijumba kama vya kuchezea watoto ktk kaya za watu wengi mkoani pwani.Vijumba hivyi vimeezekwa kwa amkutu, mabati na nyasi, na ukubwa wake hauzidi ukubwa wa ndoo ya kuchukulia maji.Je nini maana yake?
 
kwa waliotembelea nyuma za watu wa pwani,watakuwa wameona vijumba kama vya kuchezea watoto ktk kaya za watu wengi mkoani pwani.vijumba hivyi vimeezekwa kwa amkutu, mabati na nyasi, na ukubwa wake hauzidi ukubwa wa ndoo ya kuchukulia maji.je nini maana yake?
hizo ndiyo nyumba ndogo wewe hujui tu
 
Mkuu,
Tuwekee picha basi.

Sikuweza chukua picture mkuu ,devices zangu zote hazikuwa na charge.Ila nadhai soon tutapata mtu wa kutututumia pamoja na maelezo.Vingi vina urefu kama wa 2inches, na radius ya kama 1/2 inch.Vingine vimewekewa paa kwa ustadi mkubwa sana,nimeone vingine vina bati expensive,vingine makuti yamewekwa kwa ustadi mkubwa sana ila pembeni havijazibwa.Kwa ukubwa wake ni kuku wawili au watatu tuu wanaweza pata shade kipindi cha jua ila hata mtoto hawezi ingia.

Kuna maeneo vinaonekana hadi vitatu,maeneo mengine viwili huku pakiwa na mchanganyiko wa design na meterial waliyotumia.
Its interestiing kwa ni kwa ustadi wa kutengeneza na unadhifu unaonekana si rahisi kufikiri ni sehemu ya utundu wa watoto.
 
vinaitwa vibanda vya kinyankela au vinyankela,ni vibanda vinavyohusiana na ushirikina ,wanavijenga kwa ajili ya hao vinyankela ni kama nyumba za vinyankela, wanatumia kwa ajili ya kutambikia wakati mwingine wanaweka mayai au sarafu ndani ya hivyo vibanda na mtu huruhusiwi kuchukua kitu chochote ndani ya hivyo vibanda(wenyewe wanasema ukichukua utapata madhara) zamani vilikuwa vingi sana maeneo ya Pwani lakini siku hizi vinapungua.
 
Kwa waliotembelea nyuma za watu wa pwani,watakuwa wameona vijumba kama vya kuchezea watoto ktk kaya za watu wengi mkoani pwani.Vijumba hivyi vimeezekwa kwa amkutu, mabati na nyasi, na ukubwa wake hauzidi ukubwa wa ndoo ya kuchukulia maji.Je nini maana yake?
...Nicholas; Hivyo vijumba vidogo ni utamaduni wa makabila yaliyoko mkoa wa pwani zaidi hasa wazaramu na Wakwere. Wao wanaamini kwenye kitu kinaitwa kinyamkela kaya nyingi za kizaramo na kikwere huchukulia kinyamkela kama njia ya kuabudu mizimu yao. Ofcourse hufanya matambiko kila baada ya kipindi fulani na hili tambiko linapofanyika uhusisha ngoma inayoitwa madogoli ambapo hiyo tambiko kufanyika na vitu mbali mbali kutolewa sadaka kama vile vyakula, baadhi ya sarafu za kizamani zile zenye tundu kati kati. Wao huheshimu sana hivi vibanda lakini mwisho wa siku kwa imani zao zaidi otherwise hakuna cha ajabu mle unaweza hata kukichapa teke na kusitokee lolote..."usije kuwa kama yule dogo aliyekojolea nanihii"
 
Nashukuru kwa maelezo mazuri.Kwa kweli ukivitazama utaona kuwa haviwezi kuwa ya mtoto mdogo, na haviwezi kuwa model km wanazokuwa nazo architects .Very interesting.

Unaweza vichapa teke wakikuuzia na kuwahamisha.na wasione kwani habari zikienea ujirani utakuwa mgumu sana.
 
vinaitwa vibanda vya kinyankela au vinyankela,ni vibanda vinavyohusiana na ushirikina ,wanavijenga kwa ajili ya hao vinyankela ni kama nyumba za vinyankela, wanatumia kwa ajili ya kutambikia wakati mwingine wanaweka mayai au sarafu ndani ya hivyo vibanda na mtu huruhusiwi kuchukua kitu chochote ndani ya hivyo vibanda(wenyewe wanasema ukichukua utapata madhara) zamani vilikuwa vingi sana maeneo ya Pwani lakini siku hizi vinapungua.

Nashukuru sana kuyaelewa haya.Ni miaka mingi sana nilikuw anaona,ila mara zote niliona hizo nyumba zikiwa na watoto wengi kwa hiyo nilijipa jibu kuwa itakuwa ni watoto wanajifunza jenga kama wakubwa wanavyojenga nyumba za kuish.This time around nilijikuta najiuliza zaidi na zaidi.
 
JK na Rizwani wanaweza kuwa navyo katik kila nyumba walizojiwekea?Sidhani kama ktk hawa kuna mpagani kabisa,almost kila mtu ana dini hata ya mazoea kt ya Ukristu na Uislam huku wengi waliwa waislam ,sasa hii inakwenda vipi na imani zao za dini?
 
Kwa waliotembelea nyuma za watu wa pwani,watakuwa wameona vijumba kama vya kuchezea watoto ktk kaya za watu wengi mkoani pwani.Vijumba hivyi vimeezekwa kwa amkutu, mabati na nyasi, na ukubwa wake hauzidi ukubwa wa ndoo ya kuchukulia maji.Je nini maana yake?

Cheya watu wa Pwani wewe?
Kwa jibu sahihi muulize mkuu wa kaya!
 
Vingi vina urefu kama wa 2inches, na radius ya kama 1/2 inch.Vingine vimewekewa paa kwa ustadi mkubwa sana,nimeone vingine vina bati expensive,vingine makuti yamewekwa kwa ustadi mkubwa sana ila pembeni havijazibwa.Kwa ukubwa wake ni kuku wawili au watatu tuu wanaweza pata shade kipindi cha jua.

Mkuu wewe nawe ni kituko! yaani kwa ukubwa huo unafikria kuingiza kuku wawili au watatu? Ulisoma wapi hesabu za vipimo wewe?
 
JK na Rizwani wanaweza kuwa navyo katik kila nyumba walizojiwekea?Sidhani kama ktk hawa kuna mpagani kabisa,almost kila mtu ana dini hata ya mazoea kt ya Ukristu na Uislam huku wengi waliwa waislam ,sasa hii inakwenda vipi na imani zao za dini?

........enyi watu !(all human being !) Muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu (Adam na Hawa) ili mpate kuokoka. Qur'an: 2:21.

........na shikeni sala, toeni zaka, na inameni pamoja na wanao inama. Qur'an: 2:43

.......na tafuteni msaada kwa kusubiri na kusali: na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu. Qur'an: 2:45.
 
Vingi vina urefu kama wa 2inches, na radius ya kama 1/2 inch.Vingine vimewekewa paa kwa ustadi mkubwa sana,nimeone vingine vina bati expensive,vingine makuti yamewekwa kwa ustadi mkubwa sana ila pembeni havijazibwa.Kwa ukubwa wake ni kuku wawili au watatu tuu wanaweza pata shade kipindi cha jua.
Mkuu wewe nawe ni kituko! yaani kwa ukubwa huo unafikria kuingiza kuku wawili au watatu? Ulisoma wapi hesabu za vipimo wewe?
Sasa mkuu kituko kipo wapi hapa?Nilivyoviona ni kweli ni vidogo,na nilipojaribu kiuliza kama inawezekana vikaya ni kwa ajili ya kuku basi vitakuwa ni vidogo sana.Hao kuku wawili watatu ni taswira ninayotaka mpatia msomaji ambaye nataka anisaidie hilo.Kwa mwenye akili hawezi tena sema "labda ni za kuku..." kwa vile tayari nimempa clue.Hizo hesabu zako za vipimo unazotaka niambia lazima niwe nazo siadhani kama zinahitajika kihivyo.

Kwa vipimo vya vitu vinavotuzunguka mara nyingi huwa tunakadiria tukiwa na precision nzuri sana.Sijui ulishawahi uliza nyumbani akina mama wanavyopika vitu vingapi huwa hawapimi ila mwisho wa siku chakula huwa almost perfect?Kuanzia nyanya,vituu,mafuta, maji, chimvi ,unga etc .Vivyo hivyo hata wauza nyama na wengine,huwa wanakata kipande kwa makisio na huishia kuongeza kidogo sana kama si kupunguza kidogo.Hao hawajasoma hicho unachotaka sema na mwishowe wake huwa wanakuwa hawajakatakata Nyama hovyo.

Sijui ujumbe wako nini ndugu yangu?Ungefanya la maana sana kama ungetuambia nini unajua kuhusu hivyo vijumba zaidi ya approach yako ya kutafuta vitu vidogo vya pembeni kuleta ubishani.
 
Back
Top Bottom