Tunaomba dakika 30 tukajadiliane nje ya ukumbi tutarejea na msimamo wa nchi

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,428
Nimesikiliza majadiliano flani na mahojiano kuhusu kukwama kwa mambo mengi ya Jumuhia ya Africa Mashariki ambapo haya mambo yamenikera na kuniuzunisha kuyasikia kutoka kwa wawakilishi wa Taifa moja kubwa EAC.

Inadaiwa katika kila kikao Cha maamuzi wawakilishi wa Tanzania lazima waombe kutoka nje ya kikao na kujadiliana pembeni na hata wanaporudi msimamo wao huwa ni "KWENYE JAMBO HILI NAOMBA SISI KAMA NCHI TULIACHE HADI KIPINDI KIJACHO TUTAKAPOKUJA NA MSIMAMO WA NCHI YETU"

Vikao vinavyofuata pia utasikia bado serikali inalifanyia kazi na tutalileta kwa majadiliano vikao vijavyo.

Napenda wale wanaofaham namna serikali inavyofanya kazi watuelimishe, Unapomtuma mtu kwenye vikao vya nje ya nchi unamtuma mtu mwenye mamlaka ya kuamua kwa niaba ya nchi au unamtuma mwakilishi wakwenda kuandika yaliyojadiliwa na kukuletea? Kama kikao kinafahamika ni Cha viongozi wa ngazi flani na agenda za vikao zinatoka kabla ya kuingia kwenye kikao, je tunashindwaje kupata msimamo kabla ya kuingia vikaoni.

Hoja hii naona pia ikifanya kazi katika majadiliano maeneo mbalimbali ya nchi, urasimu ni mkubwa kwa sababu ya watu kuogopa kutoa maamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi kama nchi bado tuko kwenye mkakati na mkakati bado tunaufanyia kazi.
 
Back
Top Bottom