Tunaofunga Kwaresma hii tukutane hapa

Kufunga kwa mtu anayemfuata Kristo ni kila siku haijarishi nikwaresma au sio kwaresma kiukweli ni kwamba

Ukiona unaishi maisha matakatifu kipindi cha kwaresma tu wewe sio mkristo we ni mpagani tu kama wapagani wengine

Hatuwezi mkristo kufanana na upande wa pili ambao wanaacha kula nguruwe kipindi cha mfungo tu

Ukiacha kuishi maisha matakatifu kisa sio kwaresma we ni MPAGANI SIO MKRISTO
Kwaresma inakusaidia kuishi bila ya kitu kinachokutenganisha na Mungu wako.

Ukikifunga na kuishi kwa nadhiri ya kuokolewa nacho hata baada ya siku takriban 50. Bhasi itakuwa umeshinda pakubwa

Usisahau kwaresma ina vitu vitatu vikubwa

1. Sala

2. Sadaka

3. Matendo mema

Hivyo usiihukumu kwaresma kwa matendo ya waumini wake bali dhumuni la uwepo wake

Kwaresma njema mkuu
 
Ni kweli kabisa mkuu Nipo pamoja na wewe

Ila ukaribu na MUNGU ninao hata pasipo kwaresma

Na sina uhakika kama kwaresma liliagizwa na YESU na sijaona mahali wanafunzi wa YESU wakilifanya naona ni Watu wa dini walikaa wakalitunga

Uhakika wa maisha MUNGU amenipa ninao kwa kuwa kufunga kwangu ni Mara kwa Mara sitegemei tarehe flani ili eti nifunge hapana na maisha matakatifu hayategemei siku flani Bali ni kila siku
 
Pamoja sana mkuu! Utakuwa muda mwafaka sana ukimaliza hiyo saa 10 unaunga moja kwa moja kwenda kanisani. Inaonesha ni jinsi gani ulivyo Mkatoliki halisi, ubarikiwe sana na uwe na mfungo mwema!
Nashukuru asante nawe pia.
 
Leo ni Jumatano ya majivu ambapo sisi Wakristo tunaanza rasmi mfungo wa Kwaresma kwa siku 40.

Nichukue fursa hii kuwatakieni Wanabodi wote hapa Jukwaani Kwaresma yenye Baraka na Amani ya Bwana na ile ya Dunia.

Kadhalika kwa wale wanasiasa wanaoamini katika Kristo lakini kwa namna moja au nyingine wamewakwaza wananchi ama kwa kuhama vyama au kutotimiza ahadi walizoahidi hii ni fursa muhimu kwao kufanya toba mbele za Mungu.

Binafsi niwaombe radhi wale wote niliowakwaza hapa jamvini katika kutekeleza sayansi ya siasa kwani maendeleo hayana vyama.

Duniani tunapita tu hapahitaji mbwembwe.

Mungu awabariki sana!
 
Kufunga kwa mtu anayemfuata Kristo ni kila siku haijarishi nikwaresma au sio kwaresma kiukweli ni kwamba

Ukiona unaishi maisha matakatifu kipindi cha kwaresma tu wewe sio mkristo we ni mpagani tu kama wapagani wengine

Hatuwezi mkristo kufanana na upande wa pili ambao wanaacha kula nguruwe kipindi cha mfungo tu

Ukiacha kuishi maisha matakatifu kisa sio kwaresma we ni MPAGANI SIO MKRISTO
Nakazia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi hichi cha mfungo kwaresma ukiwa kwenye ibada hii ya mfungo je unaruhusiwa kuwasilana na mpenzi wako? Mimi ni muislam lakini nina mpenzi kesho anategemea kufunga nataka nifahamu mipaka yangu kwake yeye kwa kipindi hichi chote akiwa kwenye mfungo
Wasiliana nae tu mkuu, kama mlikuwa mnafanya uzinzi kabla ya kwaresma mka-pause kipindi cha kwaresma kisha kuendelea baada ya hapo hakuna kitu mmefanya. Kama hamtendi dhambi yoyote kwaresma pia haiwazuii kuwasiliana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimetoka church,.Mungu awabariki sana. Kuna ibada nyingine mchana na jioni watakaoweza wajitahidi kwenda
 
Kwaresma ni kipindi kitakatifu cha kukumbuka mateso ya bwana Yesu, wakristo tunakumbushwa kumrudia Mungu huku tukitafakari kwa kina maisha yetu katika imani. Wenzetu wana mwezi wa Ramadhani sisi tuna Kwaresma.

Tuliopanga kufunga tuwe tunapeana updates na kutiana moyo. Haijalishia utafanikiwa kufunga siku ngapi.

Pia tuambie kitu gani hutafanya kabisa mwezi huu, binafsi napanga nisiguse hata chupa moja ya ulabu au pombe ya aina yoyote.
Amina..ila kukushirikisha wewe nia yangu ya Kwaresima..ni pagumu hapo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumsifu Yesu Kristo, mm kwa ujumla wakati huu, huwa najitahidi kufunga siku zote 40.

Kama ilivyo desturi haitupasi kufunga siku ya jpili kwa kuwa siku hiyo ni Pasaka ndogo.

Vile vile tujitahidi pia kufanya matendo ya HURUMA. Kama ni mkaazi wa Dar waweza kusanya nguo zako na za watoto ambazo hauzitumii na kuzipeleka Kanisani MUHIMBILI ambako hugawia wagonjwa au ndugu za wagonjwa.

Kuliko nguo hizo kuzipigia deki au kuzitupa . halikadhalika Kuna Majirani ambao halizao siyo nzuri katika kujikimu kimaisha ni wakati wa kuonesha upendo wa Kristo .
 
Ni kweli kabisa mkuu Nipo pamoja na wewe

Ila ukaribu na MUNGU ninao hata pasipo kwaresma

Na sina uhakika kama kwaresma liliagizwa na YESU na sijaona mahali wanafunzi wa YESU wakilifanya naona ni Watu wa dini walikaa wakalitunga

Uhakika wa maisha MUNGU amenipa ninao kwa kuwa kufunga kwangu ni Mara kwa Mara sitegemei tarehe flani ili eti nifunge hapana na maisha matakatifu hayategemei siku flani Bali ni kila siku
Kristu alifunga siku arobaini na huo ndio mfano wa kwanza thabiti ambao umefuatwa. Hakuna aliyekaa kwa firkra zake binafsi akaitunga

Kingine haukatazwi kufunga katika siku za kawaida. Mfano kwa wakatholiki kuna novena ambayo mtu huweza kuisali na kufunga kwa ajili ya lolote kwa siku yoyote ili

Kumbuka Kipindi hiki ni cha kutafakari kwa kina kuhusu state ya kiroho, mahusiano na Mungu na njia aliyoitumia kristu kutukomboa.
 
Mapendo.....
Nawatakia wakristo wenzangu (waroma) duniani kote jumatano njema ya majivu na katika kipindi hiki cha kwaresma tujitahidi kujinyima, kufanya yaliyo mema na kudumisha amani na upendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom