Tunaochapika Januari baada ya kutapanya Christmas tufarijiane hapa

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
4,963
15,240
Wakuu hali ni mbaya!

Baada ya kuweka heshima vijijini huko Moshi kipindi cha Krismasi na mwaka mpya, ambapo ilikuwa ni mwendo wa kuchinja mbuzi, bia kwa wingi, na kufuru za kila aina, sasa cha moto nakiona.

Tangu Januari hii imeanza mambo hayaendi kabisa. Yaani naishi kama digidigi hapa mjini. Ndani hakuna kitu, hela imekata, yaani daaah.

Wakuu nyie vipi mnavushaje huu mwezi?
 
Huu mwezi buku inaitwa EFLU MOJA
Kuna Ada ,uniform sijui madaftari bado hela nyingi imemalizwa na sikuku bado kuna wako wa Kodi alafu kwenye biashara ndo mwezi ambao haziendi vizuri zaidi ya mikopo tuu.. Wale wajiriwa nao hela ndo ilishakata kabla ya mwaka mpya
 
TOHATO,
Daah mkuu hapa hiyo tarehe 23 kila siku zinavyoenda nayenyewe ni kama inasogea mbele haitaki kabisa kufika.
 
Wengne balaaaa aisee watoto watatu Kila mmoja 2.5m daaadek alafu masista mashulen Wana kaza na huku bia zilikuwa tamu na michepuko juu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila masista kipindi hiki hua wanatuchora sana jinsi mtu unavyoenda na kitambi chako pale halafu unaanza kulia lia.. Wanajua tu hili zembe limenywea bia ada ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
Pole mkuu,mimi nimebadilisha muda wangu wa kuonekana nyumbani,kila siku naanza kuonekana kuanzia saa 4 usiku na saa 10 alfajiri naondoka na kisingizio changu ni kuwa kazi zimeongezeka,kwakweli cha moto tunakiona...
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Leo asubuhi nimecheka sana.
Dawa ya meno imeisha sasa leo ikabidi nibomoe ile tube ya colgate niingize mswaki mle ndani nianze kuchokonoa walau mswaki upate ile harufu ya dawa. Hapo kila nikiuangalia mtungi wa gesi presha inapanda kwani unaonekana kabisa umeshanyong'onyea na muda wowote utakata. Mfukoni nna 6,000 ndio hela iliyobaki. Daah..!!!!!
 
Kwnini mkuu! Ninachapika vilivyo mvua hazikati kila kitu kimesimama!

Hahaaaa wewe kuchapika kwako ni tofauti kabisa na huku kwakwetu.. huku hali ni tete lakini ukituona mtaani huwezi amini kama ndio sisi. Halafu mimi nna tabia moja, kipindi nikichapika ndio hua nakua smart sana yaani napiga pamba kali, safi... kiatu safi na tai shingoni ukiniona utadhani mtu.๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Hahaaaa wewe kuchapika kwako ni tofauti kabisa na huku kwakwetu.. huku hali ni tete lakini ukituona mtaani huwezi amini kama ndio sisi. Halafu mimi nna tabia moja, kipindi nikichapika ndio hua nakua smart sana yaani napiga pamba kali, safi... kiatu safi na tai shingoni ukiniona utadhani mtu.๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ safi sana! Mie mbwembw nafanya nikiendaga mjini...huku muda wote uko hovyo hovyo tu yaan! Alafu ndo napenda ...sina hata ratiba za kwenda saloon!lakini ka-walet kanasoma figures nzuri!...ila ni mapito tu haya!
 
Back
Top Bottom