Tunao ujasiri wa kuwahukumu watoto wajamzito?

Jielewe

Member
Jan 10, 2017
38
125
Matukio ya watoto wa kike kupata ujauzito yanaongezeka. Kwa mujibu wa Takwimu za Elimu (BEST) wanafunzi 4,718 wa sekondari kwa mwaka 2012 na 3,439 mwaka 2015 walikatishwa masomo yao kwa sababu ya ujauzito. Takwimu kamili hazipatikani lakini kwa elimu ya msingi hali haina tofauti kubwa. Hata hivyo, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) linadai kwamba msichana mmoja kati ya sita wenye umri wa miaka 15 mpaka 19 wakiwemo wasiokuwepo shuleni hupata ujauzito kila mwaka hapa nchini. Ni wazi kuwa mimba za utotoni ni tatizo kubwa katika jamii yetu.


Aidha, matukio ya mimba yanakwenda sambamba na ongezeko la ngono holela miongoni mwa wanafunzi. Utafiti uliofanywa na Method Kazaura na Melkiory Masatu mwaka 2009, ulibaini kwamba asilimia 32 ya watoto na vijana wenye umri wa miaka 10 mpaka 19 walikuwa wanashiriki vitendo vya ngono. Wengi wao hawana elimu ya afya ya uzazi. Jarida la African Population Studies toleo Na.29 la 2015 linathibitisha matokeo hayo.


Kwa mujibu wa Eunice Muthengi na Abebaw Ferede waliofanya utafiti uliochapishwa na Jarida hilo, idadi kubwa ya vijana hapa nchini wanakosa taarifa za msingi ambazo zingeweza kuwasaidia kufanya maamuzi yanayoongozwa na uelewa. Hata hivyo, vijana hawa wanapopatiwa elimu ya afya ya uzazi mapema, asilimia 52 wanaonekana kuweza kuchelewesha maamuzi ya kuanza ngono.


Tunaishi kwenye nyakati zenye uholela mkubwa wa taarifa. Changamoto, hata hivyo, ni kukosekana kwa elimu na huduma za afya ya uzazi kwa vijana. Wazazi, kwa mfano, wameendelea kuogopa kuzungumza kwa uwazi masuala yanayohusiana na ngono kwa imani kwamba ni kinyume na utamaduni wetu. Mtoto huyu anapokwenda shuleni anakutana na walimu wasio na ujasiri wa kuyashughulikia mambo haya kwa uwazi. Katika mazingira haya ya uhaba wa taarifa sahihi katikati ya uholela wa taarifa zinazohimiza ngono, ni wazi maamuzi mengi wanayofanywa na wanafunzi yatakuwa batili.


Pia, tunafahamu watu wazima wakiwemo wazazi na walimu wameshindwa kuonesha mfano mwema wa kimaadili. Maadili yamebaki kuwa hotuba za majukwaani wakati maisha ya watu faraghani ni jambo jingine kabisa. Wazazi wanaohubiri maadili hadharani, kwa mfano, ndio hao hao wanaofuga ‘nyumba ndogo.’ Walimu waliopaswa kuwaelekeza watoto njia sahihi ya kufuata ndio wanaowashawishi wanafunzi wao kushiriki nao vitendo vya ngono. Kwa ujumla, jamii inayomzunguka mtoto inamwaminisha kuwa ngono holela ni sehemu ya maisha.

Jambo la kushangaza ni kwamba mtoto anapoiga yale anayoyaona na kujiingiza kwenye vitendo vya ngono jamii hiyo hiyo inamshangaa.
Endelea hapa.
 

Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,155
2,000
Elimu ya afya ya uzazi iwe lazima kwa shule za msingi na sekondari na wazazi waongee na watoto wao.

Sio mzazi unamuonea aibu kijana/binti yako na kushindwa kumpa elimu ya afya ya uzazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom