Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Ridhiwani Kikwete alipokuwa akijitetea mbele ya vyombo vya khabari kuwa hakuhudhuria kikao cha Mwanza ambacho Dr. Slaa alidai kiliweka mipango ya kuchakachua matokeo ya kura za uchaguzi hakutoa kielelezo hata kimoja cha ushahidi ya kuwa kweli alikuwa nje ya nchi kwenye tarehe hizo na hivyo asingeweza kushiriki katika kikao kinachodaiwa kiliendeshwa chini ya uenyekiti wa baba yake JK katika kupanga mikakati ya kuyachakachua matokeo...........................
Ninamwomba Ridhiwani atupe vielelezo vya ushahidi vifuatavyo:-
a) Nakala ya kurasa za pasipoti zenye kuonyesha mihuri ya uhamiaji ya hapa nchini na ya nchi anazodai alikwenda kuvinjari kwenye hati yake ya kusafiria ikionyesha tarehe za kuondoka nchini na kurudi........na majina ya nchi Ridhiwani anadai alikuwa amekwenda.....
b) Nakala ya risiti za hoteli alizofikia............
c) Nakala za tiketi za ndege alizopanda kwenye safari zake hizo.........
d) Nakala za hati za viapo za mashahidi wake kule nje ambao anadai alikutana nao ili kuthibitisha ukweli kama alikwenda au ni fumbo mfumbie mjinga lakini mwerevu kuling'amua........
e) Nakala za hati za viapo vya mashahidi wake ambao walimsindikiza wakati akienda na wakati akirudi zikiwemo namba za magari zilizomsindikiza na kumpokea.....
f) Ushahidi mwingine atakaona Bw. Ridhiwani unafaa kumbeba kwenye sakata hili......
Kama Ridhiwani Kikwete atashindwa kutoa ushahidi huu ni moja kwa moja ni haki yetu kuona anasema uongo na kwa kukosa utetezi yaani "alibi" basi alihudhuria kikao hicho ambacho ndicho kimeliletea taifa letu aibu kubwa ya kuchakachua matokeo ya kura za uchaguzi huu wote...................