Tunamuonea Rais Kikwete?

Alichofanikiwa Kikwete ni kuteuwa majaji wengi na kutuongezea mzigo wa kuwatunza, kumbe hamkujuwa ni kwa nini aliwateuwa majaji wengi kwa kadiri ya uwezo wake.

Tangu ile Hukumu iliyokuwa chini ya jopo la majaji 7 wakiongozwa na Jaji Mkuu na kushindwsa kutenda haki katika kesi ya mgombea binafsi nilishakatishwa tamaa na utawala wa sheria nchi hii.
 
Mshahara wa dhambi ni mauti, ukiua kwa upanga nawe utakufa kwa upanga, na "dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu ukishaanza hutaacha na itaendelea kukutafuna tu" Mwl. Nyerere. Kikwete alitumia mbinu mbaya zana kufika hapo alipo tusisahau namna Lowasa na Rostam walivyotumiua mbinu za kimafia kumfikisha hapo, kwahiyo yanayomkuta aliyatengeneza mwenyewe, kwahiyo hakuna wa kumuonea huruma acha yamkute.
 
  1. Kwa mtizamo wangu ni mtu aliyelemewa na wasaidizi wazembe na waongo wanaomdanganya na wasiopendana wao kwa wao na ni wanafiki.
  2. Moyo wa kuwatumikia watanzania anao ila vikwazo ktk mfumo inaonekana vimemshinda haswa ukizingatia mavuguvugu mengi (mfano kipindi kile wanataka wamuondoe kwenye uenyekiti wa taifa wa CCM) mpaka sasa anaiogopa sana CCM!
  3. Uongozi wake unatia shaka.
  4. Machoni pa watanzania walio wanyonge anaonekana ni msaliti.

Sio kweli, kwani wasaidizi nani anamchagulia? Hatuna rais kwa kifupi. Watu wanakwambia ukiona rafiki zangu wezi basi na mimi mwizi.
 
Huwezi kupewa shukrani kwa kutimiza majukumu yako ya kila siku ambayo unalipwa mshahara kwayo. Ila utalaumiwa na kuandikwa magazetini kwa kushindwa kutimiza majukumu yako uliyopaswa kuyatimiza. Na hiyo ndo habari.
Hakuna gazeti, litaandika leo Rais ameingia ofisini saa mbili na amefanya kazi zote alizojipangia. Hiyo siyo habari ha haiuziki.
 
Kunung'unika hakusaidii chochote! Wananchi walimkabidhi nchi na machinery zote kwa matarajio ya kuona mabadiliko chanya. Utamlazimishaje mwananchi aliyekuwa ananunua sembe kwa sh 250/kilo mwaka 2005 lakini sasa hivi anapata sembe hiyohiyo kwa zaidi ya sh 1000 pasipo ongezeko lolote la kipato; ktk hilo mwananchi huyo atawezaje kukupongeza zaidi ya kukuzogoa ama kukununia kabisa
 
M.mwanakijiji unaponuia kufanya jambo ni vema ukafanya kwa dhati na kusubiri kupongezwa au kusifiwa.mh rais amekuwa akifanya mambo kwa mtego kuona ni vipi atapongezwa,ni vipi atasifiwa.binafsi nampongeza kwa transparency leadership lakini si kipaumbele kwa watz,wanataka fursa za kujikwamua kimaisha zipatikane,wanataka wapate matibabu ya uhakika,wanataka kuona maamuzi yakitolewa yanayomgusha kila mtu,wanataka kuona kiongozi mbunifu kama kuna sehem tumekwama anakuja na alternative,sasa hayo hakuna watamshukuru kwa lipi sasa.uongozi ni kukubali changamoto lakini pia kutafuta majibu ktk changamoto kwake yeye ni tofauti anakuja na kuomba kuonewa huruma,je ndo dhana ya uongozi?watz wa sasa wengi wanauelewa juu ya nini serikali yao inatakiwa iwafanyie ili na wao watimize wajibu wao lakini imekuwa tofauti tuonacho ni kuwa ukitaka kuwa safe kwa ulaghai,wizi,ubadhirifu na ubabe vema uwe na madaraka maana hutoguswa na ndiyo maana watu hutafuta madaraka kwa gharama yoyote,sasa watz wasifie dhuluma?wasifie wizi?wasifie ubabe wawateule wake?kwakweli nijuavyo mimi kwa uelewa wangu wa kawaida nafasi ya urais si ya kusubiri makofi ya pongezi au vifijo vya sifa ama shukrani bali ni nafasi inayohitaji kuwa jasiri,usiyechoka kufikiri ktk pande tatu,mwenye wito na well committed na kazi yako,busara na hekima ya kipekee ndo kisima chake na mengine mengi mazuri.so ndg yangu mwanakijiji mh.rais na yeye akijua wajibu wake hatotumia nguvu kutuonesha zuri alilofanya tutaona wenye na tutaona anastahili kitu gani kama ni pongezi ama shukrani.kifupi anatakiwa kuwa visionary leader.
 
Hotuba zake tatu za hivi karibuni zimejaa manung'uniko na malalamiko ya mtu ambaye haeleweki, hapendwi, hasifiwi au ambaye hashukuriwi. Hotuba yake kwa wazee wa CCM wa Dar-es-Salaam baada ya mgogoro wa madaktari na hotuba yake ya Mei Mosi mbele ya wafanyakazi kule Tanga zinatuonesha hisia za mtu ambaye wananchi wake inaonekana hawamshukuru vya kutosha.

Katika hotuba zote tatu Rais amejaribu kutuonesha ni jinsi gani amejitahidi kufanya mambo kadha wa kadha ambayo kwa kweli watu wangemshukuru kuwa ameyafanya lakini inaonekana hashukuriwi. Ni hotuba ambazo zimejaa "tenda wema nenda zako" nyingi. Madaktari hawamshukuru, wafanyakazi hawamshukuru, wapinzani hawamshukuru, na hata wana CCM wenzake yawezekana hawamshukuru. Lakini pia kwenye hotuba ile ya mambo ya nishati ambapo alisifia serikali yake kufanya mengi katika kuzalisha umeme nchini kuliko serikali zilizomtangulia nayo pia ilijaa kutokuwa appreciated.

Ndio sababu najiuliza ni kweli yawezekana Rais Kikwete anaona Watanzania hawamshukuru vya kutosha na kuappreciate vitu alivyovifanya? Ni kweli Kikwete amefanya makubwa sana ambayo anapaswa kushukuriwa kwayo? Ni kweli kwamba Watanzania wanambebesha lawama kwa kumuonea tu japo "amejitahidi" sana kufikia malengo mbalimbali kulinganisha na viongozi wengine waliomtangulia?

Kama ni kweli amefanya yote ambayo anadai amefanya ni kitu gani basi kinawafanya Watanzania wasiyaona mambo hayo na kumpatia pongezi zaidi kiasi kwamba badala ya kuongeza kura zake mwaka 2010 alizipunguzwa kwa asilimia 20 hivi? Kwamba pamoja na yote mazuri anajikuta anashinikizwa kuvunja baraza, utawala wake ukilaumiwa sana na wananchi wakiwa na kiu zaidi ya mabadiliko na uongozi. Tumeona juzi hata baadhi ya viongozi wa chama chake wakimuambia waziwazi kuwa "awe mkali kidogo".

Labda tujiulize swali la ugomvi zaidi - ni uongozi gani ambao Kikwete anapatia taifa kiasi kwamba anafanya mambo mengi mazuri lakini analaumiwa zaidi? Yaani, anafanya mambo ambayo anaamini ni makubwa lakini mbele ya wananchi yanaonekana kama 'hakunaga'?

Yawezekana, we are missing to recognize the genius in our midst? are we that blinded by whatever to the extent that we can not appreciate the work of superb and beloved leader? Ni matatizo ya sisi wananchi kutomtambua yeye au ni tatizo la yeye kutotambulika?

Niliwahi kuambiwa way back nilipokuwa high school kwamba ukiona unapendwa sana ujue una matatizo wewe binafsi na ni jukumu lako kuyajua na kujirekebisha before it is too late. I believe the same applies to this man maana alipendwa sana miaka hiyo ya 90s na watu hawakumjua undani wake. Kuna wazee wangu waliokuwa wananiambia usije kukosea kumpigia kura kwani hafai huyu na mtajuta. Sikumwelewa kabisa. Kweli sikumpigia kura hata mara moja kwani sikuwepo nchini kipindi hicho alipogombea. Watu wajifunze kuwa wachunguzi maana kumpenda mtu haimaanishi anaweza kazi. Faza-House sasa yey ukisikiliza speech zake siku hizi analalamika tu na kusema utawala uliopita (ambao ulifanya much better kulinganisha na yeye au watawala waliopita) lakini anatakiwa ajue kakosea mahala fulani katika utendaji wake wa kazi. Professionals wanafanya kazi kufuatana na matakwa ya wanasiasa (rais akiwa mmoja wao) na hiyo haifai. Bot inafanya kazi kisiasa na ndio maana uchumi umekuwa mbaya kwa watu wa kawaida na hiyo haifai. Yako mengine mengi tu ambayo the current leadership imechemsha ndio maana watu wamekuwa wakali.
 
Mh. Kikwete,
Kinachomsumbua ni kutaka kusifiwa kwa mambo anayofanya, na hii ni hatari sana kwa kiongozi
Wananchi wanashindwa kumsifia kama anavyotaka kwa sababu hafanyi mambo ya msingi wanayotaka
Kama anataka asifiwe, awakamate wezi wa EPA, meremeta, TANGOLD, Kagoda na wengine aone kama CUF, CHADEMA na wanachi wengine hawakuandamana kumpongeza kwa kazi nzuri
Kama anahitaji sifa kutoka kwa waTanzania walalahoi arekebishe na kusimammia bei za bidhaa na mfumuko wa bei
Sifa ataipata tu mara SHILINGI ya mnyonge itakapokuwa na thamani aendepo kufanya manunuzi
Akizuia madini na maliasili zisisafirishwe kiholela nje ya nchi, waTanzania ninao wafahamu mimi watamsifia!
 
sidhani kama kwake yeye mwenyewe ime sink in kwamba kweli yeye ni rais. He is still dumbfounded. Atakumbuka shuka asubuhi tu
 
[QUOTE

Pengine kama kuna kitu ambacho bwana mkubwa Kikwete tutamkumbuka na kwa kweli kimetufikisha hapa pa kusema pasi na woga ni kukuza uhuru wa kujieleza...pamoja na kejeli zake pale awali kama vile kelele za mbu hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi, kwa kweli nafuu ipo kinyume na ilivyokuwa wakati wa Mr ANBEM co-founder(mh Mkapa ukipenda muite Mr Kiwira), Mzee Ruksa au Mwalimu.

Walau sasa tunaongea kwa uhuru mkubwa tu...kwa hili pongezi Rais wangu, mheshimiwa, Dk, Luteni Kanali Mstaafu J.M. Kikwete.

Nawasilisha.[/QUOTE]
Kusema kuwa ameleta uhuru wa vyombo vya habari huko nikumpa too much credit wakati hali halisi ni kwamba uhuru wa maoni umetokana na maendeleo ya teknolojia.Enzi za Mkapa,ni watanzania wangapi tulikuwa tunapata access ya mtandao?Kupiga simu ili kupeana habari na taarifa ilikuwa shida pia,unayetaka kumpa taarifa hana simu au yupo sehemu hamna mtandao bila kusahau gharama za kupiga simu enzi hizo.Hata Mkapa asingeweza kuzuia nguvu ya mitandao bila kugeuka kuwa the ultimate dictator.Kikwete angezuia vipi nguvu ya mitandao ya kijamii?Pia vyombo vya habari vilianza kwa kumsifia sana hivyo hakuwa na jinsi baada ya vyombo vile vile vilivyomsifia mwanzo kuanza kumponda.
 
wanaomgharamisha kikwete ni watendaji wake wanaodhani wamepewa nafasi zile kwa manufaa ya matumbo yao, lakn whatever he ave done, we are still blame on him because of his poor action to his assistances who ave got a number of scandals, which if he could act the nation could ave gone so far, yes he did, but it is upon his rensponsibilities, no need of waiting thanx while he is the one who contested, no one forced him, he also accumulate a lot from our taxes....
 
Mr President is the failure of himself, until now am failing to understand what was his motive running for the presidency. Sasa naamini mwalimu alivyosema uyu bado mtoto, hakumaanisha mtoto kwa umri but he meant mtoto kwa uwezo wake na uelewa wake wa kupembua mambo ni mdogo. Lakini mwisho wa siku wa kulaumiwa ni sisi wananchi why at first time tulimweka uyu jamaa? Naona yeye mwenyewe labda ashafanya assessment na kagundua approval rate yake is below marginal level sasa kilichobaki ni kulalama lalama tu.
 
Mr President is the failure of himself, until now am failing to understand what was his motive running for the presidency. Sasa naamini mwalimu alivyosema uyu bado mtoto, hakumaanisha mtoto kwa umri but he meant mtoto kwa uwezo wake na uelewa wake wa kupembua mambo ni mdogo. Lakini mwisho wa siku wa kulaumiwa ni sisi wananchi why at first time tulimweka uyu jamaa? Naona yeye mwenyewe labda ashafanya assessment na kagundua approval rate yake is below marginal level sasa kilichobaki ni kulalama lalama tu.

that is very true...
 
Humjui Kikwete1

Hotuba za Kikwete zote, ni fundisho kwa watu kama wewe wanaolalamika na kunung'unika kila siku lakini mnachonung'unika hakijulikani.

Hotuba aliyoongea na wazee kuhusu madaktari, licha ya kuwaelewesha kilichojiri, alitamba sana na hata kukejeli. Na mpaka leo tumeona madaktari ni kimya na wala hutowasikia tena wakilalamika. Huyo ndio JK.

Hotuba ya juzi umeona alivyowanyamazisha kwa kukurupuka na kudakia hoja kwa mafanikio ya jitihada zake.

Humjui Kikwete1
KIJANI: Pengine hatuna shukurani, lakini baadhi ya tunayoyanung'unikia ni:
1. Maisha bora kwa kila Mtanzania v/s
2. Mfumko wa bei wa kutisha
3. Giza totoro kila uchao
4. Madudu yake na ya watendaji wake (orodha kubwa)
5. Rais mtoro (Jenerali Ulimwengu).
6. Mawaziri na watendaji wa chini yao mapanya wanaokula noti (hili kalikubali hata yeye mwenyewe)...kwa kutaja machache tu.

BLUU:

Hizo ndio za Jamadari, Dk. Mheshimiwa Kikwete, kukejeli na kunyamazisha. La mwisho, "Ni upepo tu utapita".

NYEKUNDU:

Kweli hatumjui Dk. Kikwete. Kikwete huyu tuliyenaye sie yule tuliyemchagua kwa matumaini, aliyeahidi mambo lukuki akijua kuwa hayatekelezeki. Kulikuwa na haja gani ya kuweka ahadi 60 badala ya kushughulikia 4 za msingi:
1. Kuchagua watu watendaji na wajibikaji. 2. Mfumko wa bei 3. Umeme/Maji 4. Kuwawajibisha bila kuwaangalia usoni wa hapo nambari moja.

Lakini pengine Dk. Kikwete hakustahiki lawama zote kwani mambo TZ hayakuanza kuharibika leo, yalianza kuharibika tangu enzi za Nyerere. Kama alikuwa halijui hilo wakati anaingia madarakani, ninammuonea huruma. Na kama aliyajua, na alipaswa kuyajua, alikuwa na chaguzi mbili, ama anaingia madarakani kuyazuwia au asiingie kabisa. Uongozi si taasisi ya "trial and error", wananchi hawalifahamu hilo.

Licha ya kuwa TZ haikuanza kuoza leo, yaye ndiye aliyekamatwa na ngozi. Kwa kuwa kajikubalisha jukumu awe tayari kupokea lawama zote. Watanzania tuna wajibu wa kumsaidia Dk. Kikwete, wakianza wale aliowachagua. Sasa ikiwa wengi aliowachagua, ambao walipaswa kuwa kigezo cha kumsaidia na sisi kuiga, lakini wamemwangusha na yeye anawachekea, anawalinda, anawaogopa...
- Toka ameingia madarakani, ni madudu mangapi yamefanywa na hatua gani amechukua zaidi ya kubadilisha wabovu na kuweka wabovu zaidi?
- Kongozi anapothubutu kusema "hatuwezi kuwashitaki wabadhirifu kwani uchumi utayumba" unataka tumuelwe vipi?
- Kiongozi baada ya dhoruba ya hivi karibuni, anathubutu kukejeli "Ni upepo tu utapita" tumwelewe vipi?
- Kiongozi "anapofurahishwa tu umakini na uwazi wa wabunge" bila ya kuchukua hatua muafaka tumwelewe vipi zaidi ya kuwa anataka kutupoza ili "upepo upite". Bado tuna wajibu gani wa kumsifu kimtindo wa Zidumu Fikra za Mwenyekiti?
Nehi, nehi, nehi!!

Narudia kauli yako, ni kweli Hatumjui Kikwete.
 
Kikwete ajilaumu mwenyewe na sio watanzania wala hao wanaoitwa wasaidizi wake.

Hafanyi yale tunayotegemea ayafanye tutampongeza kwa lipi? sitegemei wanangu na familia yangu kwa ujumla wanipongeze kwa kuwapatia lishe bora, usingizi mnono, kuwapeleka shule bora na kupata mahitaji yao muhimu huo ni wajibu wangu kama baba, ila nataegemea wanilaumu kwa kutowatimizia mahitaji yao ya msingi kama hayo na badala yake najenga jina bar!na kwa majirani a.k.a small house!.

Tunategemea awe na uchungu na nchi hii, wale wote wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu tulitegemea wawe wamewajibishwa na sheria inafuata mkondo wake, huhitaji kusubiri ushahidi wa kutosha kumfukuza waziri, tetesi tu inatosha kumwajibisha na kusubiri ushahidi wa kutosha tayari akiwa pembeni, na hapa ndio maana sasa tutahitaji katiba mpya itupe majibu ya masuala kama hayo.
 
Tatizo moja la Kikwete ni kwamba mara nyingine anasahau kuwa yeye ndiye rais wa maamuzi na kujiona kama observer tu. Nakumbuka kuna wakati alisema asilimia 30% ya bajeti huishia mifukoni mwa watu. What did he do about it? Nothing. Halafu alipokuwa Davos akasema tatizo moja la uwekezaji ni kwamba mfumo wetu bila ya rais kuingilia kati hufiki popote. He is in a position do to something about it, but instead akawakaribisha wale waliokuwa wanamsikiliza pale Davos waje wamuone yeye ili mambo yao yaende sawa. Sasa which is which? Katika hili suala la mawaziri, kama kweli ni yeye alipendekeza ripoti ya CAG ijadiliwe bungeni, mbona hakuwachukulia hatua za mara moja mawaziri wake aliowateua mwenyewe? Kulikuwa na sababu gani za kuliweka taifa in suspense kama ilivyo sasa kuhusiana na kama mawaziri wanajiuzlu au hapana? Angefuta baraza la mawaziri mara moja Watanzania wangemuelewa, lakini hivi sasa inaonekana kuwa ni mchezo wa maigizo tu.
Jasusi

Kikwete hapendi lawama wakati kazi yake haikwepi lawama. Kama aliyaona madudu kwenye ripoti ya CAG ambayo alikuwa nayo tangu mwaka jana nini kilimfanya asi act hadi asubiri wabunge watake kumtoa ndipo aanze kuwasifu? eti na yeye amefurahishwa jinsi wabunge walivyowasulubu mawaziri, what a weak prezida is.

Lengo la hotuba yake ya juzi lilikuwa ni kujikosha mbele ya watu kwa kukwepa wajibu wake na kukwepa lawama endapo atawatosa marafiki zake. Lengo lake jingine ni woga alionao mbele ya chama chake, anataka kutuambia yeye hakuwa na nia ya kubadili baraza ila ameshinikizwa tu na wabunge, ni kama alikuwa anajikosha kote kote kwa wabunge, kwa chama na kwa wananchi, ili yeye azidi kupendwa.
 
Humjui Kikwete.

Laiti ungemjuwa usingeleta pumba ulizozileta.

Ni hotuba ipi aliyonung'umika kama utakavyo iwe?

Hotuba za Kikwete zote, ni fundisho kwa watu kama wewe wanaolalamika na kunung'unika kila siku lakini mnachonung'unika hakijulikani.

Hotuba aliyoongea na wazee kuhusu madaktari, licha ya kuwaelewesha kilichojiri, alitamba sana na hata kukejeli. Na mpaka leo tumeona madaktari ni kimya na wala hutowasikia tena wakilalamika. Huyo ndio JK.

Hotuba ya juzi umeona alivyowanyamazisha kwa kukurupuka na kudakia hoja kwa mafanikio ya jitihada zake.

Kikwete, hakupewa "favor" kuupata Urais kama ilivyokuwa kwa wote wa kabla yake. Kikwete alijuwa kabisa kuwa anataka awe Rais na alijipanga hivyo kwa miaka mingi sana na akaupata licha ya kuletewa mizengwe na Nyerere katika uhai wake.

Nakuona una haha kutafuta la kusema kuhusu Kikwete lakini ukweli ni kwamba hamumuwezi kabisa, kila afanyacho hufanya kwa maslahi ya wananchi na si ya kwake binafsi. Leo hii kikwete angekuwa na madudu japo asilimia 1 tu ya madudu ya Mkapa sijui kama angebaki kwenye Urais, maana mlivyomsakama si kidogo, lakini hamna zaidi ya kuzuwa tu na kutafuta kisichopo, mtatafuta sana lakini bure tu.

Humjui Kikwete, unamsikia tu na unamkisia, he is way too far ahead from your way of thinking. Wewe bado una fikra za kizamani sana, za wakati wa dhiki za chai kukorogwa kwa lawalawa badala ya sukari.

Mnajionea nafsi zenu wenyewe na ndio mpaka zinawafanya mnakuja kubwabwaja hapa hapa, ati "tunamuonea Kikwete", una ubavu upi wewe wa kumuonea Kikwete?

Humjui Kikwete1

Mkuu does it make any sense to you kuna issue ya madaktari anaenda kuongea na wazee? why? wazee ndio suluhisho la ubabaishaji na ufusadi wizara ya afya?

Unasema Kikwete angekuwa na madudu japo kwa asilimia 1, ni mzuri gani aliyofanya kwa aslimia 10? Natinal defence, natioanl unity, economy, security, finance, employement, (labda sports aliileta Real Madrid??? na Brazil), unenyekiti wa chama wewe mwenyewe unaona jinsi CCM ilivyo ovyo sasa, mara huyu anaongea yule anaongea mpaka wengine wanatukanana kwenye facebook.

Leading or ruling a modern state can be a daunting task, if you do not have what it takes to do so. JK presidency was not head on platter, it was nasty and dirty and that is what is costing us dearly at present. we had a lot of expectations, and we thought he was mesiah. He may be the best as you see him, but the trouble is, we have not seen the best of him, Mkapa was the worst but we managed to see the best of him.That is the difference.
 
Tatizo la siasa za Tanzania ni kwamba wale wote wanajiita ma "pundit" kama MMK wanaishia kuchambua mambo kihisia zaidi. Uchambuzi objective wa performance ya kiongozi haupaswi kusukumwa na yanayosemwa barabarani. Tunahitaji wachambuzi watakaozungumza kwa takwimu, watuambie:
1. Grafu ya uzalishaji umeme Tanzania ikoje tangu tupate uhuru. Halafu walinganishe kiasi cha uzalishaji umeme na ukuaji wa idadi ya watu.
2. Watuonyeshe ratio ya wanafunzi wanaograduate chuo kikuu to that ya wananfunzi wanaomaliza kidato cha sita.
3. Watuonyeshe mabadiliko katika vifo vya wajawazito na watoto tangu tumepata uhuru.
4. watuonyeshe takwimu za jinsi burden za magonjwa yanayoathiri maisha ya watanzania kwa kiasi kikubwa kama malaria na AIDS ilivyopunguzwa katika awamu mbalimbali.
5. watuonyeshe kilomita za barabara zilizojengwa katika awamu mbalimbali.
6. watutolee takwimu za vigogo wabadhilifu kuchukuliwa hatua katika awamu mbalimbali.
7. Watuonyeshe indicators za uhuru wa vyombo vya habari katika awamu mbalimbali.
8. watuonyeshe jinsi migogoro ya kijamii ilivyotatuliwa katika awamu mbalimbali.

Tuongee kwa takwimu, la sivyo tutakuwa tunapiga porojo tu.
 
Back
Top Bottom