Tunamuhitaji "Joey Greco" wetu katika kukabiliana na tatizo la "mpango wa kando/nyumba ndogo" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunamuhitaji "Joey Greco" wetu katika kukabiliana na tatizo la "mpango wa kando/nyumba ndogo"

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nzi, Apr 30, 2012.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,530
  Trophy Points: 280
  Salaam wana JF! Kwa sasa tatizo la "mpango wa kando/nyumba ndogo" limekuwa likiota mizizi kiasi kwamba linaonekana kama ni tabia ya kawaida kwa wanandoa na watu walio kwenye mahusiano. Tatizo hili katika jamii ya kitanzania, limekuwa kama ni "sifa" kwenye mhusika, hususani mhusika wa kiume; yaani sasa inaonekana kwamba, mwanaume mwenye "mipango ya kando" mingi ni "kidume - mwanaume kweli" n.k. Ingawa mwanamke mhusika, uonekana malaya - mwanamke hasiye na heshima na staha katika jamii husika - mchunaji n.k.

  Hali hii si salama haswa kwa watu walio katika ndoa, kwani mara nyingi hali hiyo husababisha ndoa kuvunjika (hivyo kuathiri malezi ya watoto, na kuleta madhara katika ukuaji wa watoto hao - hivyo kuleta madhara pia katika aina ya jamii inayojenga taifa) na pia kuleta magonjwa ambukizi kama UKIMWI n.k., hivyo kuleta pia madhara katika familia kwa ujumla.

  Vilevile hata kwa watu walio katika mahusiano ya kimapenzi (wasio wanandoa) - boyfriend-girlfriend relationship, nao hawaepukiki na hili wimbi la "mipango ya kando". Nao pia wapo katika hatari ya kuweza kupata maambukizi ya magonjwa, na hivyo kuleta athari katika mahusiano yao na pengine afya zao.

  Sasa Marekani kuna kipindi kimoja cha televisheni kiitwacho "Cheaters" - kwa tafsiri hisiyo rasmi - "Wadanganyaji katika mahusiano ya kimapenzi au ndoa". Hiki kipindi ni maarufu sana - lakini aliye maarufu zaidi ni bwana Joey Greco, mtangazaji na muongozaji (host) wa hicho kipindi. Joey, mtaalamu wa mambo ya saikolojia na ushauri nasaha, amekuwa akiendesha kipindi hicho kwa mafanikio toka mwaka 2002. Anajulikana zaidi kwa namna anavyoweza "kuwapoza" wanandoa au wahusika ambao wamefura kutokana na kugundua kwamba wenzi wao wamekuwa wakiwadanganya kwa kutoka nje ya ndoa au mahusiano yao.

  Kwa kutumia utaalamu wake amekuwa mara nyingi akiweza kutuliza vurugu, fujo na ugomvi unaotokea baina ya waliofumaniana; ingawa wakati mwingine uacha wahusika hao wachapane kidogo. Kwa kutumia watu waitwao "cheaters investigators" au wachunguzi wa siri - kipindi utoa nafasi kwa wanandoa au watu walio kwenye mahusiano, ambao wanahisi/wanadhani wenzi wao wanaweza kuwa wanatoka nje ya ndoa/mahusiano. Hivyo upeleka dukuduku lao kwa waandaji wa kipindi hicho ambao kwa kutumia hao wachunguzi, ufanya kazi ya kufuatilia mienendo ya mwanandoa anayehisiwa kutoka nje ya ndoa - uchunguzi waweza kuchukua muda mrefu hadi wiki moja - katika kufuatilia mienendo yake.

  Uchunguzi ufanyika kwa siri bila ya anayechunguzwa kufahamu - kwani wachunguzi utumia kamera na vinasa sauti katika kuweza kupata picha na mawasiliano ya anayechunguzwa. Kisha baada ya wachunguzi kujiridhisha kwamba wameweza kujiaminisha kwamba mhusika anatoka nje ya ndoa/mahusiano kweli, urudi na kutoa ripoti kwa mhusika aliyeomba uchunguzi ufanyike. Mhusika pamoja na Joey na timu yake ya wachunguzi na "mabaunsa" (katika kudhibiti ugomvi na vurugu katika fumanizi) uenda katika eneo ambapo aliyekuwa akichunguzwa yupo pamoja na "mpango wa kando/nyumba ndogo" ili kufanya fumanizi.

  Hapo ndipo kunakuwa na kasheshe na songombindo, kwa mara nyingi fumanizi uishia kwa ngumi na vurugu zinazofanana na ngumi. Wakati mwingine aliyefumania anapewa kichapo, wakati mwingine inakuwa kinyume chake. Na kipindi uisha kwa mhusika aliyeomba uchunguzi kuamua katika ataendelea na ndoa/uhusiano huo au la.

  Sasa kwa yale niliyoyasema mwanzo, kwamba tatizo la "mpango wa kando/nyumba ndogo" kushamiri Tanzania; hakika tunahitaji "Joey Greco" wetu na timu yake katika kuweza kukabiliana na vitendo hivyo. Hii ni biashara nzuri kwa wale wenye uwezo wa kuanzisha kitu kama hiki; kwani hii inahitaji uwe na mtaji wa kutosha - katika kuajili "investigators" na mabaunsa, kuwa na vifaa, kama kamera za kisasa (za kutosha), kuwa na pesa ya kuweza kufanya uchunguzi na kuwa-sustain wachunguzi kwa muda mrefu n.k.

  Hivyo kama mtu anaweza kufanya hivyo, hakika ni biashara ambayo atavuna pesa - kwani wanandoa na watu wengi walio kwenye mahusiano wanatamani "Joey Greco" aweze kuwasaidia katika matatizo ya "mpango wa kando/nyumba ndogo".
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Aya...aya...aya jamani!
   
 3. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,277
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Ni wazo zuri; Wajasiriamali mpooo. Wateja tunawasubiri kwa hamu.

  Ila inaweza kuwa ngumu kupata leseni maana viongozi wetu ndio kwanza wanashindana idadi ya vimada.
   
 4. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0

  ushafumaniwa mara ngap?
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kuchiti.
   
 6. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Joey Greco hawezi kufanikiwa katika TZ, wamarekani hawacheat sana kama sisi. I think we are over the record ndio maana majibu tunayaona magonjwa, jamii zinazopotea sababu ya malezi duni and etc. Wazungu akicheat anafanya siri, pale ambapo itajulika ujue ndio mwisho wa relationship or you have one more chance to go lakini kwa sisi hizi nyumba ndogo zinakuwa dhahiri na imeshakuwa ni kitu cha kawaida. Sometimes wote wahusika wanaweza kujua kuna nyumba # 2 somewhere or wote wakawa wanajuana.

  I think we are somehow lost case.
   
 7. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Hujambo Rose?
   
 8. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  unaonekanaga na msimamo sana juu ya hili,big up!
   
 9. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  biashara matangazo!
   
 10. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Usikate tamaa mama,nafasi ya ku redeem hii hali ipo.
   
 11. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Si kila king'aacho ni dhahabu!
   
 12. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  I love your avatar... I just do. lol
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Kuna member mmoja hapa alikuja akasema ameshaanzisha sijui kaishia wapi, ila mimi wasiwasi wangu ni kwamba twaweza kuwakamata viongozi wetu.....hahahaa sipati picha itakapofikia kwene confrontation
   
 14. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Thank you, mwanamke mapambo :)
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Acha kuhate bana
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Apr 30, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Mwanne Othman binti mwenye nyingi fani..
   
 17. M

  Mama Ashrat Member

  #17
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nampenda Joey Greco...
  Yuko fit sana kwenye fani yake.
   
 18. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #18
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Sijawahi kuwaza kuua mtu. Ila nitakapogundua kuna kijimtu kinafuatilia maisha yangu hasa ya siri, wazo hilo laweza kunijia. Sijui...
   
 19. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,530
  Trophy Points: 280

  nyumba kubwa. Mkuu hakuna haja ya leseni,kwa sababu ni kipindi kinatengenezwa na kwenda kuuzwa kwenye TV stesheni yenye leseni. Ni sawa na bwana Paskali Mayala anavyoandaa vipindi vyake na kuvipeleka kwenye stesheni fulani
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,530
  Trophy Points: 280

  MadameX. Huoni kama kipindi kama hicho kitabadilisha mienendo kwa kiwango fulani? Kwani cheaters watakuwa wakijiadhari wasije naswa na "Joey Greco" and company.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...