Waziri wa fedha aliyekaa wizarani kwa muda mrefu kuliko wote ni Amir Habib Jamal, alikuwa waziri tangu mwaka 1960 hadi 1985, kuanzia mwaka 1972 hadi 1975 alikuwa waziri wa viwanda na biashara kwa miaka mitatu tu alijenga viwanda zaidi ya hamsini vikiwemo viwanda vya ngozi na nguo, ndani ya uongozi wake tulishuhudia ukuwaji wa viwanda na uchumi wa Tanzania kwa hali ya juu. Hadi anaondoka wizara ya fedha thamani ya shilingi yetu ilikuwa shs 5 kwa dola moja ya marekani.