Tunamtaka Joh Makini wa 'Hao', huyu wa ni-come ndugu zake njooni mumchukue

kanali mstaafu

JF-Expert Member
May 17, 2015
4,319
4,089
Mimi ni mmoja wa mashabiki wa msanii Joh makini tangu anatoka akitengenezwa kuja kuchuana na msanii mwenye kipaji kuliko wote bongo (Chid benz).

Mwamba wa kaskazini alitikisa anga la mziki na kila mkwaju alioachia ulikuwa wa Moto ndio maana alipojiita Tz Jay z sikumbishia sana.

Nakumbuka ngoma zake kama Mfalme,Hao,muda,sijutii,Stimu zimelipiwa,Show za Joh,Kilimanjaro n.k, collabo alizopiga akangaa kama utaipenda ya Hussein machozi na nyinginezo.

Huyu Joh makini wa Weusi simuelewi kabisa yaan amepwaya katika uandishi kuliko zaman, hatumuoni kama Hip hop icon wa kaskazini yaani anakoelekea haeleweki kabisa.

Chondechonde tunamhitaj Joh Makini wa Hao, huyu wa madaraka,Nicome ndugu zake njooni mumchukue.
 
Upepo umebadilika zile hardcore hiphop sasa zinaonekana "haziuzi" tena in the sense kwamba wale wanaobakia na hardcore hiphop ni wale walio na misingi yao "economic resilience"cheki watu kama Watengwa recs. wao wamebakia na hardcoreHiphop kutokana na mahaba yao sasa kwa sababu ya "njaa" hardcore hiphop inatupwa kando japo ni mziki wenye kutoa uhalisi wa maisha ya "watu wetu" nafikiri ndio chanzo cha Joh na wengine wengi kufanya hihop laini.
 
Sidhani kama hawa jamaa ni watu wa kupenda ku expose their possession kihivyo mkuu...All in all wana progress flani ya maana tuu sio wa kufananishwa na Lord Eyes.
oouh labda kweli maana siwezi jua lakini mafanikio hayajifichi.

Namfahamu john vizuri saana achana na JOh wa kwenye kideo kama utapajua 360 utanielewa na mtaa wa jaluo walipohamia. Asante.
 
Back
Top Bottom