Tunamsaidia apone haraka au tunamsifia tu Kinafiki tupate Umaarufu huku kama vile tukiwa ' tunamchulia ' sasa afe kabisa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,617
2,000
Tupunguze Kumsifia ' Kinafiki ' na tujipange Kwanza katika Kumsaidia ili apone na arudi katika ' Game ' kama kawaida. Kwa tunaojua Imani za Kiafrika kumpamba na kumsifia Mtu ' Mgonjwa ' sana ni ' Uchuro ' Kwake na dalili mbaya za Kifo chake kuja. Huu si wakati wa kila Mtu kutaka Kujilikana haraka na Jamii kupitia Yeye ( Mgonjwa ) bali ni wakati wa ' Kumpambania ' mno ili arejee.

Kwa ninavyowajua Watanzania wenzangu hii ' Kampeni ' ya kumsaidia Mgonjwa wetu Waandaji wengi wataitumia katika ' Kupiga ' na Kujitajirisha na huhitaji kuwa na Elimu kubwa kujua au kuona kwamba inavyofanyika sasa imekaa ' Kinafiki ' zaidi na siyo ' Kiuhalisia ' zaidi.

Mgonjwa hakuanza Kuugua leo na nadhani kama kweli hawa ambao nawaona Siku mbili hizi wanajifanya wanamjua sana, wanampamba na kumsifu kuwa bila Yeye wao wasingekuwa hapo huku wengine wakijifanya kwamba hawana ' Uadui ' nae wakati Kiuhalisia tunajua wana ' Mabifu ' ya Kufa Mtu, je walikuwa wapi huko nyuma? Walisubiri azidiwe hivi, akose Pesa ( Msaada ) ndiyo leo wajifanya wanampambania?

Tupunguze ' Unafiki ' na nyie mchangine ila Mimi kwakuwa ni Mtani wangu mkubwa sana halafu sina Hela nitamsaidia tu kwa ' Mizimu ' ya Kwetu Mkoani Mara ambayo nitaiomba ' imponye ' haraka ili tusialikwe Kula Uji, Ndizi, Lubisi na Nyama huko Mkoani Kagera na Machozi yakitububujika.

Nawasilisha.
 

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
15,140
2,000
Na usijekuta kale kajamaa kenye kupenda kujibrand 'Msemaji wa Familia' kameshaanza kujiandaa kupitapita kakilabila na kujiliza kama ju-ha kwa unafiki.

Hatma ya mwanadamu huamuliwa na Mungu tu.
 

mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,082
2,000
Tupunguze Kumsifia ' Kinafiki ' na tujipange Kwanza katika Kumsaidia ili apone na arudi katika ' Game ' kama kawaida. Kwa tunaojua Imani za Kiafrika kumpamba na kumsifia Mtu ' Mgonjwa ' sana ni ' Uchuro ' Kwake na dalili mbaya za Kifo chake kuja.
Nani huyo funguka
 

Faru Kabula

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,178
2,000
Na usijekuta kale kajamaa kenye kupenda kujibrand 'Msemaji wa Familia' kameshaanza kujiandaa kupitapita
Si vizuri kukejeli watu wanaojitolea muda na rasilimali zao nyingine kutumikia misiba ya wengine. Ni makosa kudhani kila anayejitokeza kwenye misiba anatafuta maslahi yake, wengine wameumbwa kuwa na roho ya kutumikia watu
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,617
2,000
Si vizuri kukejeli watu wanaojitolea muda na rasilimali zao nyingine kutumikia misiba ya wengine. Ni makosa kudhani kila anayejitokeza kwenye misiba anatafuta maslahi yake, wengine wameumbwa kuwa na roho ya kutumikia watu
Rejea upya Kuusoma Uzi wangu kwani nina uhakika hujauelewa na ' umekurupuka ' nayo tu kama ' Kinyesi ' cha alfajiri.
 

Kete Ngumu

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
5,857
2,000
Badala ya neno unafiki ambalo limekaa kimipasho zaidi basi lengo lengwa la uzi wako mimi naweza kusema kwa lugha iliovaa nguo kuwa ni kampeni.
Binafsi wacha ifanyike hata kama kuna kuibiwa basi zitakazofikia malengo hazitokuwa haba kwa mgonjwa hasa familia yake ambayo ndio inajua uzito wa mgonjwa mwenyewe. Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 

BINOTO

Member
Oct 24, 2018
85
125
Kwa kweli hata mm nimeshangaa, kila kukicha huyu wala yule anasema lake. Wala aliniambia nifanye hivi wala vile, kwani imekuwaje? Kama kawasaidia ni issue ya kufungua wallet yako kimya kimya ili jamaa apone. Na kuna wengine wanasubiri kuna na ile issue ya pengo halitazibika nk nk.
 

BINOTO

Member
Oct 24, 2018
85
125
Kwa kweli hata mm nimeshangaa, kila kukicha huyu wala yule anasema lake. Wala aliniambia nifanye hivi wala vile, kwani imekuwaje? Kama kawasaidia ni issue ya kufungua wallet yako kimya kimya ili jamaa apone. Na kuna wengine wanasubiri kuna na ile issue ya pengo halitazibika nk nk.
 

kcamp

JF-Expert Member
Aug 31, 2014
6,788
2,000
Si vizuri kukejeli watu wanaojitolea muda na rasilimali zao nyingine kutumikia misiba ya wengine. Ni makosa kudhani kila anayejitokeza kwenye misiba anatafuta maslahi yake, wengine wameumbwa kuwa na roho ya kutumikia watu
Hakika bado hujamwelewa jamaa hapo

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
 

Mdomo bakuli

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
3,218
2,000
Tunajua na tunatambua kila mahali kuna unafiki! Hata huku ndani tumekuwa wanafiki kwa kila jukwaa! Kuna mtu atapost utumbo wake ila kwakua ni maarufu huku Jf basi kuna watu watamsapoti japo kinafiki!
Kuna waloguswa na mgonjwa wetu na wako tayari kuchangia kweli lakini pia kuwazuia wanafiki haiwezekani!
Wabongo unafik kwetu ni kwa karibu 98%

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom