Tunampenda kama Mama wa Taifa ila anahitaji public speaking training haraka sana!

Kila mtu ameumbwa na haiba yake,wapo wauza sura mbele ya macho ya watu,vyombo vya habari na wapo ambao kweli iko ndani yao hawezi kuuuza sura mbele ya macho ya watu mana lazima uweke kaunafiki kidogo.

Nafikiri sio sawa kila kukicha kumsema first lady wetu, katiba yetu inasemaje? yeye hakuuomba urais ili aje aongee na wananchi wake sasa kwa nini mumtake apewe mafunzo ya kuongea mbele za watu?
 
Nimekuwa nikimfuatilia kila mara tokea wakati wa Kampeni hadi Mumewe aliposhinda Urais na sasa kawa Mama wa Taifa rasmi ( First Lady ) ila nimegundua Mke wa Mheshimiwa Rais wetu Mama Janet Magufuli anahitaji mafunzo ya haraka mno ya kujua kuzungumza mbele ya hadhira kubwa kwani kila siku akipewa tu muda wa ama wa kusema chochote au kuzungumza amekuwa akinisikitisha sana kwani nisifiche wala kuwa mnafiki katika hili First Lady wetu hajui kuzungumza mbele za Watu ni si kitu kizuri.

Nitoe ombi tu kwa Wahusika kuwa hebu jaribuni kumpa basi mafunzo ili awe vizuri hasa katika kuzungumza halafu nimshauri tu kidogo Mama yetu Mpendwa wa Taifa ( First Lady ) kuwa aache kuzidisha kuwa mpole sana kwani naona kama vile upole wake muda mwingine anautumia eneo ambalo kimsingi hapatakiwi upole bali panatakiwa umakini ili kile anachokiwasilisha kilete mantiki mbele ya Umma.

Mwisho kabisa nimshauri Mama Janet Magufuli kuwa ajifunze kutofautisha kati ya kuwa Muumini wa TB Joshua na First Lady wa Tanzania kwani kwa majukumu yake ya sasa tunataka kumwona akiwa na umakini mkubwa pale anapokuwa anazungumza na Watanzania. Pia nimsihi tu aache kuzidisha kuwa mpole kwani kuna wakati huo upole wake anauonyesha mahala pasipotakiwa na kupelekea kutuboa.

Kila akipewa muda wa kuzungumza na Watanzania iwe ni Kanisani au Ukumbini au Uwanjani amekuwa akiharibu sana na hapa nisiwe mnafiki wala nisizunguke First Lady wetu hajui kuzungumza kabisa na kinachoniuma sana huyu Mama ni Mwalimu tena mzuri tu sasa nashangaa nini kinamfanya asiweze kuzungumza vizuri mbele ya hadhira.

Kama hatojali anaweza tu akawaomba hawa Wanawake wafuatao waweze kumfundisha kuongea vizuri mbele za Watu na siku zijazo asituboe tena na tukaanza kumtilia shaka:

  1. Mama Ananelia Nkya.
  2. Mama Hellen Kijobi Simba.
  3. Mama Jenister Mhagama.
  4. Mama Anna Mnghwira.
  5. Mama Regina Lowassa.
  6. Mama Magdalena Sakaya.
  7. Mama Sofia Mjema.
Naomba kuwasilisha na nitafurahi kuanzia siku chache zijazo nikimwona First Lady wetu Mama Janet Magufuli akitiririka vizuri bila kuona aibu, kuchekacheka na kuwa mwoga.
Uko sawasawa mkuu ataufanyia kazi ushauri huu.
 
Kwenye nchi hii kila mtu ana mama yake hatuna mama wa Taifa. Labda ni mama yake mleta mada.
 
Ila huyu uliyemtaja ( Former First Lady ) a.k.a Chinga kuna Mtu hapo juu kasema kuwa hata yeye nae hana tofauti na the current First Lady na labda tofauti yao ni majina yao huyu Janet na yule Salma ila udhaifu wao unafanana utafikiri wale Watoto Mapacha wa Mzee Reginald Mengi aliozaa na Jacklyn Ntuyabaliwe a.k.a K ya lini.
Gentamycine una vituko sana
 
Unaposema lets mind our own business unataka kutuambia nini labda? Naomba jibu lako haraka au upesi sana ili nami niweze kukujibu jibu litakalokufaa hasa kwa siku kama ya leo ya kufungua Vifurushi vya zawadi.

Sina haja ya kutafsiri sentensi yangu,ipo clear kabisa..

Na kingine,unaonesha wazi hilo jibu unalo tayari kichwani,sina haja ya kutafsiri kitu ili nikupe greenlight ya kulitoa hilo jibu lako...

Cha msingi litoe moja kwa moja uhitaji greenlight yoyote from anyone.

Acha kutisha watu,watu wenye mbwembwe sana kama wewe are the weakest available...ni upungufu wa akili kudhani mtu anaheshimika kwa matusi,watu wanaheshimika kwa wisdom and how they treat all people with respect.

I know where u are going,hey knock yourself out!
 
Back
Top Bottom