Tunamlaumu kiongozi mkubwa kumbe madudu yapo huku chini

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
992
1,000
Wakuu natumai mu wazima wa afya.

Kama mada inavyokuja ni huku kumlaumu baba yetu, kumbe huku chini kuna watoto hawawajibiki vizuri maagizo ya baba yao.

Ni hivi huku Wilayani Mbarali mjini Rujewa watu waliandikwa majina mwezi wa tano ili serikali ije itoe msaada wa vyandarua au net lakini cha ajabu mpaka leo wamepewa wachache, wengine wanaambiwa hawana vikaratasi vya kuwatambulisha kua walijiandikisha, sasa swali linakuja kwamba wao walivokua wanawaandika majina kwanini hawakuwapatia hivyo vikaratasi Wakawapatia wachache tu?
Hizo ndiyo sababu mojawapo za kuchukia viongozi wetu kumbe wapo wasababishi.

Viongozi najua mnapitiapitia humu, wafuatilieni hao wa chini wenu, hasa mabalozi, wenyeviti wa vitongoji ili muone hili zoezi kama lilienda kiufasaha.

Malalamiko hayo nimeyakuta kwenye mtaa au kitongoji cha Luwilindi mtoni mtaa ambao ipo ofisi ya TAKUKURU Rujewa Mbarali Mbeya.

Wakina mama wanalaumu kwanini waliandikwa majina, wanachezewa hivo wakati wao ndo wapiga kura wa kuaminiwa.
 

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
992
1,000
Hii habari naona waheshimiwa watakua hawajaiona au kwasababu wako busy na kampeni hawapiti kwenye uwanja huu, kazi kwao manaake mapungufu hayo ndo yanayosababisha wapate ugumu kwenye kampeni.
 

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
5,257
2,000
Ulitaka alaumiwe nani mkuu,kwani mwenye wajibu wa kuhakikisha wanawajibika ni nanai?
By the way ndio maana Upinzani kiujumla wao wanataka katiba mpya ili mambo mengine kama hayo madogo madogo wananchi wawawajibishe wahusika moja kwa moja bila kusubiri rais maana ilivyo sasa hadi ishu ya vyoo na madawati mara vyumba vya madarasa ni hadi rais asimamie,hii system ya kiutopolo ndio inatakiwa iondoke,chagua upinzani uache kulalamika
 

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
992
1,000
Ulitaka alaumiwe nani mkuu,kwani mwenye wajibu wa kuhakikisha wanawajibika ni nanai?
By the way ndio maana Upinzani kiujumla wao wanataka katiba mpya ili mambo mengine kama hayo madogo madogo wananchi wawawajibishe wahusika moja kwa moja bila kusubiri rais maana ilivyo sasa hadi ishu ya vyoo na madawati mara vyumba vya madarasa ni hadi rais asimamie,hii system ya kiutopolo ndio inatakiwa iondoke,chagua upinzani uache kulalamika
Mkuu hapo kwenye katiba nimekuelewa.
 

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
992
1,000
Ulitaka alaumiwe nani mkuu,kwani mwenye wajibu wa kuhakikisha wanawajibika ni nanai?
By the way ndio maana Upinzani kiujumla wao wanataka katiba mpya ili mambo mengine kama hayo madogo madogo wananchi wawawajibishe wahusika moja kwa moja bila kusubiri rais maana ilivyo sasa hadi ishu ya vyoo na madawati mara vyumba vya madarasa ni hadi rais asimamie,hii system ya kiutopolo ndio inatakiwa iondoke,chagua upinzani uache kulalamikaIla pamoja na hayo mkuu wanatakiwa warekebishe hayo mapungufu.

Mnawaandika watu majina halafu mnawapa wachache kwa kigezo cha kutowapatia vikaratasi vya utambulisho.

Sasa hao ambao hamjawapa vyandarua vyao mnataka muviuze hivyo vyandarua ili mpate pesa mifukoni?

Huo ni ufisadi pia au ukiritimba, mnatafutia pesa kwenye vyandarua vya msaada.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom