Konzo Ikweta
JF-Expert Member
- Oct 3, 2013
- 735
- 1,464
MFAHAMU BIBI CHRISTINA MGAYA WA NYANG'OMBE
Ameandika Francis Daudi
Hayati Bibi Christina Mgaya wa Nyang'ombe alikuwa mke wa tano(Kati ya wake 22) wa chifu Nyerere Burito. Hayati Bi. Mgaya ndiye mama mzazi wa baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Chifu Burito alikuwa kiongozi wa kabila la Zanaki wa Butiama wakati wa Ukoloni. Alitawala kuanzia 1912 mpaka mwaka Machi 30, 1942 alipofariki.
Inasemekana Bibi Mgaya wa Nyang'ombe alizaliwa mwaka 1897. Alijaaliwa kupata watoto sita ambao ni Nyerere (Julius)Kambarage, Nyangete Nyerere, Nyakahu Nyerere, Nyakigi Nyerere, Kizurira (Joseph)Nyerere na kitindamimba aliyeitwa Kiboko (Josephat) Nyerere.
Hivyo utaona mama huyu alikuwa na kazi kubwa ya malezi kwa watoto, akiwemo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuja kuwa baba wa Taifa letu.
Kwa sifa zake, Inaelezwa Bibi Christina Mgaya alikuwa mtu mwenye busara kubwa na aliyependa kuongea kwa mafumbo yenye kubeba mafunzo Fulani.
Hata Mwalimu Nyerere alipokuwa raisi bado bibi huyu aliendelea kushiriki shughuli za shamba na hata sherehe za utamaduni na watu wengine hapo Butiama kabla ya umauti kumkuta mwaka 1997.
Kulingana na Mzee Peter DM Bwimbo Katika kitabu chake kinachoitwa: ‘MLINZI MKUU WA MWALIMU NYERERE’ anaeleza kwamba Mwalimu Nyerere alimuheshimu sana mama yake, Bibi Mgaya Nyang’ombe.
Mara zote akiwepo Butiama, aliamka mapema kabla ya kufanya chochote alienda kumsalimu. Hata kulipotokea jambo ndani ya familia, aliheshimu kauli ya mama yake bila kujali madaraka yake kama raisi wa nchi.
Inaaminika alifariki akiwa na miaka 105( mwaka 1997) amezikwa karibu kabisa na kaburi la Chifu Nyerere Burito.
Ingawa maandiko mengine yanaeleza kuwa alizaliwa mwaka 1897 hivyo basi kwa mwaka 1997 angekuwa na miaka 100.
Kiufupi, Bibi Christina Mgaya wa Nyang'ombe ni sehemu muhimu sana katika uandishi wa historia ya Tanzania.
Yeye ni kati ya WANAWAKE waliosahaulika kabisa katika kurasa za historia yetu lakini ujenzi wa TAIFA hili uliitaji mtu aliyepitia malezi muhimu hasa utotoni. Ambaye alifunzwa tangu utotoni kupenda watu, kutetea watu na kuamini katika Misingi ya HAKI na USAWA.
Bila shaka elimu hii hakuipata kwa kumsoma KARX MARX au PLATO, ilianzia kwa mama ambaye hakupata kabisa elimu rasmi. Ila mwenye ucheshi, mkarimu na upendo wa hali ya juu. Huyu ndiye mama yake Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere