SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,104
- 7,857
Mmabo mengi waumini wenzangu tunayafanya kwa ama kutofikiria au kwa kuiga iga tu bila kutazama mantiki zake.
Imeibuka hii tabia ya kucheza mitindo ya kwenye disco na sehemu za ufuska na maovu mengine tukiwa madhabahuni. Juzijuzi nimetoka kuona video vijana wanatwanga sijui ndiyo Amapiano ile, wanabambiana kabisa madhabahuni, tena wakiongozwa na mchungaji wao. Hii siyo sawa. Najua nia ni kuwavutia vijana waje kwenye ibada na majumuiko mengine ya vijana ila Mungu inabidi abaki kuwa Mungu.
Napenda jinsi Wayahudi (na labda niseme hata Waislamu) wanavyoheshimu ibada na sala zao. Hawachanganyi madesa, kwanza wana muda maalumu, pia kuna mavazi maalumu, na hata jinsi ya kusali tu inaonyesha hili ni tendo la kipekee. Sasa wenzangu na mimi kila kitu mpela mpela tu.
Turudi tujitafakari ndugu zangu.