Tunamchangia Prof J kwa sababu tunampenda au hana uwezo wa kugharamia matibabu au nimazoea?

Kaka mwisho

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
402
164
Kwasasa hapa nchini pamekuwa na utaratibu mtu akipata matatizo tunakimbilia kuchangishana fedha.

Mtu kama Joseph Haule a.k.a Prof J alipopata maradhi na kulazwa, familia yake ikaomba achangiwe kusaidia gharama za matibabu, bila shaka familia hawana uwezo wa gharamia matababu kutokana na maradhi yanayomkabili.

Sasa mtu kama Prof J anachangiwa, je kuna Watanzania wangapi ambao hupoteza maisha kwa kushindwa kugharamia matatibabu na hawana nafasi ya kuchangiwa.

Tupiganie Bima afya kwa wote yenye uwezo wa kugharamia magonjwa yote kama ilivyo kwa watumishi, hii ya kuchangiana iwe kama ziada na isiwe ndio mkombozi.

Mkombozi iwe BIMA YA AFYA na tuchangiane kama dhararu tu.
 
Yote yanaweza kuwa majibu. Na pia hongera kwa kutoa wazo zuri, na ambalo limekuwa likipigiwa kelele kila siku! Lakini utekelezaji wake kutoka serikalini ni 0.
 
Wadau na mataifa mengi Duniani yalichangia kwenye tetemeko la Ardhi mkoa Kagera ,na Hadi Sasa wanaendelea kutuchangia madarasa na vyoo vya shule,He hatuna uwezo Kama Taifa?
 
Kumchangia prof ni sahihi mana waliomba kama familia , milion 4 per week sio mchezo kwenye matibabu unatakiwa uwe fisadi haswa, ni kweli redion kila week huwa naona kuna vipind vya majanga ya namna hyo na watu huwa wanasaidiwa, mfano redio free Wana kipind kila jumapili asubh , clouds wao Wana njia panda.

Hata hvyo ukweli unabaki pale pale maelf ya watanzania wanashuka kaburini sababu ya huduma mbovu mahospitalini na Gharama kubwa za matibabu, naunga mkono hoja bima ya Afya Kwa wote itasaidia Sana
 
Hakika umenena mkuu. Bima ya afya ndiyo suluhisho la kuomba kuchangiwa. Kuna watanzania wengi mno wasio na uwezo na siyo maarufu kwa majina au kazi zao wanaugua wanakufa kwa kukosa kumudu matibabu. Ili kuondoa hali ya kuhisi tumetengwa basi serikali ijitahidi kuwezesha watu kupata bima ya afya
 
Usiwe na matumaini makubwa katika bima ya afya kwa wote katika hizi nchi utakuja kufa na kikadi chake kwenye msuli tafuta hela na punguza kuhonga kama huwezi kuacha na tumia akili nyingi katika kuwekeza
 
Usiwe na matumaini makubwa katika bima ya afya kwa wote katika hizi nchi utakuja kufa na kikadi chake kwenye msuli tafuta hela na punguza kuhonga kama huwezi kuacha na tumia akili nyingi katika kuwekeza
Mawazo haya ni next level
 
Back
Top Bottom